Akhsante sana Mwalimu wangu wa Saikolojia kwa Elimu kubwa ya Saikolojia ambayo sasa naanza kuiona Tanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,543
108,877
Nakumbuka alisema Darasani kwamba siku zote mkiwa katika Watu wengi halafu ukataka Kumjua ' Mhalifu ' kwa haraka sana basi ukiona tu Mtu mmoja kati yenu ndiyo anapenda sana ' Kujitokeza ' huku na kule na mara nyingi anapenda ' Kuongea ' na ' macho ' yake hayatulii halafu hana ' wasiwasi ' wowote jua ndiyo mwenyewe.

Jana binafsi mida ya kama Saa 11 za Alfajiri nikiwa nasubiri Usafiri wa Mwendokasi eneo la Kimara huku tukiwa Watu wengi niliibiwa Simu ' Kitaalam ' kabisa kisha nikamwona Mtu mmoja akianza Kuongea sana na kujifanya Mtu mwema hivi Kwangu katika Kunisaidia ila ghafla nikamwona ametoka pale Kimara amepanda Bodaboda ameelekea pande za Oysterbay ambapo hata Mimi pia kwakuwa Simu yangu ilikuwa ni ya Bei kali ilinibidi nikodidshe ' Uba ' ambapo nilimfuatilia ila nikaambiwa ameonekana akikatisha mitaa ya kwenda Masaki na kutokomoea.

Bora hata angeniibia tu Pochi yangu lakini siyo ile Simu yangu kwani Simu yenyewe nayo nilipewa na Marafiki zangu wawili wa Kizungu baada siku moja kunikuta nikifanya sana Mazoezi yangu ya ' Ukakamavu ' pale Coco Beach huku nikiwa na Simu yangu ya ' Tochi ' ndipo waliponiita, kujenga Urafiki nami, tukajuana na wakanizawadia hiyo Simu ambayo ni ya Kisasa kabisa halafu imeweza hata kunifanya siku hizi mechi zote za Simba SC nisiwe naenda Kuziangalia Uwanjani bali naziangalia tu kupitia hiyo hiyo Simu.

Huyo Mwizi wangu hata sasa hivi Sura yake naikumbuka na hata Sauti yake nayo naikumbuka vizuri sana tu. Akhsante sana Mwalimu wangu wa Saikolojia kwani tayari Mwizi wangu aliyeniibia / aliyenikwapulia Simu yangu jana Saa 11 Alfajiri pale Kimara nimeshamjua hivyo nami sasa najiandaa kwenda Kwetu Kumalizana nae kwa Mitishamba na baadae Albadiri.

Nawasilisha.
 
Una Maana gani?
 
naona bashite anashambuliwa tu leo
 
Huu si muda wa kutuhumiana umeambiwa toka Jana kuwa hata kama una taarifa ndogo kiasi gani ambayo inaweza kusaidia upatikanaji wa Lê Billionaire ziwasilishe kwenye mamalaka husika na si kupost hapa kijiweni
 
Pamoja na digirii yako lakn kichwani unaonekana mweupe kabisa, yaani empty set, wanasaikolojia wanakuita tabularasa,aya karibu kwa mipasho yako dada isha mashauzi a. k. a genta.
 
Huu si muda wa kutuhumiana umeambiwa toka Jana kuwa hata kama una taarifa ndogo kiasi gani ambayo inaweza kusaidia upatikanaji wa Lê Billionaire ziwasilishe kwenye mamalaka husika na si kupost hapa kijiweni
Aise, hivi kumbe [U]GENTAMYCINE[/U] ni bilinear!? Sasa kwanini apande mwendo kasi na baada ya kuibiwa simu yake akakodi UBA? Mambo ya simu yake na mamlaka husika ni wapi na wapi!? Anyway, anasema pia alienda polisi Ostabei, sasa afanye nini zaidi ya hapo!? Au mi ndio sijaelewa hapa!?
 
Nakumbuka alisema Darasani kwamba siku zote mkiwa katika Watu wengi halafu ukataka Kumjua ' Mhalifu ' kwa haraka sana basi ukiona tu Mtu mmoja kati yenu ndiyo anapenda sana ' Kujitokeza ' huku na kule na mara nyingi anapenda ' Kuongea ' na ' macho ' yake hayatulii halafu hana ' wasiwasi ' wowote jua ndiyo mwenyewe.

Jana binafsi mida ya kama Saa 11 za Alfajiri nikiwa nasubiri Usafiri wa Mwendokasi eneo la Kimara huku tukiwa Watu wengi niliibiwa Simu ' Kitaalam ' kabisa kisha nikamwona Mtu mmoja akianza Kuongea sana na kujifanya Mtu mwema hivi Kwangu katika Kunisaidia ila ghafla nikamwona ametoka pale Kimara amepanda Bodaboda ameelekea pande za Oysterbay ambapo hata Mimi pia kwakuwa Simu yangu ilikuwa ni ya Bei kali ilinibidi nikodidshe ' Uba ' ambapo nilimfuatilia ila nikaambiwa ameonekana akikatisha mitaa ya kwenda Masaki na kutokomoea.

Bora hata angeniibia tu Pochi yangu lakini siyo ile Simu yangu kwani Simu yenyewe nayo nilipewa na Marafiki zangu wawili wa Kizungu baada siku moja kunikuta nikifanya sana Mazoezi yangu ya ' Ukakamavu ' pale Coco Beach huku nikiwa na Simu yangu ya ' Tochi ' ndipo waliponiita, kujenga Urafiki nami, tukajuana na wakanizawadia hiyo Simu ambayo ni ya Kisasa kabisa halafu imeweza hata kunifanya siku hizi mechi zote za Simba SC nisiwe naenda Kuziangalia Uwanjani bali naziangalia tu kupitia hiyo hiyo Simu.

Huyo Mwizi wangu hata sasa hivi Sura yake naikumbuka na hata Sauti yake nayo naikumbuka vizuri sana tu. Akhsante sana Mwalimu wangu wa Saikolojia kwani tayari Mwizi wangu aliyeniibia / aliyenikwapulia Simu yangu jana Saa 11 Alfajiri pale Kimara nimeshamjua hivyo nami sasa najiandaa kwenda Kwetu Kumalizana nae kwa Mitishamba na baadae Albadiri.

Nawasilisha.
Unajua kutunga sana mkuu...kwanini usijiunge na bongo movie.
 
Back
Top Bottom