Ajifungua mapacha: kila mtoto mmoja baba yake

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
TWINCE.jpg

Katika hali ya kushangaza, madaktari wamebaini kuwa mwanamke mmoja Jijini Hanoi, Vietnam amejifungua watoto mapacha ambapo alipata ujauzito wa pacha hao kutoka kwa wanaume wawili kwa nyakati tofauti.

Kwa mujibu wa CNN, familia ya mapacha hao ilianza kuwatilia shaka watoto hao kutokana na kutofanana kwao kwa kiwango kikubwa kama watoto wa familia mbili tofauti na ndipo ikawalazimu kuwaona wataalam wa afya ya uzazi kwa ufafanuzi zaidi.

Wataalam hao waliwafanyia vipimo vya vina saba (DNA) na kisha kubaini kuwa watoto hao hawakuwa wa baba mmoja.

Rais wa Genetic Association of Vietnam, Profesa Le Dinh Luong ambaye aliongoza jopo la madaktari kufanya utafiti kuhusu sakata hilo alibainisha kuwa familia hiyo ilishikwa na mshtuko baada ya kupewa majibu ya uchunguzi huo unaoonesha watoto hao hawakuwa wa baba mmoja.

Akizungumzia uzoefu wa kitabibu, Profesa Luong alisema kuwa hali hiyo inawezekana kutokea ingawa ni nadra sana kutokea, hususan pale ambapo mayai ya mwanamke anayeweza kutunga mapacha yatakapokuwa yamefikia katika hali ya kuanguliwa na kisha akashiriki mapenzi na mwanaume zaidi ya mmoja ndani ya muda mfupi.

Kwa sasa tunaamini kuwa mwanamke huyo alilala na wanaume wawili tofauti katika siku hiyohiyo ambapo mayai yake yalikuwa tayari na hivyo akatungwa mimba na wanaume wawili, japo hili linaweza kutokea bado ni tukio nadra sana.

Hata hivyo tukio hili sio la kwanza kuripotiwa kwani mwaka jana Mahakama ya New Jersey, Marekani ilintaka mwananume mmoja kumhudumia mmoja kati ya watoto mapacha baada ya ripoti za uchunguzi wa vinasaba kubaini kuwa mtoto mwingine sio wa kwake.
 
TWINCE.jpg

Katika hali ya kushangaza, madaktari wamebaini kuwa mwanamke mmoja Jijini Hanoi, Vietnam amejifungua watoto mapacha ambapo alipata ujauzito wa pacha hao kutoka kwa wanaume wawili kwa nyakati tofauti.

Kwa mujibu wa CNN, familia ya mapacha hao ilianza kuwatilia shaka watoto hao kutokana na kutofanana kwao kwa kiwango kikubwa kama watoto wa familia mbili tofauti na ndipo ikawalazimu kuwaona wataalam wa afya ya uzazi kwa ufafanuzi zaidi.

Wataalam hao waliwafanyia vipimo vya vina saba (DNA) na kisha kubaini kuwa watoto hao hawakuwa wa baba mmoja.

Rais wa Genetic Association of Vietnam, Profesa Le Dinh Luong ambaye aliongoza jopo la madaktari kufanya utafiti kuhusu sakata hilo alibainisha kuwa familia hiyo ilishikwa na mshtuko baada ya kupewa majibu ya uchunguzi huo unaoonesha watoto hao hawakuwa wa baba mmoja.

Akizungumzia uzoefu wa kitabibu, Profesa Luong alisema kuwa hali hiyo inawezekana kutokea ingawa ni nadra sana kutokea, hususan pale ambapo mayai ya mwanamke anayeweza kutunga mapacha yatakapokuwa yamefikia katika hali ya kuanguliwa na kisha akashiriki mapenzi na mwanaume zaidi ya mmoja ndani ya muda mfupi.

Kwa sasa tunaamini kuwa mwanamke huyo alilala na wanaume wawili tofauti katika siku hiyohiyo ambapo mayai yake yalikuwa tayari na hivyo akatungwa mimba na wanaume wawili, japo hili linaweza kutokea bado ni tukio nadra sana.

Hata hivyo tukio hili sio la kwanza kuripotiwa kwani mwaka jana Mahakama ya New Jersey, Marekani ilintaka mwananume mmoja kumhudumia mmoja kati ya watoto mapacha baada ya ripoti za uchunguzi wa vina saba kubaini kuwa mtoto mwingine sio wa kwake.
Maajabu mkubwa! na btw dna = vinasaba siyo vina saba ie ni neno moja. Usitenganishe!
 
Yaani umeisha mpiga kipa chenga ume place mpira unavuka mstari wa goli kisha jamaa nae anakuja kusisitiza ndo yanakuwa magoli mawili?wonders shall never end in this world.
 
Back
Top Bottom