Akili ni nini?

Hii kitu ishajadiliwa sana hapa jukwaani. Ila next time uwe una summarize maana huu uzi ni mrefu mno. Nakuhakikishi hakuna mtu aliyemaliza kusoma ulichobandika hapo. Even Mshana Jr hajamaliza kusoma.



Sent using Jamii Forums mobile app
Ndefu mno. Watanzania na uvivu wetu wa kusoma sijui wangapi watasoma. Aliyesoma naomba summary.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wakuu, hapo ndio nime-summarize wandugu na bado kuna mitazamo mingi ambayo sijaiweka nimeona itakuwa ndefu sana.

Kuna maandiko yanayotoka kwenye BIBLE ambayo yanatakiwa kuwepo ndani yake, kuna mitazamo ya Ki-Buddha, Rastafarians wana mitazamo yao juu ya AKILI bado Hindu pia na hata Chinese na Atheists wana mitazamo yao wakuu. Kwa hiyo, ukijumuisha yote kwa pamoja kuna kitu utakipata zaidi.

Sasa ningesema niweke yote hapa pasingetosha ingechukua sehemu kubwa sana wakuu, nimetanguliza hiyo ili iwe rahisi nitakapoweka mitazamo mingine watu watafunguka na kuelewa zaid na zaid wakuu.

Thanks.
 
Hii ni moja kati ya mada fikirishi sana, kama ni mvivu wa kusoma lazma utoke NDUKI kwa kweli, safi sana.

JF kila siku ina vitu vipya aisee.
 


Bro,nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitakupa pongezi za dhati juu ya hiki ulichokiandika.

Bro umeandika elimu na kuihudumia elimu hasa. Laiti kama tukilisoma andiko hili na kutafakari,bila shaka ukakasi juu ya AKILI utatoweka mfano wa vumbi lipoteavyo angani.
 
Bro,nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitakupa pongezi za dhati juu ya hiki ulichokiandika.

Mkuu, niweze tu kusema HESHIMA kwako kiongozi kwa kuchukua muda wako wa kutosha juu ya hili.

Bro umeandika elimu na kuihudumia elimu hasa. Laiti kama tukilisoma andiko hili na kutafakari,bila shaka ukakasi juu ya AKILI utatoweka mfano wa vumbi lipoteavyo angani.

Usemacho ni HAKIKA kabisa kiongozi kusoma ni moja kati kati ya vitu vinavyoongeza UELEWA NA UPEO wa mtu then kufanyia kazi kilichosomwa ni hatua ya PILI ila wengi hiyo hatua ya kwanza tu kuipitia kwao inakuwa ngumu (KUSOMA) kwa hiyo hata hatua ya PILI (KUFANYIA KAZI) inakuwa ni ngumu zaidi mkuu.

Thanks a lot na hongera pia kwa hatua hiyo mkuu.

🙏🏼
 
gud thread,,,bt next time try to balance your source.. yo have based in quran
 
Mkuu, mwisho wa mjadala muafaka uliafikiwaje kiongozi... ?

Thanks.

Post ilitambaa mpaka replies 3000+ nikiuliza kama AKILI mtu ana akili ama hana... Nami nikatakiwa kwanza nitoe tafsiri ya akili
Mwishowe nilipotoa wakasambaratika wote...
 
Hii ni moja kati ya mada fikirishi sana, kama ni mvivu wa kusoma lazma utoke NDUKI kwa kweli, safi sana.

JF kila siku ina vitu vipya aisee.

Ni kweli mkuu.

JF is never boring kiongozi.

Karibu sana.
 
gud thread,,,bt next time try to balance your source.. yo have based in quran

Thanks a lot bro.

Ila ntaileta katika mitazamo mingine tofauti kiongozi nimeleta hii kwanza kutokana na ASILI ya neno lenyewe AKILI lilipotokea ili ikija kwa mtazamo mwengine watu waweze kuelewa zaid na zaid kiongozi.

Tuko pamoja mkuu. Thanks.
 
Post ilitambaa mpaka replies 3000+ nikiuliza kama AKILI mtu ana akili ama hana... Nami nikatakiwa kwanza nitoe tafsiri ya akili
Mwishowe nilipotoa wakasambaratika wote...

Hahahahah.

Mi huwa nakukubali sana katika kujenga HOJA MKUU kwa sababu una NGUVU ZA HOJA na HOJA ZA NGUVU zote kwa pamoja mkuu.

Hujawahi kuniangusha pale unenapo kupitia kinywa chako kiongozi.

Nakuelewa sana bro.

Thanks.
 
Je Akili huwa inaugua? Maana tunasikiaga mgonjwa wa akili. Ambao kwa ufahamu wangu ni.
1. Kichaa
2. Mwendawazimu
3. Chizi
4. Punguani na
5. Taahira.
Sasa kuna jamaa mmoja yeye ni kichaa. Ila anaakili sana. Ila ni kwenye sehemu za michezo. Huyu yupo pale lumo kule yombo. Akiwa anapita mnamwona kichaa kabisa. Ila akija kwenye draft kijasho kitakutoka. Humfungi. Na anaelekeza vizuri penye makosa. Ila akitoka hapo ni kichaa kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahah.

Mi huwa nakukubali sana katika kujenga HOJA MKUU kwa sababu una NGUVU ZA HOJA na HOJA ZA NGUVU zote kwa pamoja mkuu.

Hujawahi kuniangusha pale unenapo kupitia kinywa chako kiongozi.

Nakuelewa sana bro.

Thanks.


Jr
 
Akili ni kama ratio (mizania) ya kitu chochote kile... Lazima kuwe na vipimo vyake.... Visipungue sana wala visizidi sana.... Ili kuepusha kasoro

Jr
 
Je Akili huwa inaugua? Maana tunasikiaga mgonjwa wa akili.

Mkuu, akili haiugui kwa sababu sio kitu ambacho unaweza ukakiona au ukakishika kama ulivyo moyo au ubongo. Chukulia mathalan mtu anapoumwa Malaria si unaweza ukasema "HUYU NI MGONJWA WA MALARIA". Sasa swali lako ndivyo ulivyoliweka hivi kwamba Malaria inaugua kwa sababu anaitwa mgonjwa wa Malaria.

Hivyo hivyo kwa mgonjwa wa akili, yale ni matokeo ya utendaji kazi wake kupitia ubongo na moyo ukijumuisha matendo yake huyo mtu kwa jumla ndipo AKILI inapopatikana hapo.

Ambao kwa ufahamu wangu ni.
1. Kichaa
2. Mwendawazimu
3. Chizi
4. Punguani na
5. Taahira.

Hawa wote wana mapungufu ya akili na wote wapo kwenye kundi moja japokuwa huzidiana tu kati ya mtu na mtu kutokana na upungufu wa mtu alionao mkuu.

Sasa kuna jamaa mmoja yeye ni kichaa. Ila ana akili sana
.

Kwanza kabisa nikuulize tu mkuu, huyu mtu unayesema ana akili sana umemuweka kwenye kundi la watu wenye AKILI SANA katika mtazamo gani kiongozi... ?. Au labda kwa mtazamo unaoujua nikikuuliza kuwa AKILI NI NINI mpaka ukasema kuwa ana AKILI SANA...?

Ila ni kwenye sehemu za michezo. Huyu yupo pale lumo kule yombo. Akiwa anapita mnamwona kichaa kabisa. Ila akija kwenye draft kijasho kitakutoka. Humfungi. Na anaelekeza vizuri penye makosa. Ila akitoka hapo ni kichaa kabisa.

Huwezi kukuta mtu ambaye hana AKILI kabisa niambie lazma atakuwa na sehemu ndogo tu ya AKILI ambayo aidha itakuwa ni UTAMBUZI au KUMBUKUMBU au hata MAARIFA pia. Sasa hivi sio vigezo vya kusema eti fulani ana AKILI SANA hiyo itakuwa ni sehemu ndogo sana ya AKILI.

Na ndio maana utakuta mtu anaitwa CHIZI MAARIFA yote hiyo ni kwa sababu nna MAARIFA au UTAMBUZI au KUMBUKUMBU tu kiasi ya kufanya jambo fulani mkuu.

Na ndio mana hata CHIZI akihisi NJAA anatafuta chakula anakula, hiyo ndio sehemu ndogo ya AKILI ambayo inaweza kuwa ni KUMBUKUMBU au UTAMBUZI kwamba anatambua kuwa hapa linatakiwa lifanyike jambo fulani. Angalia wale wanyama kwenye circus wanafanya vitu kadha wa kadha nao utasema wana AKILI SANA mkuu...?

Ukitaka kujua kuwa wana AKILI au HAPANA wapime kwenye suala zima la BUSARA au hata HEKIMA pia.

Thanks a lot.

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]
 
Akili ni kama ratio (mizania) ya kitu chochote kile... Lazima kuwe na vipimo vyake.... Visipungue sana wala visizidi sana.... Ili kuepusha kasoro

Jr

Ni kweli kuwa AKILI huwa zinazidiana kiongozi wengine zipo kwa kiwango cha juu, wengine kiwango cha kati, wengine katika kiwango cha chini na wengine katika kiwango cha chini kabisa.
 
Na je ni kweli kwamba akili ikikuzidi sana inaweza ikaleta madhara?sababu ya kuuliza hivyo ni kwamba kuna brother mmoja hivi kipindi niko secondary alikuwa kichwa sana kupilitiza na alikuwa mpole mno ila siku nyengine dish likiyumba unaweza ukamkuta ghafla anaiongelesha half cake alioishika canteen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…