Kwanza kabisa inapasa uelewe kwamba kuwa na ELIMU sio kuwa na AKILI kiongozi.
Unaweza kuwa na ELIMU kubwa tu ikawa HUNA AKILI mkuu.
Kwa hiyo basi, sina hakika kama huyo jamaa aliwehuka kwa ajili ya hiyo ELIMU yake aliyokuwa nayo. Inawezekana ikawa ni sababu nyingine kabisa ndio iliyofanya akawehuka kiongozi wangu, ila katika macho ya kawaida ukaona tofauti na kufkiri kuwa labda ELIMU aliyonayo ndio iliyomfanya akawehuka.
Ila kiuhalisia katika swali ulilouliza ni kuwa AKILI ikizidi sana sidhani kama inaleta madhara ila itategemea umeangalia katika mtazamo gani na pia vile jinsi utakavyoutumia uwezo wako wa AKILI. Ila kuna msemo tu unasema kuwa AKILI NYINGI HUONDOA MAARIFA.
Thanks a lot.
SAHIHI.
Kwa hivyo tunaweza kuzungumza juu ya ELIMU kwa nyanja tatu za ubayanifu wa kiuono mifumo:-
ELIMU 1.0 : Kujua Kusoma na Kuandika
ELIMU 2.0 : Uono na Ufikirifu Mifumo
ELIMU 3.0 : Ilimu ilivyo ni metafizikia ya elimu
Neno hili asili yake limetokana na Lugha ya Kiarabu na ndipo likaja kwenye Lugha yetu ya asili ya Kiswahili, limeanza kutumika tangu karne ya 7 takriban ni miaka zaidi ya 1200 kabla ya kuzaliwa Lugha ya Kiswahili. Na mfano wa matumizi ya neno hili AKILI lilishatumiwa na MTUME MUHAMMAD (S.A.W) aliposema kuwa ; MAKTASABAL MAR-U, MITHLA A'QILI akiwa na maana kuwa HAJACHUMA AU HAJAPATA MWANADAMU KITU KILICHOKUWA BORA MFANO WA AKILI. Kwa kauli hiyo tunaweza kuona kuwa neno hili kumbe limeanza kutumika miaka mingi sana iliyopita kabla halijaja kwenye Lugha yetu ya Kiswahili. Na kwa kauli hiyo pia tunaweza kuona kuwa kumbe kati ya vitu vyote ambavyo mwanadamu atafanikiwa kuvipata katika MAISHA yake hakuna kilicho bora kati ya hivyo kuushinda ubora wa AKILI, hata awe na mali vipi kama hana AKILI basi ni KAZI BURE TU na hata WASWAHILI wakafikia hatua ya kusema kuwa "BORA UKOSE MALI UPATE AKILI.
Mash'Allah.
'Bora Ukose Mali Upate Akili'...
Namna gani hili ni ukweli mtupu?
Kitendawili hichi kinateguliwa na 'ELIMU 2.0'... Uono unafanyika kwa, vina vya tafsiri kwa mafikara juu ya mifumo na dhamira ya utu katika kujifunga na jambo la mwanajamii/jamii kwa ujumla. ELIMU 1.0 ndiyo iliyotamalaki katika ulimwengu wa leo, hii ina adha moja: ina 'ujuu juu' wa tafsiri za mambo na utetezi wa 'siasa za mkumbo' kwa sura na mienendo ya jamii. Ni ulimwengu wa 'vipofu kuongoza vipofu wenzao' kwa uratibu wa maoni, fikra na 'hisia za nje' za mwanadamu na hata 'visomo 1.0'...
ELIMU 2.0 inatuletea fremu-kazi ya uono na ufikirifu mifumo inayoweza kuchochea mabadiliko katika 'uratibu wa fikra', 'uono' na 'vina vya tafsiri' na basi kuweka hadharani mahusiano na maingiliano ya 'akili' na 'tabia' zetu kama wanadamu wenye AKILI. Hili linakuja na 'visomo 2.0' ambavyo koherensia ya ufikirifu 'inajengeka picha' kwa topolojia na topografu ya kubaini miktadha ya mambo ya mwanajamii/wanajamii.
ELIMU 2.0 itaumbua mapungufu ya 'mifumo dume' na itaonesha njia kwa ukweli wa kuishi, liberiti na udhamirifu wa furaha... Itatunasibu na namna mpya ya uchumi ambao ulikuwa ni 'njozi ya waasisi' wa taifa hili la Tanzania. Jambo ambalo kwenye katiba yetu ya sasa linatajwa kwa nasibu ya mapelekeo ya matatu:-
- 'Kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake';
- 'Matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi';
- 'Shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinaweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi';
Utajiri wa Taifa, ni pamoja na '
akili'--za wanajamii zisizo na kasumba ama kule kutokuona mambo kwa fasaha ya kweli za vina vya tafsiri... Kuna yanawezekana kufanya hata sasa na leo na tukabadilisha 'hali' zetu; pasi kubidi kufikiri eti labda mpaka 'tuwafundishe watu' kwa kiingereza basi ndipo 'maendeleo' yaje kesho...
Ni ELIMU 2.0 ndiyo inaweza kufungua tafsiri na mielekeo iliyojificha hata kwenye Katiba yetu ya sasa. Kwa mfano, je, kuna uhusiano upi hasa wa 'Utajiri wa Taifa' na 'Umaskini, Ujinga na Maradhi'?
Je, kuwa na madini, mbuga za wanyama, mito, maziwa, bahari, ardhi yenye rutuba ni 'utajiri'?
Basi kwa ELIMU 1.0, vitu ni 'Utajiri' pasi kujali mtu ana akili yenye maarifa sahihi ama visvyo; ila kwa ELIMU 2.0, Utajiri 'si mali hasa' bali >
akili za watu 'ndiyo rasilimali'< katika mchakato wa maendeleo ambavyo 'mtu ni kitu' kwa 'ndani na nje'...
Utajiri inawezekana kuwa ni 'Hisia, kujiridhisha na amali zako ama na fikara la kujichukulia kuwa mwingi wa mambo' kadiri ya upeo wa akili yako--na huku 'akili yako' inaweza ikawa 'si yako' bali ya 'kuazimwa'... Ni ule uthamani unaoujengea akilini mwako kutokana unavyoamini ama kusadiki nini maana ya kuwa 'tajiri'.
Mtu wa ELIMU 1.0 hawezi kubaini anaishi na akili ya 'kuazimwa'--kwa kule kaambiwa huo ni 'utajiri'--je, 'utajiri' maana yake 'ni wewe kuwa na vitu kwa wingi' na hali 'wenzako hawana hivyo vitu' labda?
Mtu wa ELIMU 2.0 anaweza 'kushtukia chezo' juu ya 'adha ya kufuata mkumbo' pale anapoanza 'kufikiri hasa'--kama ‘mtu pekee’ katika 'halmashauri ya kichwa chake'; na kuepukana na kule kuwa' jalala' la mafikara ya wengine juu ya uthamani wa mambo ya jamii...
Mtu asipokuwa makini, anaweza kudhani kila kinachosemwa na 'kiongozi' ni sahihi ama cha kufuatishwa tu, kinachosemwa na 'Wataalam' ni cha ukweli pasi shaka, kinachosemwa na 'Mwanasayansi' ni cha 'kumaliza ubishi' na Shuhuda za 'Matajiri' ni 'siri za mafanikio'; haya yote yanaweza kudanganya mtu katika visomo 1.0 lakini kwa uono na ufikirifu mfumo, ni rahisi kubaini sura pana ya mambo na mahusiano yake ya kweli badala ya ukomo wa fikra rahisi na tafsiri...
Rasilimali hufungamana na upeo na vipawa vya utambuzi. Mtu aweza kuwa na vitu kadhaa katika mazingira yake asijue kumbe vinaweza kutumika hivi ama vile-- na hivi kuweza kubadili ubora wa mazingira yake ya kuishi; na basi hivi hivyo vitu vitakuwa si 'rasilimali' kwake kwa wakati; mpaka yeye ajifunze ama kutaamulika kwa muktadha fulani...
Katika ngazi ya usawa, mapana na upande wa jambo hili ndiyo tunaitambua Elimu kama shughuli adhimu katika kuchochea ujuaji-- kudumisha maarifa na kutunza muktadha wa kuelimika zaidi katika utambuzi wa mtu. Hakuna haja ya kupamba shughuli ya elimu kama ni 'funguo ya maisha' ya mtu... Funguo hasa ni 'dhamira' ya mtu katika kuona umuhimu wa kujifunza na yale 'makusudio' yake katika kutafuta mbinu za visomo--kuufaa ustawi wake. Na hapa ndipo tunaweza kupata tafsiri rahisi ya maendeleo...
Maendeleo ni Kuchachuka kwa dhamira ya mtu kunakogeuzwa ni harakati za kubadili mazingira yake, kwa 'upeo' na 'imani' yake, juu ya jambo fulani... Kwa kuwa ni fanusi--kile katika lugha ya kiingereza hutajwa ni 'function'; ya imani imtiaayo mtu tumaini katika juhudi na bidii, ama hata kwa sura ingine, tumaini la mtu katika ule uvumilivu na ustahimilivu. Na hivi fanusi ya elimu pia ni kutimilisha udhanifu wa mtu kusudi tumaini lake lisiwe ni bure... Kwa kuwa, Imani ya mtu ikijishikiza katika uadilifu wa kimawazo ulio katika sehemu ya ukweli unaofanya mambo, basi mtu mwenye imani anaweza kuvuna matunda yenye kheri na ubarikika kulingana na imani hiyo; na ikiwa imani haiko katika uadilifu wa kweli mtu huja kuvuna matunda mabovu ya hasara kwa uvumilivu, ustahimilivu, juhudi na bidii zilizokuwa ni batili...
Rasilimali ya mnyonge si umoja hasa--ni minajili ya kuunganika katika 'kufikia ngazi' na 'hadhi ya daraja' la ustawi kwa mbinu na maarifa sahihi; si idadi tu ya watu.
Muktadha wa Elimu na Imani hauna budi kumulikwa katika kutokomeza ile sumu ya Utaasisi Mbofu na Michezo mitupu isiyo asili ya mwangaza halisi--ule wenye kuweza kukomboa watu toka kwenye 'harakati popo' za mikumbo na sarakasi za mifumo. Kwa kuwa mifumo yaweza kuwa si kitu ila tu vituo vya Ujinga.
ELIMU 2.0 inatuletea busara ya >
'ujazi'< pale tunapojichanganya na dhana za 'utajiri' katika visomo na ELIMU 1.0.
Na basi tutazame fremu-kazi ya uono na ufikirifu mifumo kwa taasisi za jamii, sura na mienendo yake kwa >
pembe tatu ya akili<.
Fremu-kazi hii ya Uono na Ufikirifu Mifumo inaweza kubayanisha >
'maarifa yoyote'< ya jamii...
ELIMU 2.0: UONO NA UFIKIRIFU MIFUMO JUU YA OGANAM YA NJIA YA TATU
'Kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake';
'Matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi';
'Shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinaweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi';
Tukienda mbele kidogo, kuna uwezekano tukaja kubaini sarafu ya kidijitali inawezo mkubwa wa kusapoti ubunifu, usimamizi/uendeshaji wa viwanda vidogo kwa vikubwa, na mtanuko wake, huku ikitatua moja kwa moja adha za 'mfumuko wa bei' katika uchumi. Hili litawezekana kupitia na 'mifumo ya mumo kwa mumo' ya makato, hifadhi, kodi na mahitaji -- ambayo inaweza kubuniwa kwa kutangulia kama mpango wa shughuli/biashara, kuakisi ukubwa wa shughuli yenyewe na mapana yake ya 'ukubwa' na 'muda'. Siku sijazo, kila shughuli itaanzishwa kwa marefu na mapana--muda ukifika, kila shughuli lazima igawanyike na kuwa mbili... Kulingana na mpangilio wa menejimenti na wanaoperesheni kazi, ipo namna tatizo la ajira linaweza kutatuliwa 100%...
Jamii ambayo kila mtu mwenye kuweza kufanya kazi anayonafasi ya kujishughulisha kikazi INAWEZEKANA.
Sahau yote unayosikia kutoka kwa wataalam: Wa-uchumi, siasa, uongozi na maendeleo ya jamii kuhusu 'usugu wa tatizo la ajira'... Ukiamini hili unadanganyika, na unakuwa umejinasibu na ufikirifu pofu wa kimakundi. Elimu 1.0 haina suluhu ya 'matatizo ya ajira' kulingana na paradamu ya leo hii ya uchumi na maendeleo. Na kama tumefika hapa kwa 'akili' ya wataalam wetu wa visomo 1.0, basi tujue kufika hapa ndipo 'utaalam' wao wa Elimu 1.0 ulipogotea.
Kama alivyopata kusema Mfizikia Albert Einstein, >
hauwezi kutatua matatizo kwa akili ile ile iliyoyaleta hayo matatizo<... Visomo vinavyoanza michukulio ya ukosefu na mapungufu, iwe kiuchumi--dhana kama ujadilifu kwa 'rasilimali haba' n.k. haziwezi kujinasibu kitopografu na visomo vya 'ujazi'.
Walter Russel alikuwa sahihi: dunia hii, udunya ni maradhi ya kujitakia, akilikubwa ni kujipa mwenyewe, akisema kwa maneno yake: >
"mediocrity is self inflicted, genius is self-bestowed"<...
Dhana ya 'uhaba' ama 'uchache wa rasilimali' hujifunga na uwezo wa akili katika kubaini 'maarifa sahihi' na 'mbinu za kazi'. Kwa kueleza hivi, inapelekea ukweli wa kwamba 'mbinu za kazi' na 'maarifa sahihi' yanaweza kuyeyusha tafsiri za uhaba ama uchache wa rasilimali. Fikiria kwa mfano, upo kwenye nchi ambayo imepakana na bahari lakini watu wake wanashida ya maji. Je, ikiwa yapo maarifa ya kuvuta maji ya bahari, kuchuja chumvi, kutunza kwa wingi na kusambaza kwa jamii, 'uhaba wa maji' utahusikaje na mashauri ya uchumi na huduma za jamii?
Vivyo hivyo, fikiria kana kwamba ipo suluhu ya >
vinu vidogo vya nishati< ambavyo vinaweza kufungwa katika kila nyumba za wanajamii, vikitengenezwa kwa bei chee ama hata tu watu wenyewe kupewa tekinolojia na basi wakatengenezea vinu hivyo kwenye karakana na majumbani mwao, je, uhaba wa nishati na siasa za nishati jadidifu 'zitaishi wapi'?
Fikiria, vyombo vingi vya moto, vya uchukuzi, >
kufanyiwa utundu fulani mdogo< na basi badala ya kutumia 'mafuta' kama petroli vikawa vinatumia maji, je ulaghai na porojo za uchumi wa nishati fosili 'utaishi wapi'?
Haya matatu yaliyotajwa, ni machache tu ya mfano; na yote yanawezekana tena kwa hata maarifa rahisi tu--je, watu wanadhani kwa sababu yanakanushwa na 'wataaalam'; hata kupitia mikakati maalum ya utumikivu wa vyombo vya habari -- kutokea kwenye idara za usalama (nishati na rasilimali) wa mataifa karibia yote ulimwenguni, basi 'tuwe wapole'?
Sasa, tatizo hasa kwa nini haya 'hayaruhusiwi' ni kwa sababu ya mifumo ya uchumi, maisha na maendeleo ya jamii kupambanisha na hizo suluhu 'havivaani'. Hayo yakiachiwa hovyo bila kuthibitiwa, uchumi kama tunavyoujua leo hii 'utavurugika'. Watu wengi wanaojificha nyuma ya idara za usalama(nishati na rasilimali) wamekosa maarifa ya 'mitigati' kwa majanga ya kiuchumi yanayoweza kutukia ikiwa baadhi ya 'suluhu' za namna hii zitaachiwa hadharani, sera za 'nishati na usalama' huchukulika ni jambo nyeti katika mataifa ya leo hii (Jan, 2023)--japo zina ushamba wake, 'roho ya uchoyo' na vile vile vitisho vya chini kwa chini kutoka kwenye mataifa ya kibeberu. Na hata waliodhani 'wanayomawazo na mapendekezo' kama kawaida wameishiwa 'kubezwa'...
Sasa siyo kwamba hakuna mtu hajawahi kuvumbua 'mifumo' ya namna hii: >
Watu na mifumo ya namna hii VIPO<.
Lakini hili ni suala ya 'Usalama wa Taifa'-- Sera za 'unyeti wa Nishati' na 'Mazingira' katika Nchi nyingi duniani…
Mataifa mengi wanazo tekinolojia zenye kuweza kupindua kila kitu tunachofahamu kuhusu uchumi wa mafuta, fedha na maendeleo... Lakini wanakausha.
Kwa wanaojua ukweli wa mambo hayo, na wandani wa haya, wanaweza kutoa hata sababu hizi ama zile, eti ni kwa nini jambo fulani la ugunduzi libaki siri.
Marekani ipo kabisa >
sheria inayoruhusu serikali kupokonya mtu anayevumbua vifaa visivyo vya kawaida vya nishati kwa muhuri wa 'Usalama wa Taifa'<, lakini mataifa mengine hufanya hivyo hata kwa kutumia 'Makachero' maalum--Italia, New Zealand hata Afrika ya Kusini...
Kwa mwenye hekima, sababu zao zote juu ya jambo hilo ni ubatili. Kwa kuwa hayo yote si lolote bali 'roho ya uchoyo' na >
'akili ya kimaskini'<....
Watu wenye kuhodhi tekinolojia za kimapinduzi wanajidai kuhofia 'kupoteza nguvu ya ushawishi'.... Na hakuna 'mtu kati' anayeweza kufanya tathmini ya kutosha ya mapelekeo kuachia ugunduzi kwa umma --yaani ni jinsi gani mifumo mingine yote ya stawi na tawala itakavyoathirika ama ikiwa kuna namna za kufanya ili kurekebisha adha zake mfuatano....
Wanasiasa na 'walioko madarakani', kwa sehemu kubwa hapa duniani, hawako tayari kulipa gharama kwa mapinduzi ya kiuchumi--'utamu wa madaraka' kama si 'ukupe wa kimfumo' kwa jina la 'uongozi na utumishi wa umma' -- kwa wao kuwa vishadadizi wa >
tekinolojia bomoa-mambo< -- >
Kisebusebu na roho kipapo<.
Hili litaendelea kuwa hivi mpaka wakati ambapo ELIMU 2.0 itakavyokuwa imekomaa katika jamii, na wanajamii 'kujitambua', sisi wabantu tuna msemo:
kikulacho kinguoni mwako...
Hapa tunaweza kujionea: unafiki wa mataifa ya kibeberu... Wanaweza kujigamba na kutamba jinsi wao walivyo ni 'Demokrasia' kubwa lakini kumbe ndani ya mipaka yao, wananchi wake hawana uhuru kamili wa kujiachia na matunda ya ubunifu na uvumbuzi. Wakati huku kwenye 'ulimwengu unaoendelea' tunasakamwa na wao juu ya 'Utawala Bora' na mifumo ya kidemokrasia, sisi tunajisahau kuhoji na kujihoji Je, ni kwa nini kila kitu sisi tunaiga tu na kuzuga ili tufanane na wao? Mifumo yetu ya Elimu, ELIMU 1.0 inasombwa na kasumba za >
u-Eliti< na 'mashindano' na hali. mbona haya yote kiukweli hayainui 'ufahamu wa kweli katika watu' juu ya kuishi, liberiti na udhamirifu wa furaha?
Aina yeyote ya mfumo inayodumisha matabaka, hata huu muktadha wa nchi zilizoendelea, zinazoendelea na maskini inadhalilisha >
'heshima ya utu'< wa mwanadamu. >
'Mzizi wa fitina'< ni mifumo ya fedha, uchumi na mpangiko jamii.
Huko 'mbele' vinara wa madaraka na mamlaka wanajidai kutetea 'uhuru wa kuzungumza' na 'kujidhihirisha', kwa watu wake, na kumbe kwenye masuala ya tekinolojia wanaminya huo uhuru. Huku tunasemwa 'tunabanana kwenye mambo ya uhuru wa kisiasa' lakini kumbe tunachepushwa na mambo ya msingi: kamwe hatutapewa 'msaada' wa tekinolojia za kimkakati bali 'pesa za mkopo'... Tekinolojia zote za 'turufu' tutanunua kwa gharama kubwa ama hata mikopo. Hata kama ndani ya mataifa hayo kuna tekinolojia ambazo zinaweza kutokomeza umaskini ama maradhi, kamwe hatuwezi 'kupewa bure' japo wanajinasibu misaada kwetu... Sasa je, kwa nini sisi hatushtuki kuwa tusipojizatiti kufikiria upya namna gani tujipange ili kujikwamua kimaendeleo tutabaki 'kujidogosha' kwa mataifa ya kibeberu?
Ni ELIMU 2.0 inaweza kutufungulia njia ya kujikwamua... ELIMU 1.0, kote kote katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea ni jukwa la >
mifumo Babiloni<--mifumo nyonya damu. Jamii za watu wamejikabidhi kwa >
'Mazimwi--IMF...'<; na hali sisi Wabantu tuna msemo:
Zimwi likujualo halikuli likakwisha...
Leo hii, hapa Afrika, hatuzungumzi sana kuhusu 'ubeberu na unyonyaji' kwa sababu, miongoni mwetu--baadhi yetu, tayari >
tumerithi 'madhambi' yale yale ya waliotukoloni na kudidimizia chini 'maendeleo ya kiutu' kwa ajili ya maslahi yao binafsi<. Hatuhoji ama tumekwama kimbinu katika kushughulikia adha za umaskini usiondoka kwa mifumo hii ya kileo ya uchumi, fedha na mpangiko jamii kwa kuwa tumehadaika na ELIMU 1.0... Hatuoni aibu 'Tajiri/Mwekezaji' kulipa ujira mdogo kwa wajakazi/wafanyakazi/vibarua--kadiri yeye awavyo kuonekana ni 'tajiri' tunasahau ni kwa mgongo wa wengi wanaoteseka(?). Wanaoteseka nao wanaona hayo ni 'majaaliwa', eti ni bora mkono uende kinywaji kuliko kukosa kabisa... Kasumba ya kimawazo yawa basi 'bora mtumikie kafiri upate mradi wako'... Je, Kwa nini tunajinasibu na kule kuendekeza 'unyonge' ama/na 'akili ya kimaskini' angali 'akili' tunazo?
Tunaweza kubadili sura, hadhi na mwenendo wa mambo kwa ule 'utashi' wenye kujinasibu na kuyabadili 'masadikifu' yetu na tabia zetu. Tofauti na hili, tunaendelea kuamini shida zetu husubiri 'mwamba' fulani ajitokeze ili atutetee, ama hawa 'wakubwa' -- eti kuwa kana: 'wakubwa watufikirie'... >
'Mwamba' huyo wa labda kukemea ama/na kuwanyoosha hawa wakubwa, wenye kushikilia 'vibali' vya tabu, raha ama mateso yetu<,--wengi huishi toka kuzaliwa hadi kufa huku wakimtumainia, na hali hayupo!
Labda 'mwamba' huyu, daima tuko naye--ni fumbo katika akili zetu, lenye nasibu ya 'maarifa sahihi' na 'utashi'--kujua ilivyo bora... Mwenye kujua ilivyo bora, huchagua ilivyo bora...
Kujiepusha na mifumo ya kinyonyaji, Waasisi wa Taifa letu la Tanzania, kwa busara, walijitahidi kuzingatia shauri la 'maendeleo', 'Usawa' na 'Demokrasia'--walijitahidi sana. Hata hivi imekuwa kwamba -- sisi wananchi pamoja na viongozi >
'kuteleza hapa na pale'< kulingana na muktadha wa 'machaguo ya kitaasisi' lakini siyo kwamba viongozi waungwana >
hawakukiri makosa yao ama ya wengine waliothubutu kujinasibu na mkondo tofauti<. Haya yote ni Katika kujaribu kuyafanikisha hayo 'matatu ya shauri' kwenye sura na mwenendo wa jamii yetu. Lakini pia, katika muktadha wa 'matukio, jitihada na harakati za kiutekelezaji', >
changamoto na dosari hazikukosekana/hazikosekani<. Wasomi wengi wa leo, katika uwanja wa ELIMU 1.0, wanaweza kudai uwezekano wa kutengemaa kwa >
'Ujamaa na kujitegemea'< katika jamii hii yetu ni 'utopia'. ; lakini kwa mara ya kwanza lisemwe hapa: UJAMAA NA KUJITEGEMEA NI UWEZEKANO KUPITIA ELIMU 2.0 : "Uono na Ufikirifu Mifumo"...
Kwa hivi, kama alivyopata kuimba Msanii Lady Issa miaka ya 1980,
>'Tabu na Raha Inakungojea... Inategemea Akili yako... Tafuta eh utapata... Kumbuka Maneno...'<.
Sasa >
tunayoyakutafakari< katika kipindi hichi cha mpito -- kwa kusudi la kufanya hima ili kujinasibu na 'utu mpya' na 'nchi mpya':
Mwalimu Kambarage Julius Nyerere, wakati mmoja aliona ili nchi iendelee inahitaji 'watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora'... Walau fikara la ubayananishaji wa namna hii linaasili ya Uyunani ya kale--kupatwa kusemwa na >
mwanafalsafa Aristotle<. Uzoefu wa Mwalimu, kupitia yaliyosibu nchi-taifa kufika mwaka 1978, kulimfikishia busara ya jambo ambalo hata Mwanafalsafa Aristotle hakubarikiwa kupata kuwazia katika kipindi cha nyakati zake. Mwalimu aliona, utashi wa kisiasa pekee siyo jibu kwa maendeleo, ili nchi ipate maendeleo hatuna budi kuwa na taasisi zetu wenyewe za kuharakisha maendeleo vijijini na pia mijini. Hili lilipelekea kuanzishwa kwa taasisi ya mafunzo kwa wataalam wetu wenyewe kwa ajili ya mipango na maendeleo ya vijijini. >
Chuo cha Mipango cha Dodoma< ndiyo zao la fikra ile ya kimkakati ya Mwalimu. Na Chuo hichi kinamilikiwa na Wizara ya Fedha na Mipango.
ELIMU 2.0: "Uono ni Ufikirifu mifumo" ni akili-mbinu inayoweza kutupatia mwangaza wakuchagua mustakabali wa maisha yetu kwa upeo mpana kadri tuwezavyo kwa wakati. Katika mapana haya, ndiyo huja huu muktadha wa kusema 'Kupanga ni Kuchagua'. Na hii ni kauli mbiu ya >
Chuo cha Mipango cha Dodoma<; ilivyo ni Taasisi ya kuharakisha Maendeleo ya Vijijini na Mjini kwa nchi yetu ya Tanzania.
Sasa, Chuo cha Mipango, cha Dodoma, ni moja ya 'jitihada za kiwakati' za taifa letu la Tanzania. Ikibidi kuuandaa umma na ELIMU 3.0: Ilimu ilivyo ni Metafizikia ya Elimu, baadhi ya vitu 'visivyo vya kawaida' havina budi kuanza 'kuzungumzwa kwa kawaida'. Kama vile >
tulivyopata kumulika kungine<: "hata jambo tunaloweza kudai ni 'lenye ukuu kuzidi kawaida' huwenda pia ni la kawaida... Kawaida ambayo bado sisi kuielewa. Elbert Hubbard, angalisema '
The supernatural is natural not yet understood'...."
Taasisi hii 'imetangulia kiwakati' -- imetangulia taasisi ingine, tutakayoiita 'Akademi Wakati ya Tanzania/Kwanzania'. Hii inakuwepo mahala fulani ambapo leo hii (Januari 2023) ni mkoa wa Tabora. Katika vilele vya uwezo, ujuzi, ufundi na umahiri wanataasisi wa Akademi hii--mambo mengi yanafanyika 'kuongoza matukio' katika 'nyakati' na hasa hasa ndani ya kipindi cha miaka 400-- nyuma na mbele kiwakati... Na moja ya >
novelti< inayochoreshewa picha ya kuja kudhahirika, ikiwa tunatafuta kujua hatma ya hapa tulipo na tunakokwenda, kuhususiana na 'shughuli' ya Akademi hii ni '
Liberiti Afrika' na
'Liberiti Yunivasali'. Hii Akademi itakuwa kwenye uwezo na umahiri kufika 2060-2075. Kwa hivyo Chuo cha Mipango (IRDP) leo hii kinatoa Elimu-->
ELIMU 1.0 kwa 'wataalam mafunzoni'< kwa ajili ya ujuzi na maarifa ya Mipango ya Kisupasha -- kwa lugha ya Kiingereza hutajwa ni >
'Spatial Planning'<. Ila 'Akademi Wakati' yenyewe hujengea watu uwezo kwa ujuzi wa kuratibu 'Mipangilio ya kimatukio', hili litafahamika kama 'Uokestranisho Wakati' -- si kama vile labda mwenye kuzungumza lugha ya Kiingereza angalisema >
'Temporal Planning/Manipulations'< bali >
'Temporal Orchestration'<... Ikibidi kudadavua kidogo hili ndiyo 'madudu' gani -- hayo ni matokeo ya sayansi ya nafsi/sonafi/roho ambayo kufika 2060 itakuwa 'imeiva na kukamilika' pasi shaka lolote... Hili litukumbushe hapa kwamba: tunachofikiri leo hii tunajua kuhusu 'nafsi', 'kuzaliwa', 'kuishi', 'mauti' na 'wakati' huenda bado tunadanganyika na >
'akili ya hisia zaidi' na hiyo si 'akili ya kujua'<... Chuo cha Mipango ni 'Muona Aonwaye' kwa Akademi Wakati...
Kwa hivyo, leo hii wataalam wa Mipango hupanga kisupasha kwa ajili msambaziko muafaka wa 'maendeleo ya kiuchumi' katika jamii. Chuo cha Mipango kwa mfano, visomo vyake kwa uchumi hujinasibu na dhana ya 'kupunguza umaskini' ndivyo wenye kuzungumza kwa lugha ya Kiingereza hulitaja hili kama >
'Development Economics'<. Kwa uono na ufikirifu mifumo, umuhimu wa mipango kwa maendeleo hufungamana na >
usimamizi wa rasimali fedha< na kuwa huu ni shina muhimu la kuratibu mgawanyo wa huduma za jamii, mjini na vijijini. Ni sehemu ya Elimu 2.0 iliyoleta maarifa ya kuona mipango ni >
'mzunguruko'<; lakini pia humo humo mipango ni >
kuona mbele na kuainisha mapito< kuelekea 'Maono', kama vile Wizara ya Fedha na Mipango ilivyofanyakazi na kuibuka na >
'FYDP I, II na III'<
Ni vema kubaini, kwa jinsi gani Dunia yetu ilivyo ni hadaa na hali Ulimwengu ni Shujaa, hatma ya mataifa, ustawi na maendeleo daima iko mikononi mwa >
'Wanamipango'<, tena siyo lazima kuwa hawa ni watu wenye kufahamika hadharani. Kwa 'danganya toto' ya ELIMU 1.0 wengi wangalidhani maendeleo ya umma yako mikononi mwa Wanasiasa, Vibopa wachache, vyombo vya fedha, vyombo vya habari, tasnia ya silaha na majeshi...
Tukianza na Vibopa na vyombo vya fedha, tasnia ya benki na mifumo ya biashara huria ina mengi yenye kufungamana na historia ya shughuli za ukopeshaji mitaji kwa riba, uwekezaji na mahodhi kwa njia kuu za uchumi za kitaifa na mataifa. Kiuono na Ufikirifu Mifumo, biashara zinapokuwa chini ya mtindo wa fedha, mikopo na riba na basi uwekezaji; 'mashindano', 'mbinu-akili' na 'kutangulia' vina nafasi muhimu katika >
'kuitafuta/kujenga himaya'<... Kwa hivyo ipo namna rahisi tu ya kubaini ni namna gani uchumi wa leo wa kiliberali pamoja na utandawazi si uwanja wa kugawana mema ya 'nchi' kupitia biashara huria za kimataifa, bali >
'uwanja wa fujo zenye kustaarabishwa'< kwa propaganda.
Je, tunawajibika vipi na kutoa hesabu kwa matendo yetu--ushiriki wetu na harakati zetu katika mifumo hii ya fedha na uchumi ya kileo?
Je, tukioneshana njia tofauti na mifumo tofauti tutakuwa tayari 'kujipanga upya' ama ndiyo tutasalitiana kwa kuwa wengi wetu bado tunasadiki kuwa tuko katika mikono sahihi ya ushirilkiano wa jumuiya za kimataifa na jitahada za 'maendeleo endelevu' ya Dunia?
Je, vipi ikiwa hata hayo yenye kuonekana ni mazuri kwa kuyasikia habari zake, >
maazimio ya programu za maendeleo endelevu duniani<, kuna namna yakitazamwa kwa ELIMU 2.0 ni >
'Usanii'< wenye kunufaisha makundi fulani ya kimataifa--kihijimoni siasa, uchumi, fursa na maendeleo?
Vipi ikiwa hayo yote ya majukwaa ya kimataifa ni jitihada za 'akilikubwa' za watu kutoka 'dunia iliyoendelea' kujenga ushawishi wa namna fulani juu ya >
'utamaduni globali'<; hapo hapo watalaam mbalimbali kutoka kote Duniani wakichorewa mwelekeo wa mashauri ya kupendeza juu ya maendeleo ya watu; lakini kumbe >
'wanazugwa'<(?)... Kuna mengi humo kwenye mabaraza ya kimataifa hayataruhusiwa kujadiliwa na wala kutengenezewa mikondo ya mashauri ikiwa yanajinasibu na mifumo tofauti na ya kileo ya fedha. Watu wa mabaraza hutakiwa kuzungumza katika lugha >
'inayoeleweka'< ambavyo hufangamana na taasisi za leo za ELIMU 1.0; na tena kumbe hata Elimu kwa Umma kuna namna >
'inathibitiwa'< na 'Wajanja' kokote duniani. Na basi, kutoka kwenye hayo majukwaa na mikutano, mapelekeo ya kimapendekezo ya sera za maendeleo ya watu na jamii zao yana 'ukomo wa uvisomofikra'...
Kwenye fremu-kazi ya uono na ufikirifu mifumo, mambo ya sera ndiyo yanajitukiza kwenye vekta ya '
Mwongozo'; Mabaraza na majukwaa ni sehemu ya vekta '
Muundo' wa
vyombo vya ufanyaji maamuzi kupitia ujengaji wa vekta '
Ushawishi'. Maamuzi ya watu daima ni muafaka wa vekta '
Kujisikia' na vekta '
Vina vya Tafsiri' kimawazo/fikra;
ikiwa watu wanajua ilivyobora, watakata shauri ilivyo bora. Hili ni nasibu ya 'UONO' ama mitazamo ya Jamii.
Aidha, wanaoshiriki ama kushirikishwa kwenye vekta
Mifumo yake, KIWAKATI, hutumia uhuru wao wa kimawazo kuafiki vekta '
Nia' na vekta '
Vitendo' kupitia maazimo juu ya mahusiano ya shughuli za Kitaasisi. Basi vekta '
Dhamira' ikihusika katika kutekeleza hayo 'maazimio', kwa mfano, hujinyooshea katika 'sera mahsusi' juu ya 'ushughulikaji na makundi ya huduma kwa jamii' ilivyo ni miongozo ya kiutendaji na tawala--kokote kunakokusudiwa katika jamii. Hii ni nasibu ya 'ONTOLOJIA YA TAASISI'.
Hatua zinazochuliwa kubadili sura, hadhi, muktadha na mapana ya maendeleo ndiyo husenwa ni '
suluhu kwa adha za kijamii',--hizi zinaweza kuwa kisiasa, uchumi, utamaduni ama mazingira; na mchakato wenyewe, kiuono mifumo, huitwa 'intavensha'; wenye kuzungumza lugha ya Kiingereza wangalitaja hili kama 'intervention'--uingiliaji kati wa masuala ya jamii. Hili ni nasibu ya 'SURA NA MIENENDO YA JAMII'.
Kwa hivyo fremu kazi ya "Uono na Ufikirifu Mifumo", ilivyo ni kwa ELIMU 2.0, ni nyenzo ya kunyambulia jambo tunalokwenda kulifahamu kama 'Jiometria ya Utendekavyo Maamuzi Jamii'. Wanaozungumzia hili kwa lugha ya Kiingereza, wangalihusisha hili na kusema >
'Geometry of Actionable Decision Making'<. Maisha yetu yote ni >
'mchezo wa maamuzi'<; lakini vitovu vya maamuzi vina 'vina' vyenye kuweza kutofautiana kiakili na fahamu. Na basi hili ndilo huleta 'vina vya tafsiri'--kufanya tabia zetu kiakili katika kule kujiuliza uliza maswali na kujijibu akilini (Urazini) kuweza kutabirika kwa >
jeometria ya utendekavyo maamuzi ndani ya mtu mmoja mmoja ama kikundi<. Elimu 1.0 haiwezi kukanyaga kwenye visomo vya JUM ila 'visomo haba' ya udadisi wa sura, tabia na mienendo... Kwa kusema hivi, JUM inatubayanishia muktadha wa kutafsiri na kubashiri, Je, ni kwa jinsi gani
jamii isiyojua ilivyobora, haiwezi kutenda ilivyo bora...?
Mtu kutofanya 'maamuzi' na huu nao ni 'uamuzi'... >
Uamuzi wa daraja na hadhi ya chini kabisa< -- wakuamua kutokufanya uamuzi. Katika kikundi, mtu anayechelea kufanya ama kutofanya maamuzi, maamuzi yake 'yatafanywa' na wengine kwa 'niaba yake'--kwa yeye kupenda ama kutokupenda hali hiyo. Basi ndivyo 'watu wa madaraka' , kwa mfano, hufanya maamuzi kwa niaba ya wengi, iwe wao wanapenda ama hawapendi--na hakuna lolote la wao 'wanaofanyiwa maamuzi' wanaweza kufanya ila 'kuruhusu' kulingana na miundo ya kitaasisi. Namna hii, 'lawama' katika jamii ni upofu wa kutobaini mahusiano ya kiuwajibikaji na maamuzi katika jamii yoyote--kama kikundi cha watu wenye urazini na tena nasibu ya kujitambua na utashi.
....
++++