Ajinyonga Live Kwenye Internet Baada ya Kutoswa na Mpenzi Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajinyonga Live Kwenye Internet Baada ya Kutoswa na Mpenzi Wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Monday, September 07, 2009 2:01 AM
  Mwanaume mmoja wa nchini Chile amejinyonga live kwenye internet baada ya uhusiano wake na mpenzi wake kuvunjika. Polisi wa Chile walisema kuwa kijana huyo ambaye alikuwa na stres za kuvunjika kwa uhusiano wake na mpenzi wake alijinyonga huku mpenzi wake huyo akiangalia Live kwenye internet kwa kupitia webcam.

  Polisi walisema kuwa kijana huyo aliyejulikana kama Simon Venegas mwenye umri wa miaka 26 kabla ya kujinyonga alikuwa akichati kwenye Yahoo Messenger na mpenzi wake huyo wa zamani ambaye uhusiano wao ulivunjika mwaka mmoja uliopita.

  Wakati wakiendelea kuchati huku wakionana kwa kutumia webcam, Venegas aliielekeza kamera ya webcam yake kwenye mti uliokuwepo mbele ya nyumba yake.

  Polisi waliendelea kusema kuwa Venegas alitengeneza kitanzi kwenye mti huo na kisha kumwambia mpenzi wake "Angalia kitu nitakachokifanya, Nakupenda, kaa salama" na kisha alijinyonga.

  Mpenzi wake huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 23 alishtushwa na kitendo hicho na alianza kuwapigia simu marafiki wa Venegas ili wamzuie asijiue lakini walipowasili Venegas alikuwa tayari ameishafariki.

  Uhusiano wa Venegas na mpenzi wake ulivunjika mwaka mmoja uliopita lakini inasemekana kuwa Venegas alikuwa hajaridhia uhusiano huo kuvunjika.

  Tukio hilo la kujinyonga lilitokea ijumaa kwenye mji wa San Felipe, uliopo takribani kilomita 90 toka mji mkuu wa Chile, Santiago.

  Polisi walitoa taarifa ya tukio hilo jana jumapili.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3018286&&Cat=2
   
Loading...