Ajira za kuwa freelance | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira za kuwa freelance

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by MMOJA, Oct 12, 2012.

 1. M

  MMOJA JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45

  Inasikitisha sana hapa JF kwenye safu ya ajira, ikionekana tu kazi hiyo ni ya kutafuta masoko na kuzunguka na bidhaa mtaani(FREELANCE), Utasikia watu wanaanza kuleta dharau na kuisemea mabaya kazi hiyo, watu hao wamesahau kuwa watu wanatofautiana malengo na msimamo,hivyo kitu kwako inawezekana kikawa hakifai lakini kwa mwingine kikawa ni bora zaidi kuliko unavyofikiria,ni bora kama unaona haikufai ukapotezea na kulipita tangazo la hiyo kazi.
  Inabidi tufahamu kuwa malengo ya kazi yanatofautiana baina ya watu.Na pia hakuna nchi hata moja duniani ambayo imeajiri watu wote kukaa ofisini,lazima wapatikane watu wa kuwa wanafanya kazi field na ni ajira ya msingi kwa nchi yeyote ile duniani kwa kufanya kazi field.
  Japokua kazi hii ya freelance ina changamoto zake kama kujigharamia mwenyewe kwa pesa yako unapokua kwenye mazingira ya kazi kama kutoa nauli yako mwenyewe,kujigharamia chakula mwenyewe, jua lako,mvua yako na bado unaweza mwisho wa mwezi usilipwe kutokana na mauzo yatakavyoenda. Angalau kidogo forever and living product wameboresha kazi hii kwa kuweka SYSTEM OF NETWORK MARKETING.
  Ingawa wanaofanya kazi hii ya freelance wengi wao(sio wote) wanafanya kazi hizo baada ya kukosa fursa ya kazi za kukaa ofisini.Lakini bado si sababu ya kuidharau kazi hii.
  [FONT=&quot] Hivyo haipendezi kutoa dharau hadharani kuhusiana na hii kazi,wewe tafuta kazi unayoitaka [/FONT]
   
 2. Justin Dimee

  Justin Dimee JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 1,148
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Kweli.
   
 3. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Uko sawa kabisa kila mtu lazima aishi kulingana na ndoto zake alizonazo, lakini mimi nimeona hapa kuwa kuna watu wanavunja wengine moyo, ebu tuwe na mawazo endelevu kama wewe hutaki kazi ya aina fulani basi acha wengine wafanye
   
 4. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Kweli mkuu, kwanza watu wote hatuwezi tukawa tunafanya similar jobs, free lancers wanahitajika sana, na wapo, ukiona wewe siyo ndoto yako, waachie wanaoweza! mimi mmoja wapo siwezi kazi ya kuzunguka na bidhaa au kutafuta masoko, lakini napenda huduma zao, eg wanakufikishia bidhaa hadi ulipo, wanakueleza uzuri wa bidhaa hiyo na ukitaka kujua zaidi juu ya bidhaa hiyo unapata kinaga ubaga!!
   
 5. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wengi hawajui kuwa kazi ni kipato sio mazingra au ofis
   
Loading...