Hii ni kwa wasaidizi wa Mhe. Rais Magufuli: Naomba Mheshimiwa Rais asaidiwe kuhakiki akaunti zake zote zilizoko katika mitandao ya kijamii hasa Facebook maana kumekuwa na akaunti zaidi ya tatu zinazojibainisha ni zake. Mnaweza kuwasiliana moja kwa moja na wamiliki wa Facebook. Hii itatusaidia sisi wananchi kuwa na imani kuhusu ujumbe tuuandikao kupitia akaunti hizo. Pia itasaidia kuzuia matapeli wenye nia mbaya ya kutumia jina la Rais kwa matakwa yao binafsi.