Ajira za udereva na wanawake

Mto wa mbu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2021
Posts
4,515
Reaction score
11,383
Hi

Kuna kitu kinashangaza, hivi kwanini wanawake hawapewi nafasi sawa na wanaume kwenye kazi za udereva.

Je hawawezi, au Ni dhana ya kuwa mwanaume ndo ataweza kazi ya udereva.

Je kwa wewe mwanaume utakubali mke wako awe dereva?
 
Akiwa na mimba itakuaje na anatakiwa kazini, au atatapika njia nzima ilimradi safari yake afike?
 
Akiwa na mimba itakuaje na anatakiwa kazini, au atatapika njia nzima ilimradi safari yake afike?



Wala haihusiani kabisa ,

Mimba si ugonjwa.

Tena Mjamzito akijiweka bize hata hizo mambo za vichefuchefu hakutani navyo kabisa!

Kwani kwenye hizo ajira nyingine wajawazito wanamudu vipi kufanya hadi ufike wakati wa kujifungua?

Havihusiani
 
Sema ni mambo ya mfumo dume tu na wanawake wenyewe wanahitaji Ukombozi wa fikra.
 
Tena wakipatikana madereva wakike ingependeza sana,

Ajali za barabarani zingekoma kabisa au kupungua sana kukaribia na kuisha kabisa Yani ingebaki historia tu.

Wanawake huwa makini sana katika kufanya kazi.

Ndio maana hata magerezani
Wako wachache sana kupita maelezo!
 
Hi

Kuna kitu kinashangaza, hivi kwanini wanawake hawapewi nafasi sawa na wanaume kwenye kazi za udereva.

Je hawawezi, au Ni dhana ya kuwa mwanaume ndo ataweza kazi ya udereva.

Je kwa wewe mwanaume utakubali mke wako awe dereva?
Sio siri huwa nakereka sana na hizi mada ambazo huwa zinakua na vijishutma vya ubaguzi wa jinsia.
Mkuu nadhani ungeanza kwenye sehemu wanakoajiri hao madereva uangalie ni wangapi wanaomba na wakati wa usaili huwa inakuaje tutakua tumepata majibu.
 
Hawapewi nafasi kivipi mkuu? Mbona wanawake wanapewa vipaumbele sana!!

Pita pita kwenye sahili mbalimbali huko utagundua kitu.
 
Hi

Kuna kitu kinashangaza, hivi kwanini wanawake hawapewi nafasi sawa na wanaume kwenye kazi za udereva.

Je hawawezi, au Ni dhana ya kuwa mwanaume ndo ataweza kazi ya udereva.

Je kwa wewe mwanaume utakubali mke wako awe dereva?
Wanawake kwenye fani ya udereva wako wachache sana. Kwa hiyo likitolewa tangazo la madereva kati ya wanaoomba wanawake wanakua wachache mno. Na kwenye interview ya udereva ukikutana na mdada unagombania naye nafasi ya udereva na iko moja, na wewe ni mwanaume andika mamumivu, uwezekano mkubwa atapita mdada tu, maana mashirika mengi yanawapa kipaumbele kwa nafasi za udereva ili kuleta uwiano wa kijinsia kwenye nafazi za udereva, kwa sababu unaweza kuta shirika lina madereva 15 labda, ila mdada ni mmoja tu, au hakuna kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…