Ajira yangu shindano kwa vijana

Aug 15, 2013
55
23
#TUNAANGAZA_FURSA

AJIRA YANGU BUSINESS PLAN COMPETITION.

Kuhusu Ajira yangu Business Plan Competition:
“Ajira Yangu Business Plan Competition” ni mpango mkakati wa kutatua changamoto za ajira kwa Vijana, Tanzania. Ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana nchini, Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), kwa pamoja wamebuni mpango huu. Mpango huu umebuniwa kwaajili ya vijana kupata ujuzi wa kuanzisha na kuendeleza biashara na kuwawezesha mitaji, ili waweze kuanza au kuboresha biashara zao, na kutengeneza nafasi za ajira kwao wenyewe na kwa vijana wengine.
Ushindani huu wa kuandaa mpango biashara, utawawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha au kuboresha biashara zao. Katika mashindano haya, vijana watatakiwa kuja na mipango rasimu ya biashara kwaajili ya mashindano katika sekta zifuatazo:

I. Biashara ya Kilimo na kilimo usindikaji ikiwa ni pamoja na viwanda.

II. Biashara inayohusu vyombo vya habari, masoko, mawasiliano, michezo, vifaa, sanaa na utamaduni, utalii na burudani.

III. Biashara inayogusa mazingira na utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na biashara ya kijamii.

IV. Biashara inayohusu habari na mawasiliano, teknolojia ikiwa ni pamoja na usindikaji.

Vijana 6 wenye mawazo bunifu watapewa mtaji ili waweze kuanzisha au kuboresha na kukuza biashara zao.

Sheria na masharti ya mashindano.

a)Waombaji lazima wawe ni vijana wa kitanzania wenye miaka kati ya 18-35.

b)Waombaji lazima wawe wanzilishi wa kampuni au biashara.

c)Biashara lazima iwe na msingi na ifanye kazi Tanzania.

d)Waombaji wanaweza kuwasilisha maombi mara moja tu.

e)Majibu lazima yasizidi kiwango cha maneno kilichowekwa.

f)Maombi lazima yatumwe katika mfumo wa PDF.

g) kanuni na masharti haya zinaweza kubadilishwa na waandaaji wa shindano hili.

Mwisho wa maombi na Tarehe muhimu
• Uzinduzi wa maombi: Aprili 18, 2016.
• Tarehe ya mwisho: Mei 9, 2016.
• Washindi kutangazwa: 13 Juni 2016.

Maelezo jinsi ya Kutuma maombi:
Maombi yanaweza kutumwa kupitia;
Barua pepe:

ajirayangu@uwezeshaji.go.tz

Kwa maombi ya mtandaoni yanaweza kupakuliwa kutoka:

www.uwezeshaji.go.tz

Kwa mawasiliano au maswali yoyote zaidi tumia
Shirika la Kazi Duniani,
S.L.P. 9212
Dar es Salaam Tanzania
Simu: +255 22 2196700
Simu ya mkononi: +255 786 110060 Barua pepe: daressalaam@ilo.org

AU

Baraza la uwezeshaji wananchi Kiuchumi, S.L.P 1734,
Dar es Salaam,
Simu: +255 22 2125596
Barua pepe:ajirayangu@uwezeshaji.go.tz
Tovuti: www.uwezeshaji.go.tz
 
Back
Top Bottom