Ajari mbaya maeneo ya Riverside Dar

Siku hizi boda boda ndizo zinazoongoza kwa kuuwa watu! Kuliko ukimwi! Boda boda ni janga la wadanganyika
 
Mara nyingi wanalaumiwa madereva pale ajali zinapotokea,lakini ukweli ni kwamba watembea kwa miguu wengi ni wazembe na wanavuka barabara bila umakini wowote.
watu wazembe sana eneo hilo wanatembea as if wako bed room kwao....mi napasua mtu tu kama anavuka bila utaratibu
 
watu wazembe sana eneo hilo wanatembea as if wako bed room kwao....mi napasua mtu tu kama anavuka bila utaratibu
Mkuu inapaswa kuwa makini na kauli kama hizi. Kuna wenzio waligawa sanda...haikupita muda mrefu mauti ikawakuta. Kwenye ajali hamna utaratibu kiongozi...Angalia usije kupasuliwa wewe.
 

hayo ni mawazo yangu hayakuhusu...baki na ulokole wako niache niamini ninachoamini..lakini siwezi kupindua gari kukwepa mtu anayevuka sehemu isiyokuwa na zebbra cross...watanzania ni mbumbumbu sana kwenye mambo ya msingi na tumejaliwa kuongea ongea tu....what do u expect mtu anavuka barabara sehemu isiyo na zebbra cross? i just accelarate sio jukumu langu kumkwepa..
 
Hapa ndipo ninapomshangaa uumbaji wa mungu, aliumba watu wa aina mbalimbali hata wenye vichwa kama binadamu wengine lakini ubongo mdogo hata wa Mbu anayenyonya damu na kupasukia hapohapo ni mkubwa.

Niliwahi kuishi maeneo hayo takriban miaka 10, nimeondoka mwaka juzi tu, unaweza kumlaumu mtembea kwa miguu, lakini jamani tuwe wakweli, gari linaongozwa na binadamu huyo huyo, inakuwaje dereva aendeshe kasi bila tahadhari kwenye eneo analojua kama si watoto hata watu wazima huwa wanavuka ghafla.

Madereva tukumbuke hata sisi itatokea siku tutatembea kwa miguu iwe kwa kupenda au kwa lazima (wenye hekima watanielewa hapo).

Je na wale waliogongwa wakiwa kando ya barabara tena mmoja wapo ni mama lishe akiwa eneo lake la kazi njia panda ya Tegeta/Wazo ni uzembe, wewe unasema maneno ya dharau kumbuka hicho kidogo ulichonacho usijisahau ukafikiri umemaliza muombe sana Mungu akupe hekima ya kukitumia la sivyo leo unamgonga mwenzio kisa ni mzembe kesho yatakukuta yaliyomkuta Mafisango, Mtoto wa Dandu, Moshi Willy n.k wote hawakupenda kufa ila andiko lilitimizwa.
 
Ndugu yangu km umeweza kupost hapa JF kwa sinu ya mkononi basi fuata thread hiihii ya Ajari ui-highlight neno (iwe ndani ya kuuvuli cheusi halafu i-click)Replay itatokea ktk kibox maelezo ya yoyote uliyoya replay sasa yafute / delete andika yako ukifika mwisho ruka kiBox utakuta neno attachment na Managment attachment ya click mojawapo utaingia ktk memory ya cm yako hapo itafute hadi kwenye Device ukiiclick utahamia ktk Upload ikishajaa utaona neno Done click utarudi ktk box una send /submit replay km kawaidaAngalizo ni wenye sim za mkononi tu na lazima waende kwenye JF Mobile kwani Desktop angalau una uzoefuJamani ndo raha ya kuichangia JF wote tutakuwa waandishi /wapiga picha bila kuchujwa hata pori la wapi na ndo maana ALJAZEERA Ana-win taarifa za habari wakishachuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…