Ajinyonga kwa kanga, aacha mtoto wa miezi tisa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
Manyoni. Mtu mmoja amekutwa amejinyonga kwa kanga hadi kufa akiwa nyumbani kwake eneo la Mamatatu, kijiji cha Muwanzi nje kidogo ya Hopitali ya Wilaya ya Manyoni.

Diwani wa kata hiyo, Maghembe Machibula amesema tukio hilo limetokea jana Jumatatu saa tatu asubuhi.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumanne, Machibula amesema kabla ya kujinyonga, marehemu alienda katika mgahawa wa Agnes Charles kwa ajili ya kunywa chai huku mgongoni akiwa amembeba mtoto wake mwenye umri wa miezi tisa, mgongoni.

“Kabla hajanywa chai alimuacha mtoto wake kwa mhudumu huyo kwa madai ya kwenda kujisaidia lakini hakurudi na baadaye ndipo ilipobainika kuwa alikwenda kujinyonga,” amesema Diwani huyo.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Jamil Mbwana amethibitisha kutokea tukio hilo ingawa alidai hana taarifa zaidi za marehemu kwa kuwa ni mhamiaji.


Chanzo: Mwananchi
 
Dah... imagine unakuwa unakuta hiyo stori eti mama yako alikuacha mikononi mwa mtu hotelini akaingia kujinyonga! Mungu ampe wepesi mtoto
 
Hapo usikute chanzo ni njemba lililotundika mimba limelala mbele!
 
Mama alikuwa kwenye mawazo ya kiwango cha juu kabisa. Mungu amkuze vyema mtoto. Pumzika kwa Amani mama. Lakini kama chanzo ni mwanaume aliye zaa nae, Mungu Mapenzi yako yatimizwe. Amen
 
Akizungumzia tukio hilo leo Jumanne, Machibula amesema kabla ya kujinyonga, marehemu alienda katika mgahawa wa Agnes Charles kwa ajili ya kunywa chai huku mgongoni akiwa amembeba mtoto wake mwenye umri wa miezi tisa, mgongoni.
 
HUWA NACHUKIA SANA KUSIKIA MTU KUJIUA KIKATILI KAMA KUJINYONGA,HALAFU TENA UNAACHA MTOTO,AFU MTOTO MWENYEWE MDOGO,TENA MCHANGA WA MIEZI MICHACHE??!!!!
 
Back
Top Bottom