Ajenti wa Korea Kaskazini akamatwa Australia

Ajenti wa Korea Kaskazini akamatwa Australia

Chillah

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2016
Posts
9,547
Reaction score
10,906
Ajenti wa Korea Kaskazini akamatwa Australia
  • _99239950_opbyahautarrest2.jpg
    Haki miliki ya pichaAUSTRALIAN FEDERAL POLICE HANDOUT
Image captionAjenti wa Korea Kaskazini akamatwa Australia
Mwanamume mmoja amekatwa kwa madai kuwa alikuwa ajenti wa biashara wa Korea Kaskazini, kwa mujibu wa polisi nchini Australia.

Chan Han Choi, 59, ameshtakiwa kwa kuwa dalali kwa mauzo yaliyo kinyume na sheria kutoka nchini humo na kuzungumzia biashara ya silaha za maangamizi makubwa.

Polisi wanasema kuwa amevunja vikwazo wa Umoja wa Mataifa na Australia.

Kesi dhidi ya Bw Chan ambaye ameishi Australia kwa zaidi ya miaka 30 ni ya kwanza ya aina hiyo nchini humo.

Picha za kombora jipya la Korea Kaskazini zinatuonyesha nini?

Bomu la Korea Kaskazini bado linatetemesha ardhi

Mwanajeshi wa Marekani aliyehamia Korea Kaskazini afariki

Korea Kusini yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

Ndiyo mara ya kwanza mtu yeyote amestakiwa chani ya sheria za mwaka 1995 za silaha za nchi hiyo za maangimizi makubwa.

Polisi wanasema kuwa kuna ushahidi kuwa Bw. Chan, amekuwa akiwasiliania na maafisa wa vyeo vya juu wa Korea Kaskazini.

Wanadai kuwa alihusika na kutoa huduma za kuuza mipango ya silaha ya Korea Kaskazini ikiwemo kuuza teknolojia ya makombora ya masafa marefu kwa mataifa ya kigeni, ili kuutafutia fedha utawala wa Korea Kaskazini.

Bw Chan pia ameshtakiwa kwa kuhusika na uuzaji wa mkaa wa mawe kutoka Korea Kaskazini kwenda nchini Indonesia na Vietnam.

Anakabiliwa na mashtaka 6 kwa jumla baada ya kukamatwa nyumbani kwake siku ya Jumamosi usiku.

_99239953_custody.jpg

Haki miliki ya pichaAUSTRALIAN FEDERAL POLICE HANDOUT
Image captionAjenti wa Korea Kaskazini akamatwa Australia

Chanzo: Ajenti wa Korea Kaskazini akamatwa Australia
 
unakumbuka Australia Alijifanya Ana Mdomo Sana Kuhusu N Korea Kim Akamwambia Atamshambulia Kwa Nyuklia Mama Yao Kuona Mtoto Anatishiwa Theresa May Akajibu Watajibu Kwa Nyukilia Iwapo Watatishiwa Na Rocketman Hapo Hapo Russia Akatishia Kuizamisha Greatbritain Ndiyo Ukawa Mwisho Wa Udaku
 
Kosa la mtu mwingine linawagharimu watu wengine.
Hiyo ni noma sana.
 
Kim Jong-Un na NK wako kila mahala.

Hata USA wenyewe wanamtambua dogo.
Maana financial institutions za USA (ndani) zimekuja kushituka mwezi wa September, 2017mwaka huu kuwa NK ina mzunguko mkubwa sana wa pesa ndani ya USA kwa zaidi ya miaka 30 bila USA kungundua.

Wameing'amua tu hivi karibuni.


Kwa kifupi, NK wako vizuri sema propaganda ni nyingi kuliko uhalisia wa mambo.
 
unakumbuka Australia Alijifanya Ana Mdomo Sana Kuhusu N Korea Kim Akamwambia Atamshambulia Kwa Nyuklia Mama Yao Kuona Mtoto Anatishiwa Theresa May Akajibu Watajibu Kwa Nyukilia Iwapo Watatishiwa Na Rocketman Hapo Hapo Russia Akatishia Kuizamisha Greatbritain Ndiyo Ukawa Mwisho Wa Udaku
[emoji23][emoji23][emoji23]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom