Akamatwa na vipande 8 vya meno ya tembo Katavi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
meno-ya-tembo-2.jpg

Mtuhumiwa Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbende Wilaya ya Mlele akiwa katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa na meno ya tembo vipande nane yenye thamani ya shilingi milioni 120 hapo juzi.

meno-ya-tembo-3.jpg

Kamanda wa Polisi wa Mkoa Katavi Dhahiri Kidavashari akiwa ameshika meno ya Tembo aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Nzuri Ndizu mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ambae alikamatwa juzi akiwa na vipande 8 yenye thamani ya milioni 120 .

meno-ya-tembo.jpg

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi amekamatwa akiwa na meno ya Tembo nane yenye uzito wa kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni 120 ambapo ni sawa na Tembo wanne waliuawa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mida ya saa tatu na nusu .

Kidavashari alisema mtuhumiwa Ndizu alikamatwa kufuatia misako na uparesheni mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi ikiwa ni kuhakikisha wahalifu wa makosa mbalimbali wakimemo wawindaji haramu wa wanyama pori wanakamatwa.

Siku hiyo ya tukio jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa Raia wema kuwa katika pori la akiba la Lwafe kuna watu wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo .

Kidavashari aliendelea kuwaambia waandishi wa Habari baada ya taarifa hizo kupokelewa ufuatiliaji ulifanyika kwa polisi kufika kwenye eneo hilo na kuweka mtego ambapo walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Nzuri Ndizu akiwa na meno ya Tembo vipande nane akiwa ameyaficha kwenye pori kwa ajili ya kusubiria wateja .

Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa hatua za upelelezi zaidi ilikuendelea kubaini mitandao yote inayojihusisha na biashara hiyo haramu ya meno ya Tembo na kufikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Chanzo: Katavi Yetu blog
 
Ningekuwa mimi rais, suala la kulinda maliasili lingepewa kipaumbele cha kwanza. Bila kulinda maliasili, dunia itajifia natural death, wala hata kiama hakitatakiwa
 
Mkoa wa Katavi na mbunga ya Wanyama ya Kativi bado ni eneo ambalo lina utajiri mkubwa wa Wanyama pori. Kuanzia Milima ya Lyambalyamfipa ,Katavi ,Stalike, Inyonga hadi Ugalla River ni mapito na makazi ya Wanyama pori.
Kumekuwepo na uwindaji haramu kuanzia family levels kwani huko nyuma takrabani kila nyumba ya Mbende ( waenyeji wa wilaya ya Mpanda) ilikuwa wanamiliki bunduki iliyoyengenezwa kiienyi (gobole). Inyonga pamoja na kilimo cha Karanga lakini pia ni kituo cha uwindaji haramu wa meno ya tembo. Njia yao huwa ni Burundi na pia kwa njia ya train kuja Dar.
Kwa sasa ni mhimu pia Katavi ikapewa umhimu mkubwa wa uhifadhi kama ilivyo kwa Serengeti, Ngorongo na hata Seleou. Faida kubwa kwa Mbunga ya Katavi na maeneo yanayoutengeneza ukanda huo ni kuwa Wanyama pori wake ni wakubwa kwa maumbo yao kuliko wa sehemu nyingine. Hivyo walindwe.
Kilichofanyika ni sahihi na cha kuigwa mfano sehemu zingine ambapo mambo kama hayo yanatendeka.
 
Back
Top Bottom