Ajira kwa vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira kwa vijana

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Jpinduzi, Nov 14, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu Marafiki ni matumaini yangu ya kuwa tunaendelea vizuri na shughuli za kijamii pamoja na ugumu wa maisha ya kila siku.Leo hii napenda kuchangia juu ya maada ifuatayo''Ajira kwa Vijana'' hii ni changamoto iliyopo mbele yetu hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa yanayochangiwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia.Mkutano wa ''Ajira ya Vijana'' Youth Employment Summit uliofanyika Alexandria nchini Misri mwaka 2002 yalijadiliwa mambo kadhaa kubwa likiwa ni tatizo la ajira kwa vijana.

  Sera ya ajira,ajira ya vijana ipo katika maeneo mawili sekta rasmi (Formal sector) na sekta isiyo rasmi (Informal sector).Katika sekta rasmi vijana utegemea kuajiriwa na kulipwa mishahara,sera ambayo kwa hapa Tanzania na kwingineko duniani serikali zimekwisha jitoa.Hapa Tanzania hali hii imesababisha uchumi kuporomoka na hivyo hivyo ukosefu wa ajira kuongezeka kwa kuwa maeneo ya ajira kama viwanda,mashirika,mashamba makubwa yamebinafsishwa baada ya kuhindwa kujiendesha kwa faida.

  Baada ya ubinafsishaji viwanda,mashirika n.k vimekuwa katika hali ya kuleta mabadiliko yenye ushindani lakini kwa kiwango cha chini bila mafanikio makubwa.
  Pia tatizo lingine ambalo naliona ni ukosefu wa mfumo mzuri wa elimu kwa vijana,hali hii inasababisha vijana wengi kushindwa kupata ajira pindi wamalizapo shule kutokana na kukosa elimu ya vitendo,mashuleni ufundishwa zaidi nadharia ambayo haiendani na mazingira halisi.

  Pia kwa mawazo yangu nafikiri kuwa serikali lazima ifanyie mabadiliko sera ya uwekezaji.,wawekezaji watoe kipaumbele na kuongeza ajira kwa vijana wenye sifa ikiwa ni pamoja na kuwaendeleza kitaaluma ili waweze kutoa mchango mkubwa kwa taifa lao ambalo linawategemea kwani wao ndio nguvu kazi.Pia serikali isiruhusu uwekezaji holela kama kuwekeza katika kutengeneza dawa za kienyeji,ukulima wa matunda na nyingine nyingi shughuli hizi waachiwe vijana na wazawa.Vijana waelimishwe juu ya mambo yanayowahusu kama vile kujua sera za maendeleo zinazowahusu wao.
  mimi naamini vijana wakiwezeshwa wanaweza endapo watajituma na kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa yao na wengine.Ahsanteni​
   
 2. URASSA THE DON

  URASSA THE DON Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mfumo mzima wa elimu tanzania ni finyu kama ulichokiandika hapo
   
 3. frank lujaju

  frank lujaju Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee yote uliyoyasema ni sahii,ivi rafiki unafikiri ili tatizo ni la kuisha leo ama kesho?tatizo ili litaendelea kututesa vizazi mpaka vizazi coz hatuna viongozi wenye kujali masilahi ya vijana na hata ho tunaowalilia waingie madarakani bado watacheza mule mule tu,viongozi wenye uchungu na nchi washaondoka ,kilichobaki ni kugawana tu kilicho baki,ungugulization kwenda mbele ,daah survival for the fittest
   
 4. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mawazo yako mazuri ila yafikishe kwa wahusika - Kabaka, Makongoro na Shitindi. Labda wataweza kuyafanyia kazi.
  Sidhani kama nitarajie jambo lolote jipya.
   
 5. b

  babacollins JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 879
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Cha msingi ulichokianzisha ni mjadala tu lakini mawazo yako yanakinzani tatizo ni hakuna ajira au kuna ajira na vijana hawana elimu au hawajitumi? kwa mtazamo wangu elimu inayotolewa bado kwa kiasi fulani inaweza kutumika kwa mazingira tuliyonayo. Bado kuna watu wengi wanatumia elimu hihii tunayoidharau kufanya mambo mazuri kwenye ajira zao(sio ufisadi tafadhali). Pia tusisahau elimu haina mwisho mapungufu tuliyonayo kwa mfumo huo wa elimu tuyatafutie ufumbuzi tukiwa kazini hata kujifunza kuongea kingereza manake wengi wetu ndio upungufu(au kikwazo kwenye usaili?) tunaoufikiria. Suala la kuboresha maeneo yanayotoa ajira hilo naliunga mkono kabisa ni chanzo cha watu wengi kukosa ajira. n.k n.k
   
 6. Elly B

  Elly B JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 1,194
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ajira bado zipo ingawa ni kwa uchache. Lakini hata inapokuja hapo kwenye kuajiriwa bado watu wengine wanakosa "sifa muhimu" zinazohitajiwa na waajiri siku hizi. Bahati mbaya hao wawekezaji(wachukuaji) wa kigeni ndio ambao wanaweza kutoa nafasi fair za ajira,ingawa ni katika nafasi ambazo huenda hazivutii sana. Ila ukija kwa ajira za kibongo Lazima uwe na sifa zifuatazo:
  1.Uwe na ndugu au jamaa anayekujua. Hata kama huna sifa Bosi kazi utapata.
  2.Ujue kula nao.
  Bahati mbaya hili limeshaingia serikalini longi. Kama hawalioni vile! Ukitaka mfano uliza bandari.
  HUENDA KUNA HAJA YA KUANGALIA NAMNA MPYA YA KUPATA LUGHA SAHIHI YA KUTUMIA ILI WATU WASIENDELEE KUATHIRIKA ZAIDI.
   
Loading...