Akili ya binadamu

fanya hivyo mkuu usiwe na haraka kabisa.
 
Mkuu OMOYOGWANE
Kuna mechanism gani ya mtu kujua kuwa hapa nilipo naota..
Yaani nipo ndotoni lakini najua kuwa hapa naota..
Hii inanitokea sana..?
 
Pia kuna issue inayoambatana na tatizo la stroke yaani kupooza. nayo ni NEUROLOGY. Kwenye eneo la kufahamu uwezo wa AKILI, tunawezaje kumfanya mtu anayepoteza kumbukumbu kupitia tatizo la neurology kurejea kwenye hali ya kawaida.

Ukirejea, jibu swali hili pia la uwepo wa immaginary cloud kwenye kila akili ambapo kumbukumbu zinahifadhiwa. kKule kwenye pg ya kwanza ulisema kuwa memory zinaweza kufutwa... how?
 
Mbona point ya mwisho umepalasa?
 
Mkuu hapa napingana na wewe kwenye hilo swala la kuamka na kuandika huo msamiati, kiukweli kabisa binadamu tuna sehemu mboli za memory storage ambazo ni temporary and permanent storage, hiyo temporary ni ile ambayo mtu unaihifadhi kwa muda mfupi tu baada ya kuona au kusikia kitu na hufutika haraka sasa ili kitu kiende kwenye permanent storage unahitaji kurudia rudia mara nyingi hilo jambo either jina la mtu,namba ya simu,sura,maneno,njia,nyimbo etc. Sasa wewe hilo neno la kiingereza sio kwamba lilikuja tu automatically bali kuna sehemu uliliona au kulisikia ila kwa kuwa hukulitilia maanani basi ubongo ukahifadhi kwenye temporary storage , hii pia hutokea sana kuna kipindi unakuta umeota ndoto na kwenye hiyo ndoto kuna sira ngeni tu ,hiyo pia sio bahati mbaya ni kwamba ubongo uli store picha za watu wakati unatembea so during bedtime hizo memories zinaanza kuji play
 
Mh. Hakuna tatizo linaloitwa neurology...!!
Neurology ni muunganiko wa masomo/mafundisho yote yanayohusu neurones/mfumo wa fahamu wa binadamu/wanyama! Ni sawa na masomo yahusuyo urology, oncology, orthopaedics n.k,
Pia kupoteza kumbukumbu halijawahi kuwa tatizo, tatizo ni unapoteza kumbukumbu kwa kiwango gan...!!?
The creator/mother nature vyovyote unavyoita na kuamini! Aliweka memory loss purposely, laiti kama kila tunachopitia kuona, kuhisi, kusikia, kugusa na kunusa memory zake zingekuwa permanent hii dunia isingekalika!
Lakini mother nature through memory loss ameneutralize mambo!
Kila kitu kwenye mwili wa binadamu kina ideal condition yake kikipungua au kikizidi ndiyo tunaita tatizo sasa,
mfano blood pressure, ikiwa juu ya wastani ni tatizo na ikiwa chini ya wastani pia ni tatizo,
Sukari(sugar/glucose) ikiwa juu ya wastani ni tatizo na ikiwa chini ni tatizo pia...!
Umewahi kujiuliza kwanini na kwa namna gani magonjwa(diseases) au disorders zinatokea??!



Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Mwenzetu aliyetoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa fahamu na ubongo, amejitahidi sana kutokuwa biased hasa pale alipoliweka somo hili kwa mtindo wa maswali...!
Amefanya somo limekuwa rahisi kueleweka kwasababu, kuna mtu anauliza swali linalofanana na mfumo wa fahamu lakini specific limebase kwenye socialogy, au psychology, au psychiatric, au neurology, au imani za kidini kabisa...! Mtoa mada endapo kama angeanza kuleta desa moja kwa moja asingeweza kukata kiu za hawa wasomaji wote...!! The nerve system is a complex system amongst!
Mungu ameweka mifumo mbalimbali ili mwili wa binadamu ufanye kazi vizuri lakini mfumo wa fahamu ndiyo baba lao...!!

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…