Ajira kibao: Outsourced freelancing!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira kibao: Outsourced freelancing!!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Kichuguu, Jun 16, 2012.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ndugu watanzania, hasa wasomi wanaograduate katika fani za Computer Science (hasa programming katika lugha mbalimbali), Engineering (hasa CAD design na analysis), English Language (hasa writing), statistics, marketing (graphic design) na Accounting. Kuna ajira nyingi sana za freelancers hutangazwa katika mitandao ya www.elance.com, www.freelancer.com, www.guru.com, www.vWorker.com na www.oDesk.com ambazo unaweza kuzifanya ukiwa hapo hapo ulipo hata kama mwajiri anaishi Marekani. Utaratibu wake ni wewe kujiandikisha kwenye mitandao hiyo (bila malipo yoyote) halafu unapitia kazi zlizotangazao pale. Iwapo utakuta kuna kazi unayoweza kuifanya, basi unatuma maombi yako kwa kushindana na wengine wanaotaka kazi ile pia (bidding.) Utaeleza ujuzi wako kulingana na kazi hiyo, na kiasi unachotaka ulipwe kwa saa au kwa kazi yote. Mwenye kazi atawasiliana nawe kwa email halafu mikubaliana mnapeana mkataba na unaanza kazi ukiwa nyumbanni kwako. Ukimaliza kazi unamtumia mwajiri huyo halafu unatumiwa pesa yako kwa njia utakayotaka mwenyewe: Paypal, Moneygram, Westernunion au hata kwa bank direct deposit ingawa hiyo huweza kuchukua muda mrefu. Kuna kazi nyingine unaweza kulipwa downpayement ya 30% to 50% kulingana na mtakavyokubaliana.

  Ninavolunteer katika organization moja inayosaidia vijana kupata kazi katika mazingira ya leo ambapo kazi zimekuwa adimu, na juzi tulikuwa na kongamano fulani kuhusu kuwawezesha vijana kujiajiri na kujipata wateja wa kutoka mbali. Mtoa mada mmoja alizungumzia ajira hizo za freelancing na kuwasihi vijana wasiwe wanadai malipo makubwa sana kwa vile ni afadhali kupata kidogo kuliko kukosa kabisa. Baadaye nimekaa na kufanya utafiti wa kina kuhusu mitandao hiyo nikagundua kuwa kazi nyingi hutoka nchi za magharibi ambako labor cost ni kubwa sana, halafu watu wengi wanaozipata huwa ni watu wa Asia (hasa India, Pakistan, Bangldesh na China) ingawa siku za hivi karibuni kumekuwa na waafrika wachache kutoka Kenya na South Africa ambao wamekuwa wakizipata pia. Utakuta kazi ambayo mmarekani angetaka alipwe dola 50 kwa saa, anapatikana mtu kutoka bangladesh mwenye qualification zaidi ya yule mmarekani na yuko tayari kuifanya kazi hiyo kwa dola 5 hadi 10 kwa saa. Nina imani kuwa kuna vijana wa kitanzania wanaoweza kufanya kazi hizo pia kwa kushindana na hao wabangladesh na wakafanikiwa. Kazi nyingi zina kiwango cha masaa 40 kwa wiki, kwa hiyo mapato kati ya 200 hadi dola 400 kwa wiki ni ajira nzui sana, na hasa kumbuka kuwa unaweza kufanya kazi za namna hiyo mbili au tatu kwa mpigo na hivyo kujipatia hadi dola 1200 kwa wiki.

  Haya vijana wa kitanzania, changamkieni tenda hizo!
   
 2. N

  Nyakwec's Bro JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  thankx bro,dat nyc!....
   
 3. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ntatembelea hiyo web nijionee mwenyewe
   
 4. pettymarcel

  pettymarcel JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 1,433
  Likes Received: 611
  Trophy Points: 280
  vp kwa watu tuliosomea mambo ya jamii tunaweza kufanya application?
   
 5. KML

  KML JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kaka asante ingawa tatizo kubwa la wabongo kazi wanajua sema sasa lugha ya kigeni ndo tatizo sasa katika kucommunicate na uyo anaetoa ajira ndo utata kwa wengi unapoanzia.nafikili kama kuna madalali wanaoweza kusaidiana na wabongo katika hili si mbaya wakiwasaidia
   
 6. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Tatizo ni watu kama wewe daima mnatafuta sababu za kuwavunja moyo wenzenu
   
 7. pettymarcel

  pettymarcel JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 1,433
  Likes Received: 611
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa watu wanapenda kukatishana tamaa
   
 8. KML

  KML JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  tatizo m bongo cku zote ukimwambia ukweli anakua mkali sana ila huo ndo ukweli kubali kataa
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ni kweli lugha inaweza kuwa tatizo, isipokuwa kuna kazi nyingi ambazo hazihitaji ujuzi wa lugha. Unaweza kumtafuta mtu akusaidie kuandika profile yako vizuri halafu ukawa unaomba kazi ambazo hazihitaji lugha kwa makali sana; kwa mfano programming, website development, CAD design, graphic design, statistical analysis, na accounting hazihitaji ujuzi mkubwa sana wa lugha zaidi ya utaalamu wenyewe.
   
 10. Edoedward1

  Edoedward1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 799
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 60
  Thanks for the tip bro!!! i do appreciate very much
   
 11. M

  MTK JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Bravo, contribution kubwa sana hii umetoa, keep it up. kazi kwao vijana !!
   
 12. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na kazi nayo atakufanyia dalali?
   
 13. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Iga vingine lakini si UDHAIFU...
   
 14. pettymarcel

  pettymarcel JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 1,433
  Likes Received: 611
  Trophy Points: 280
  Hahaha nimeipenda
   
 15. i

  iyomana Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Unaweza kueleza kifupi jinsi ya kujiunga? Au kutoa mifano na contact za Mtanzania yeyote anayefanya kazi na kulipwa online ili anisaidie. Maana nikitembelea hizo website, hazionyeshi kuwa unaweza kupata kazi moja kwa moja.
   
Loading...