DOKEZO Ajira zilizotolewa na TAMISEMI (Afya) zimekuwa changamoto kwenye malipo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Habari za jioni.

Kuna ajira zilitolewa na Tamisemi mkataba mwaka huu 26 January.

Waajiriwa wapya waliripoti kwenye vituo vyao vya kupitia Halmashauri zao mbalimbali wakiwa na idadi 295.

Ajira Hizi zinasimamiwa na Mradi unaoitwa Tanzania maternal and child initiative project (TMCHP) unaofadhiliwa na World Bank chini ya wizara ya afya na Tamisemi.

Changamoto iliyokuja kuonekana hadi leo tar 17/3.

Hatujalipwa malipo ya mwezi wa pili na hela ya kujikimu ilhali tuko makazini na tunatambulika kama watumishi wa umma.

Mstakabali wa malipo haueleweki hadi leo tumebaki njia panda.
Poleni sana. Mbaya zaidi utakuta uliipigia kura ccm.
 
Subirini wahuni wagawane pesa za kikundi.mishahara yenu wame peleka rejesho
 
Back
Top Bottom