Abuwhythum
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 837
- 495
Serikali kupitia kwa Waziri wa Utumishi wa umma na utawala bora ilitangaza kuwa mwezi ujao inategemea kuajiri walimu wa sayansi na hisabati pamoja na Mafundi sanifu wa maabara ambao kwa ujumla wao ni 4348.
Izingatiwe kuwa hadi tangazo hilo linatoka waziri husika alisema walimu wa sayansi waliotuma maombi (izingatiwe muda ulishaisha) ni 2,100 mafundi sanifu wa maabara wanaendelea kutuma vyeti hadi tarehe 20/02 lakini serikali tayari inajua idadi ya watu itakaowaajiri.
Swali langu ni je huu uhakiki wa vyeti una lengo la uhakiki kweli? Au nikuendelea kuchelewesha muda wa kutoa ajira na stahiki nyingine za walioajiriwa tayari?
Mafundi sanifu ni wachache sana wakilinganishwa na Walimu wa sayansi na hisabati, cha kushangaza wamepewa takriban mwezi mzima kuwasilisha vyeti ika Walimu walipewa siku tano tu! Hapo bado majina ya ajira zao walimu na mafundi sanifu watataka wayatoe kwa pamoja! Kumbukumbu hapo bado hawajawaongezea muda! Kweli hata kama ni mtoto mdogo ukiwa muongo kwa visingizio ambavyo havina msingi atakugundua tu!
Katika suala hili la ajira wanaosubiri wote hakuna kuamini cha nani wala nani! Haoa cha kuamini ni pale tu majina watakapowekwa kwenye tovuti ya TAMISEMI, ukaripoti na ukaona mshahara wako wa kwanza umesoma kwenye akaunti haya mengine yoooote! HAKUNA CHA MSEMA KWELI wala vha nani!
Hata huo mwezi wa tatu uliosemwa tena mbele ya Bunge tukufu usiamini sana kwa sababu hata Jaffo alitamka mbele ya Bunge tukufu kuwa ajira za walimu (tena wote) ni Mei lakini ni miezi 10 sasa hakuna lolote tunaloliona.
Msemaji mwingine akasema ajira zinasitishwa kwa mwezi mmoja na nusu haitazidi miezi miwili, toka amesema hayo ni miezi 8 sasa hakuna lolote.
Hata anayekwambia March Usishangae inapita hivi hivi.
Sema tu hali hairuhusu ika wahusika wote tungefanya maamuzi magumu ya kutofika tutakakopangiwa kwa kisingizio tumeshapata kazi nyingine. Akili ingewasogea na huu ufisadi usingetokea tena. Japo wana kiburi kuwa kuna wahitimu wa wengine wa 2016 wapo mtaani.