CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 4,984
- 4,083
SEREKALI KUAJIRI WATUMISHI ELFU KUMI NA TATU SEKTA YA AFYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha kuajiri watumishi elfu 13 katika sekta ya afya ili wapangiwe kufanya kazi kwenye vituo vya kutolea huduma hiyo kote nchini.
Hayo yamebainishwa lNovemba 30, 2023 na Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI ambaye ni Mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi - CCM mbele ya viongozi wa chama hicho na wananchi kwenye viwanja vya Ujamaa Ikwiriri, Rufiji.
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuto ajira kwenye sekta ya afya na Rufiji imeendelea kupokea maafisa afya katika maeneno mbalimbali na hivi karibuni ameshatoa kibali cha kuajiri maafaisa afya, waganga (madaktari) takribani elfu 13, watakapoajiriwa, watapangiwa kazi kwenye vituo vyote vilivyojengwa wakati wa awamu ya sita kote nchini" amesema.
Mchengerwa ametoa taarifa ya kibali hicho cha Rais alipokuwa akifafanua maendeleo ya sekta ya afya kwenye Jimbo lake la Rufiji ambapo amesema kuwa katika kipindi cha 2021 hadi 2023 vituo vya afya vimeongezeka kutoka vinne hadi sita, Zahanati zimeongezeka kutoka 23 hadi 30 na akaongeza kuwa pamoja na mambo mengine, wamekamilisha ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa jengo la Mionzi katika Hospitali ya Wilaya na vyote hivyo tayari vimeanza kutoa huduma kwa wana Rufiji.
"Tunaishukuru Serikali, kwani katika kipindi cha kuanzia Mwezi Julai, 2023 hadi Oktoba, 2023 tayari Sekta ya Afya imepokea jumla ya Shilingi 1,438,848,000.00 ambazo zimeanza kutekeleza miradi ya Ukarabati wa Miundombinu ya Hospitali ya Wilaya, Ukamilishaji wa Zahanati na Ujenzi wa Zahanati Mpya, Ujenzi wa Matundu ya vyoo na Miundombinu yake na Ukamilishaji wa Jengo la Wodi ya Wazazi, ameeleza.
Mchengerwa ameongeza kuwa vifaa tiba vimepelekwa katika vituo vyote vya afya na kuwa pamoja na uwepo wa Hospitali ya wilaya, kiasi cha sh. Bil. 10 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya kisasa itakayotoa huduma za kupokea na kuhudumia Wagonjwa.