Ajira mpya 15000 kabla ya 30 June

matyhans

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
610
400
Serikali kutangaza ajira mpya 15000 ndani ya miezi miwili kabla ya mwaka wa fedha 2016/2017 kuisha

=====

Mpango huo ulitangazwa jana mjini hapa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Dk. Laurian Mdumbaro, kwa vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa Dk. Ndumbaro, kutokana na uamuzi huo, waajiri wanatakiwa kuhakiki vyeti vya watumishi walioomba ajira kabla ya kuwaajiri.

“Wanatakiwa kuhakiki kabla watumishi hawajaajiriwa, wanatakiwa kuhakikisha vyeti vya waliomba kazi au usahili viwe vimehakikiwa na mamlaka husika kama ni cheti cha kidato cha nne, sita au ualimu au vyovyote viwe vimehakikiwa na mamlaka husika,” alisema.

Dk. Ndumbaro alielekeza kuwa vyeti vihakikiwe na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) au chuo chochote kile kiwe ni chuo kikuu au vya Mamlaka ya Ufundi Stadi (Veta), vihakikiwe kabla hawajapata ajira mpya.

ATHARI KUONDOA WENYE VYETI FEKI

Wakati huo huo, Dk. Ndumbaro alisema kutokana na kuwaondoa watumishi wenye vyeti feki, kuna maeneo yameathirika kihuduma na kuwaagiza waajiri kwenye maeneo hayo kuwaandikia barua au kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu Utumishi ili kutoa kibali cha ajira cha dharura.

Alisema kibali hicho kitatolewa ili huduma zisiathirike.

“Waajiri wote kwenye serikali za mitaa na sekta za umma kwenye maeneo ambayo yameathirika sana na zoezi hili la vyeti feki watoe taarifa kwa Katibu Mkuu Utumishi mara moja ili kutoa vibali vya dharura waweze kuajiriwa watu wenye sifa kufanya kazi hizo,” alisema Dk. Ndumbaro.

Alipoulizwa kama ajira zilizotangazwa zinalenga kuziba pengo la watumishi walioondolewa kwa vyeti feki, alisema bado kuna watu wanakata rufani na nafasi zilizotangazwa ni zaidi ya idadi ya watumishi wenye vyeti feki.

“Tulikuwa na mpango wa kuajiri, mwanzoni tuliajiri watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, walimu wa sayansi, madaktari tulikuwa kwenye mwendelezo huo wa ajira hizo. Hii ikikamilika tutatoa ajira zingine,” alisema.

Kuhusu mchanganuo wa ajira, Katibu Mkuu huyo alisema mchanganuo wa ajira hizo utatolewa kwa kuainisha kada zote kulingana na idadi hiyo.

“Kuhusu ajira elfu 71 zilizotangazwa zilikuwa ni za mwaka 2015/16, lakini mwaka ule yalifanyika mambo mengi… kulikuwa na programu ya kuweka sawa mishahara ya walimu wa vyuo vikuu waliokuwa wakipata mishahara tofauti,” alisema.

Alisema sehemu ya fedha zilizotengwa kwa ajira hizo ilitumika kuweka sawa mishahara ya walimu hao wa vyuo vikuu na kuwapadisha vyeo watumishi ambao hawakupandishwa kwa muda mrefu.

“Fedha zilizobaki tumeendelea kutoa ajira awamu kwa awamu,” alisema Dk. Ndumbaro.

Chanzo: Nipashe
 
IMG-20170504-WA0009.jpg
IMG-20170504-WA0010.jpg
 
Mwaka jana walisema watatoa ajira 70,000. Juzi Rais alisema watatoa ajira 52,000. Jana katibu mkuu Ndumbaro kasema watatoa ajira 15,000 tu...

Kauli tatu tofauti. Serikali moja.... Kuongoza nchi sio mchezo
Huyo Ndumbaro ulimsikiliza vizuri au umeshikilia 15000 tu... hizo elfu 15 ni za dharura na zile elfu 52 sio za mwaka huu wa fedha zile ni 2017/2018 lakini hizi 15000 ni ndan ya kipindi hichi cha miezi miwili kabla ya mwka wa fedha 2016/2017 kuisha
 
Asante sana Mkuu kwa kunielewesha...
 
Huyo Ndumbaro ulimsikiliza vizuri au umeshikilia 15000 tu... hizo elfu 15 ni za dharura na zile elfu 52 sio za mwaka huu wa fedha zile ni 2017/2018 lakini hizi 15000 ni ndan ya kipindi hichi cha miezi miwili kabla ya mwka wa fedha 2016/2017 kuisha

Hizi stori tu kila siku wanasema ''wataajiri''........''wataajiri'' ila hatuoni wakitoa hizo ajira, bora wakae kimya sasa.
 
Sawa ni ajira za dharura mbona hawajatoa mode of application waombaji wataombaje kwa email kama wale waliotakiwa kwenda kenya? Au kwa barua kwenda kwa katibu mkuu?
 
Wanaotakiwa kuhakiki waajiriwa wapya wamekumbwa na zoezi la vyeti feki.

Hapo vipi?
 
Sawa ni ajira za dharura mbona hawajatoa mode of application waombaji wataombaje kwa email kama wale waliotakiwa kwenda kenya? Au kwa barua kwenda kwa katibu mkuu?
Swali zuri sana...huyo katibu mkuu hajaweka bayana...wataombaje kazi....au tayari washaomba kimya kimya?? Au zitatangazwa? Hii taarifa haina mbele wala nyuma...mtoa mada iweke sawa...au umekrupuka tu ili upate like nying
 
wewe ndio umekurupuka kuComment.. nimeweka Link hapo ingia usome sio unaleta blah blah
 
Back
Top Bottom