Ajinyonga kupinga mama yake kuolewa kwingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajinyonga kupinga mama yake kuolewa kwingine

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Maria Roza, Mar 14, 2010.

 1. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  MWANAFUNZI Simon Joseph (15), aliyechaguliwa katika awamu ya pili kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Iyela, amejinyonga hadi kufa akipinga mama yake kuikimbia familia na kwenda kuolewa na mwanamume mwingine.

  Inadaiwa mwanafunzi huyo alifikia uamuzi huo akipinga mama yake kuolewa na mwanamume mwingine na yeye kuchoshwa na kubeba mzigo wa kuwahudumia wadogo zake, ambao alikuwa akiwapikia pamoja na huduma nyingine za kawaida za nyumbani.

  Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Kata ya Iyela katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Ambakisye Mwasumbi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa tano asubuhi nyumbani kwa familia ya mwanafunzi huyo eneo la Airport.

  Alisema inadaiwa kabla ya kujinyonga, Simoni aliwaambia wadogo zake kuwa amechoshwa na adha ya kuwalea baada ya mama yao Esther Yona kuwakimbia na kuolewa na mwanamume mwingine; akidaiwa alisema ni afadhali afe.

  Alisema inadaiwa wadogo zake watatu walijaribu kumzuia na kumshauri asitimize azma hiyo, lakini aliwatisha kuwachoma kwa kisu alichokuwa amekishika, ndipo baada ya kutishiwa walikimbia na kumwacha peke yake.

  Aidha, Mwasumbi alidai kuwa baada ya wadogo zake kukimbia na kumwacha peke yake, kijana huyo alitoka nje na kupanda juu ya mwembe uliopo nyumbani kwao na kujinyonga kwa kutumia waya wa simu za TTCL.

  Diwani huyo alidai wadogo zake walimuona alipopanda kwenye mwembe na kujirusha, ambapo walipiga kelele za kuomba msaada, lakini hadi watu wanafika kutoa msaada alikuwa amekwishafariki.

  Mume wa Esther aliyetambuliwa kwa jina moja la Joseph, alishindwa kuzungumza lolote ambapo inadaiwa tangu akimbiwe na mkewe ni miezi miwili imepita na kwamba alikwishatoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Mtaa.

  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Advocate Nyombi hakupatikana kuthibitisha tukio hilo, ambapo ilidaiwa na Katibu Muhtasi wake kuwa yupo kwenye kikao cha siku nzima na hivyo hawezi kuonana na waandishi wa habari.

  Simon alikuwa aanze masomo ya kidato cha kwanza Machi 15, mwaka huu katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Iyela ambapo inadaiwa baba yake alikuwa tayari ameshamfanyia maandalizi yote ya shule  http://bongoyetu.com/the-news/468-ajinyonga-kupinga-mama-yake-kuolewa-kwingine.html
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  mhhh......
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha!!
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  mno.....
  wakinga hawa nahisi...
   
 5. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Shit!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,641
  Likes Received: 82,289
  Trophy Points: 280
  Maskini we! aliachiwa mzigo mzito uliomzidi kimo. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,827
  Likes Received: 1,996
  Trophy Points: 280
  It pains alot
  Kwa umri wake alikosa ushauri ndio maana akafikia kuchukua hatua hii ambayo akujua madhara yake.
  Wazazi wawe makini na watoto wao
  Na huyo Mama naye chizi kweli ana watoto wote hao anakimbilia kulewa alifuata nini huko? Kuzaa watoo wengine wakati hawa ameshindwa kuwahudumia hadi anawakimbia? Alifuata mtarimbo? Alifuata starehe gani? Shiiiiiit!!!
   
 8. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,827
  Likes Received: 1,996
  Trophy Points: 280
  Nimesahau
  RIP Simon Joseph. Ulale salama. Umeondoka wakati ndio kwanza taifa linakuhitaji
   
 9. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 10. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Duu,this is serious.
   
 12. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  RIP Simon...
   
Loading...