Katika pitapita yangu nimegundua kuwa kuna makampuni yana majina makubwa sana na heshima mitaani na midomoni mwa watu. Lakini nilichokibaini ni kwamba kampuni hizi nyingi zinapata faida baada ya kuwanyonya sana vijana, hasa wale wanaohitimu na wasio na ajira.
Mimi nazifananisha kampuni hizi na zile za kikoloni kama British East Africa Company, Germany East Africa Company nk.
Hebu tafakari, unapata kazi ya muda, Eti research, kufanya madodoso, unapelekwa mikoani kwa shilingi 17,000 tu kwa siku, nayo ikukimu malazi, chakula, mawasiliano yako, vinyaji, nk.
Halafu wanakuambia ukirudi baada ya research utapewa sh 10,000 kwa siku ulizofanya kazi, nayo ni baada ya kukagua kazi yote na isiwe na makosa.
Lakini kali zaidi ni kuwa hela hiyo huipati kwa wakati. Kuna taarifa kuwa kuna watu walifanya kazi kama hizo mwaka huu mwezi wa sita na hawajalipwa mpaka leo desemba.
WanaJF hapa ipoje.