Ajira ya Muda

Mtumaini Mungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2021
Posts
879
Reaction score
1,084
Habari Wakubwa!

Mimi ni kijana wa miaka 27, ninasoma UTABIBU nipo MWAKA wa pili sasa.

NINAOMBA KUPEWA AJIRA/KIBARUA CHA MUDA ILI NIPATE ADA YA KUJISOMESHA MWAKA WA MWISHO.

Hivi sasa tuko kwenye maandalizi ya MTIHANI wa MWISHO wa MWAKA wa pili, (Tabibu Msaidizi), mitihani hii itaisha mwezi wa tisa katikati, toka hapo nitakuwa na uwezo wa kufanya/kusimamia kazi yoyote ya Halali itakayo patikana.

Kazi ikiwa ni Mambo ya Afya (Zahanati, Duka la Dawa, Maabara, n.k) Biashara (Kusimamia/Kuuza), Kufundisha (Masomo YOTE, hasa Sayansi kuanzia Kidato Cha kwanza Hadi Cha sita/PCB), Au KIBARUA chochote Halali.

Sifa zangu.
1.Elimu Kidato Cha Sita PCB, 2014. Kwasasa namalizia Masomo ya Fani ya UTABIBU mwaka wa pili (Clinical Assistant)
2.Mpole, Nina HOFU ya Mungu.
3.Ninao uwezo wa Kujisimamia/Kusimamiwa katika kazi yoyote.
4.Nimehitimu mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa, Hivyo Mkakamavu na Mwenye kujituma.
5.Naongea na kuandika Kiswahili na Kiingereza Kwa Ufasaha.
6.Mwaminifu Sana.

Kwasasa nipo Mtwara, Ila naweza kufikia popote AJIRA/KIBARUA kitakapo patikana.

Naomba msaada wako, wa Mawazo, Mali, na Hali katika hili.

Ubarikiwe.
 

Unasoma chuo gani..?!
 
Umeandika vizuri sana, hpo utafanikiwa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…