Ajira za JK zafikia 1.3 milioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira za JK zafikia 1.3 milioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Naibu Waziri Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Makongoro Mahanga (Kulia) akielezea mafanikio ya Wizara hiyo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, na jinsi walivyoweza kutenenza ajira kwa vinaja ikiwa ni ahadi ya serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.Kushoto ni Mkurugenzi wa Ajira wa wizara hiyo Ernest Ndimbo

  James Magai

  SERIKALI imesema hadi sasa imeweza kutengeneza ajira mpya zaidi ya 1.3 milioni, zikiwa ni zaidi ya lengo la ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, la kutoa ajira milioni moja, katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake.Pia imekiri kuwa kuna wajanja wachache waliojichotea fedha zilizotolewa na Rais, kwa ajili ya mikopo ya kuwaendeleza wajasiriamali wadogo, maarufu kama Mabilioni ya Kikwete.

  Hayo yalielezwa jana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa ahadi ya serikali ya kutoa ajira 1milioni.

  Dk Mahanga ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema serikali imeamu kutoa ufafanuzi huo rasmi ili kuondoa mashaka kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihoji kuhusu utekelezaji wake.

  "Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, imekuwa ikitoa takwimu za upatikanaji wa ajira mpya nchini tangu mwaka 2006. Pamoja na taarifa hizi, kumekuwepo baadhi ya watu wakiwemo wabunge, kuhoji takwimu hizi na mchanganuo wake," alisema Naibu waziri.

  "Tumeona ni vema tukatoa tena kwa umma taarifa hii pamoja na mchanganuo zaidi wa takwimu za ajira mpya zikionyesha wazi kwamba hata kabla ya miaka mitano haijakwisha, ajira zaidi ya 1milioni zilizoahidiwa na Serikali ya awamu ya Nne zimeshaanzishwa," alisema.

  Alifafanua kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005, ilieleza kuwa ajira hizo zinatokana na ajira rasmi kwenye sekta ya umma na sekta binafsi, na kwamba hiyo maana yake ni ajira za kuajiriwa na za kujiajiri.

  "Hivyo jumla ya ajira mpya zilizoripotiwa kuanzia Januari 2006 hadi April 2010 ni 1,313,561,"alisema Naibu waziri huyo.

  Alifafanua kuwa mwaka 2005 ajira zote zilizokidhi viwango vya ajira zilikuwa 4,842,605, lakini kufikia Desemba mwaka 2008 kulikuwa na ajira mpya 6,114,528, likiwa ni ongezeko la ajira mpya 1,271,923.

  Alisema kati ya ajira hizo (za ongezeko), sekta rasmi ilito jumla ya ajira 232,503 sawa na asilimia 18.3 wakati sekta isiyo rasmi ilitoa ajira 1,039,420 sawa na asilimia 18.7.

  "Aidha kuanzia Januari 2009 hadi April 2010 jumla ya ajira mpya nyingine 41,638 zimezalishwa kutoka sekta ya umma.Hivyo jumla ya ajira mpya zilizoripotiwa kuanzia Januari 2006 hadi Aprili mwaka huu ni 1,313,561," alisema Dk. Mahanga.

  Aliongeza kuwa takwimu hizo hazikumuishi takwimu za ajira mpya kwenye sekta binafsi za kuanzia Januari 2009 hadi April 2010 ambazo zinaendelea kukusanywa, wala takwimu za ajira mpya kwenye sekta za kilimo uvuvi na ufugaji za kipindi cha miaka minne toka mwaka 2006 .

  Ajira za JK zafikia 1.3 milioni

  Mzee J.K anajitahidi kikazi hongera
   
Loading...