Ajira Tanna Sreekumar & Co.

masaumbe

Member
Joined
May 28, 2013
Posts
42
Reaction score
11
Habari za Jioni Wadau,naomba kujuzwa Mishahara ya Tanna Sreekumar & Co. kwnye nafasi za Audit.Natanguliza shukrani za dhati
 
hapo ukiwa muhindi halafu umemalizia india degree ya kwanza mshahara 1,500,000/=
ukiwa muhindi umemalizia bongo mshahara 800,000/=
ukiwa mtanzania umemalizia tanzania 350,000 mpaka 500,000.nenda kajaribu bargaining yako kazi wanazo sana utakuwa vizuri kwenye kazi.
 
kama wamekuita kwenye usahili nenda jamaaa wapo vizuri sana kwenye kufundisha kazi ukitoka pale sehemu yeyote unafanyakazi za consultancy,auditing,accounting etc ila kwa malipo wanabana sana haswa kwa ngozi zetu weusi kama ni wewe indian lazima uchukue mpunga mrefu wa mzee TANNA SOMAIYA ,CPA -PP no 2, after mzee reginald mengi CPA PP no 1
 
Io 350,000 ni kwa mbongo mweny Cpa au graduate was kawaida?
 
Je wabongo wanapata zile Kazi za nje ya mkoa kufanya kazi au ndio Indian first Choice?
 
Kama una element za uvivu usikanyage pale.Kama ni slow learner hawana muda wa kuvumilia.msemo wao maarufu ni kufanya kazi haraka without compromising the quality na hawana mchezo.
Pale kazi utajifunza kisawasawa.
Kama unauzoefu wa audit mishahara yao si mibaya hasa ukiwa na CPA.
Ila mzigo wa pale lazima ujipange hakuna lelemama na kazi kibao.
 
Mrazamo inaelekea ww ulikuwepo pale kipindi fulani maana hiyo ndio slogan ya kumar, no compromise on quality. Mtazamo waswahili wapo kweli pale kwa ss?
 
Habari za Jioni Wadau,naomba kujuzwa Mishahara ya Tanna Sreekumar & Co. kwnye nafasi za Audit.Natanguliza shukrani za dhati

Tuambie mkuu Masaumbe, umeshafanyiwa interview na Tanna Sreekumar & Co, vp kuna uelekeo wa maisha pale maana waswahili hatuna tendence ya kukaa pale maisha ya pale ni uhindi zaidi.
 
hii thread imenigusa sana! kama kazi yangu tuu! na kesho pia naenda kazin!! saiz nmekua expert idara zote!! marketing. finance. purchase. sale. administrator. data entry.accounts.auditor. store keeper. wahindi noma sana!! mshahara ule ule wa mwaka Jana
 
Yap Mkuu,nimegonga Interview mbili mzee,Aptitude dk 15 swali moja,I scored 95,then after five mins,akaja jamaa mmoja anaitwa Kapil,oral mkuu,so after one week watanijibu wakuu,I have one week ya Sala na maombi,am tired of staying home aisee
 
Yap Mkuu,nimegonga Interview mbili mzee,Aptitude dk 15 swali moja,I scored 95,then after five mins,akaja jamaa mmoja anaitwa Kapil,oral mkuu,so after one week watanijibu wakuu,I have one week ya Sala na maombi,am tired of staying home aisee

Masaumbe hiyo sasa ni FIX, watu tunapajua sana pale Tanna Kumar huwa hakuna taratibu za APTITUDE TEST ww ndio wa kwanza kusikia kwako, tulipomaliza UDSM na jamaa zangu watatu tulienda pale tumepiga interview ORAL TU hiyo kitu ya Aptitude haijawahi tokea. Na tunavyomjua Kapil hana maswali ya ajabu sana sana ni mambo ya kodi (TAX) kidogo ndio anajua lakini audit kama audit mweupe tu yule. Njoo Innovex/BDO uone mziki kaka. Mshahara laki 350 hakuna contract wala nn, ukichemka unaaga mwenyewe au unasepa kama wengine wanavyowafanyia.
 
Mambo hubadilika mkuu,kama uko hapo muulize huyo dada wa Reception,Great thinker tunaenda na fact,do it then proof my wrong
 
Innovex Safi sanaa,Peleka Salamu zangu kwa Mwanaisha Mchomba
 
Mambo hubadilika mkuu,kama uko hapo muulize huyo dada wa Reception,Great thinker tunaenda na fact,do it then proof my wrong

Kaka pale nimesha attend interview mara moja mwaka huu (May), experience ya pale interview haichukui zaidi ya dk 7 sasa nakushangaa ww unataka kuwafagilia anyway huenda hayo mabadiliko yameanza kuanzia mwezi wa sita kuendelea maana mwezi wa tano ndio nimefanya interview pale. All the best kaka jiandae kula pili pili kwa kwenda mbele.
 

Kweli kabisa hakuna APTITUDE TEST pale TANNA wao wanajua vitu gani basic walau uwe unajua kama huna experience na kama una uzoefu sana sana maswali ya kodi na basics za audit.Mimi nawajua vizuri sana hasa Kapil (Audit Manager) hana maswali mengi yule.

Pale kazi zao sometimes hata wahindi wanachemka jinsi wanavyokupiga pressure kwa mshahara mdogo.Wewe nenda kwa lengo la kujifunza kazi ili uweze kutengeneza CV yako basi.
 

Mtazamo nimekupata, uko kampuni gani kaka kwa jinsi unavyo comment nahisi umepita pale japo miezi kadhaa, nasikia Tanna Kumar wana msemo wao wanaita Peak Period kulala kwa ofisi ni kawaida. Mambo hiyo Inovex wala BDO hatunaga hizo. Wajuzi wa kwenye audit Firm hii kitu Peak Period ipo. PWc na wengine wakongwe tuambieni tafadhali maaana ss BDO na Innovex bado wachanga kwenye fani
 
Inabidi kwenye makampuni ya weusi tusiwaajiri weupe" bado ubaguzi wa rangi unaendelea hadi saivi
 
Ndugu zangu,Kwanza namshukuru mungu coz Leo nimepigiwa simu ya Kuanza kazi pale next monday,kesho naenda kusain contract ya one year,so kesho nitawajibu maswali yenu yote,tukubaliane na tusikatae mambo hubadilika,kazi siku zote ni daraja la kumfanya mtu apite upande wa pili wa maisha.Nimefanya kazi TAC Associate as trainee,mshahara ni mdogo,but safari ni nyingi sanaa,so kwa mwezi wakati wa peak za kazi,unaweza ukajikuta una hata 4M
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…