Akiba yetu ya mafuta imekwisha tayari?

Aug 10, 2011
81
9
Kutokana na mvutano uliokuwepo kati ya wafanyabiashara na EWURA juu ya bei ya mafuta kumalizika kwa bei ya mafuta kushushwa tulitarajia kama tulivyoelzwa kuwa tuna akiba ya mafuta ambayo inaweza kutosha kwa mwezi wote huu wa nane...hata wiki haijaisha mafuta yamepandishwa kisa eti thamani yetu dhidi ya dola imeshuka! sina tatizo na hilo la kushuka kwa shilingi yetu kwani uchumi wetu hauko imara ila kinachonishangaza ni kupanda kwa mafuta wakati hatujaagiza hata shehena ya mpya ya mafuta kwa bei mpya iliyopanda! je ilikuwa kiini macho cha EWURA kushusha bei au ndo maana ya nguvu ya wafanyabiashara wa mafuta?
 
Wamiliki wa vituo vya mafuta ni wabunge na mawaziri,so kesi ya nyani inapelekwa kwa tumbili.
 
Siku 48 ni sawa na masaa 48 kwa wafanyabiashara wa mafuta, kwahiyo stock waliyonayo itakuwa imeisha
 
Back
Top Bottom