Akaro acha wivu, January habebwi na Makamba

Akaro acha wivu, January habebwi na Makamba

mkude kibwana

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
348
Reaction score
27
Katika pitapita yangu FB nikakutana na post ya mtu mmoja anayejiita Carthbeth Akaro akimchafua January Makamba, ametumia lugha ya kiingereza na hayo kwenye mabano ni nukuu ya maneno yake na bila shaka wengi wana mtazamo kama wa Akaro. unajua wengine hatupendi hizi siasa za kuchafuana na za kupindisha ukweli, nimeona ni vema kama kijana mwenzangu nimkumbushe yafuatayo. Akaro nisikilize sasa.

Akaro huenda uko sahihi kwa kiwango Fulani lakini pia uelewe pia hauko sahihi, mawazo na maoni yako umeyatoa kwa kutumia hasira Zaidi kuliko busara na hekima, hili peke yake linatosha kukutoa katika usahihi na hivyo kuonesha bila shaka yoyote kuwa hujaongozwa na ukweli wa mawazo, bali umeongozwa na chuki binafsi dhidi ya mtu na familia yake. Hebu turejee wote ulichoandika na tupite baina ya mistari.

{January Makamba please don't play with people mind. We are smarter than you think.. You have been depute minister for two years with no clear responsibilities you had never do anything tangible in your life.}

Akaro kwanza naomba ukubali kuwa mafanikio ya wizara yoyote yanatokana na utendaji mzuri wa baraza la mawiziri na utendaji mzuri pia ndani ya wizara husika bila kuziacha idara zilizopo chini ya wizara hiyo. Kwa hiyo pongezi au lawama juu wizara haziwezi kubebwa na mtu mmoja kama unavyotaka kutuaminisha hapa, na ndio maana nilisema umeongozwa na hasira Zaidi kuliko busara.

Hata hivyo kwa kuongozwa na kweli naweza kusema yafuatayo.
Mosi:
January ameikuta sekta ya mawasiliano ikikua na yeye akiwa kama naibu waziri hiyo sekta imeendelea kukua kwa wastani wa asilimia 20, na ndio sekta pekee inayokua kwa kiwango hicho kwa kipindi kirefu. sasa hivi karibu kila mtu ana simu ya mkononi na anaweza kumudu kuitumia sio jambo lililotokea lenyewe tu kwa ajali. Sasa hivi huhitaji kuwa na mzigo wa laini za simu, uhitaji kutembea na laptop, uhitaji kufikiria juu ya vifurushi vya intaneti. Hata wewe Bw Akaro unapata uwezo wa kuandika yote haya na watu wengi kuona ulichoadnika kutokana ukuaji wa sekta hii, kinyume chake hizo hasira zako juu ya January angezisikia mkeo na watoto zako.

Pili.
Makamba akiwa naibu wiziri katika wizara hii tumeona kuimarika kwa huduma za utumaji wa fedha kwa kutumia simu za mkononi. Biashara imekuwa nyepesi kutokana huduma hizi na hasahasa mara baada ya kuwepo mahusiano kati ya mabenki na mitandao ya simu na mahusiano katika huduma za kifedha kati ya mabenki na simu. Haya yote si mambo ya kibahati mbaya kaka.

Tatu.
Kubwa ili kuhakikisha kuwa serikali haipotezi mapato katika sekta hii, 2013 umefungwa mtambo wa kufuatilia wa kisasa kufuatilia mapato ya makampuni haya na sasa mapato ya serikali kutoka sekta hii yameongezeka.

{You have no track record no historical background to judge you in future.}
Hapa pia unakosea sana, Mwalimu Nyerere alipoaminiwa kuiongoza TANU na kuongoza harakati za ukombozi hakuwa na historia ya kumbeba na usitake kuniambia kuwa uchifu wa baba yake Nyerere ndio uliopelekea Nyerere anaitwa baba wa taifa letu na kubwa Zaidi kuna mchakato wa kuitwa mtakatifu kwa upande wa kanisa alilokuwa anasali.

Uwezo wa Nyerere wa kupambanua na kuchambua mambo ndio uliomfikisha pale alipofikia, na alipoaminiwa kuyasimamia yale aliyopambanua na kuyachambua aliweza kuyasimamia kama kiongozi wa TANU na baadae kama rais wa nchi. Uwezo huo wa kupambanua na kuchambua January anao na kama ulisoma vizuri kitabu cha Padre utaamini kuwa ni kweli huyu Bwana January huo uwezo anao, hivyo ni jukumu letu kuumpa nafasi ya kuyafanyia kazi yale aliyoyachambua; na ukizingatia hakuna mwenye uzoefu wa urais katika nchi yetu isipokuwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete.

{My understanding that if you were born from normal family not having someone in your family be a politician (dad) you won't be were you're.}
Hapa napenda kusema yafuatayo.

MOSI.

Akaro usimuhukumu January kwa kitendo cha mzee Mkamba kutimiza majukumu yake kama mzazi na kama kiongozi mkuu wa familia, kama baba yako alikutelekeza katika kutimiza ndoto zako na matarijio yako hiyo ni wewe na ni tatizo lako, na katu hutakiwi kutaka wengine wapitie kadhia uliyopitia wewe baada ya mzazi wako kukacha majukumu yake(kama ni kweli.)

PILI.
Jaribu kusoma au kufutialia historia ya January vizuri, utagundua baada ya kumaliza kidato chake sita pale Morogoro alisimama yeye kama yeye, na amendelea kusimama hivyo hadi sasa. Juhudi zake ndio zimemfikisha alipo. Pia mafanikio ya mtu hutokana na ushirikiano anapoewa toka kwa ndugu, marafiki na jamaa.

Kama kuna watu wanampa ushirikiano au msaada January sababu ya jina la baba yake, hilo katu haliwezi kuwa kosa la January, na huwezi kumuhukumu January kwa kosa hilo, lingekuwa ni kosa la January endapo angetafuta unafuu wa namna yoyote kwa kutumia jina hilo.

Akaro naomba ujue, kama vile ambavyo watu wanaweza kuumpa ushirikiano na msaada January sababu ya jina la baba lake, pia watu wanaweza kumuangusha, kuchukia na kumfanyia kila aina hujuma sababu ya jina baba lake. Mfano mzuri nini wewe, chuki zote hizi kwa January ni kwasababu unamchukia mzee Mkamba na siasa zake, laity ungekuwa huna jambo na mzee Mkamba, kwa vyovyote vile huyu January ungempa sifa yake inayomstahili na si nyingine bali ni kijana mchapakazi, mweledi, mwenye maono, uthubutu na uwezo wa kuvusha toka kwenye mkwamo huu tulio nao kama taifa.

{I just listen you this morning. actual I listen it because my car radio otherwise I won't listen what you were talking. You should not be a president to implement your ideas your member of NEC, your depute minister with no responsibilities and you have all machinery to press what your ideas. Advice your party CCM to implement your ideal you should not wait to be a president to implement your ideals.}

Unamaanisha mawazo na fikra zake juu ya TANZANIA anayoiota au itaka angeyawasilisha katika vikao vya chama na katika serikali sababu kwa nafasi yake ndani ya CCM na serikali uwezo huo anao. Hapa naomba kusema yafuatayo.

Mosi.
Mimi na wewe si wajumbe wa NEC na si sehemu ya baraza la mawaziri, hivyo hatuwezi kujua yepi ameyasimamia January katika NEC na amemshauri nini waziri au rais juu mambo kadhakadha juu ya nchi yetu. Kwahiyo badala ya kusema Janury hajafanya hayo, lingeubuka swali kwa January katika vikao vya maamuzi ndani ya CCM hususani ndani ya NEC ndani ya serikali ameshauri nini hususani juu ya mambo ambayo yako nje ya wizara yake.

Kwa vyovyote vile yapo aliyoyafanya, na kwa kufanya yote hayo katu hamuondolei wajibu na ulazima wa kuweka maono yake wazi katika namna ya pekee na ya kujitofautisha na wengine walioweka maono yao wazi juu TANZANIA yetu ya sasa na mustakabali wake wa baadae. Angeonekana mtia nia wa vituko kama angefanya hivyo bila kuweka wazi maono na matarajio yake sanjari na matarajio ya watanzania walio wengi.

Katika kuhitimisha hapa, yapo mengi ameyafanya katika serikali na chama chake kwa lengo la kuboresha maisha ya watanzania na vijana wa Tanzania, lakini pia ni kulikuwa na haja ya kumsikia kama mtangaza nia tutegemee nini toka kwake pindi tukimtimizia nia yake na nini hatima ya matarajio yetu kama taifa, haja hii ameitimiza ipasavyo kupitia majibu ya maswali 40 toka kwa Padre.

{I hear you said no job for youth and that is number one in manifest please we need to go in details how are you going to that. Jakaya kikwete used the same trick with no clear plan no clear manifest and you want to use the same path Jakaya used to fool people to climb to higher office}

Hapa sipendi kuongea sana, lakini naomba soma kitabu cha Padre Karugendo swali namabari saba na majibu yke tafadhali. Hilo ni swali juu ya ajira aliloulizwa January na Padre, amejibu vizuri na amefafanua kwa uzuri kabisa.

Pamoja na mambo mengine January anaona kuna haja kuwa na sharia itakayokuja na mpango mahususi na wenye hatua kubwa wa kukabiliana na tatizo la ajira. Mpango(muswada) huo umegusa eneo kubwa la ajira( kujiajiri na kuajiriwa); wenye malengo wa kuwapatia vijana elimu yenye kuwawezesha kuhimili ushindindani katika soko la ajira, uzalishaji wa ajira nyingi zaidi na mazingira mazuri ya uanzishwaji viwanda na kutoa unafuu kwa viwanda vitakavyo jishughulisha na upandishaji wa thamani ya mazao ya kilimo.

Yako mengi, hivyo acha uvivu, soma kaka na acha wivu usiokuwa na faida.
 
Kwanini hukumalizana naye FB unatuletea huku mipasho na Taarbu zako?

Kama una macho na Masikio basi tambua kuwa "Akoro yupo sahihi na Watanzania wote ndivyo tunavyo elewa, kwa alicho kisema"

Mrudishie January hela yake aliokupa umpaishe, kwani Watanzania tuna macho na masikio! Nenda kamwambie anaye kulipa, asipoteze muda na hela zake nyingi kujitembeza.....kazi na kuwatumikia wananchi ndio kutakapo muuza!

Amefanya nini tunachokijua zaidi ya kunyoa nywele zake, ili tuseme anafaa hata kuchukua form ya urais! Wakati katiba inaandikwa na wahuni wenzie, hatujasikia kauli yake yyte ya kutetea wananchi....!

Afadhali hata Mwigulu anaonyesha kukerwa na issue ESCROW acc! January ametoa kauli gani juu ya hili sakata? Tena pengine usikute jina lake limo katika waliopewa mgao wa Escrow kutipitia Stanbic!
 
Kwanini hukumalizana naye FB unatuletea huku mipasho na Taarbu zako?

Kama una macho na Masikio basi tambua kuwa "Akoro yupo sahihi na Watanzania wote ndivyo tunavyo elewa, kwa alicho kisema"

Mrudishie January hela yake aliokupa umpaishe, kwani Watanzania tuna macho na masikio! Nenda kamwambie anaye kulipa, asipoteze muda na hela zake nyingi kujitembeza.....kazi na kuwatumikia wananchi ndio kutakapo muuza!

Amefanya nini tunachokijua zaidi ya kunyoa nywele zake, ili tuseme anafaa hata kuchukua form ya urais! Wakati katiba inaandikwa na wahuni wenzie, hatujasikia kauli yake yyte ya kutetea wananchi....!

Afadhali hata Mwigulu anaonyesha kukerwa na issue ESCROW acc! January ametoa kauli gani juu ya hili sakata? Tena pengine usikute jina lake limo katika waliopewa mgao wa Escrow kutipitia Stanbic!

kuwa muelewa,, au jifunze kuelewa,
 
niache nisije nikakulilia humu Ww mkude kibwana.... najutaaa kwenda kumpangia foleni kumpigia kura huyu kipara ngoto! amemchafua haya kamuogeshe...
 
Back
Top Bottom