Ajari mbaya maeneo ya Riverside Dar

Binafsi leo nilikaribia kumgonga muendesha pikipiki maeneo ya Mwenge. Kama si kuchukua kwangu tahadhari, licha ya kuwa katika mkondo sahihi kwa mujibu wa sheria, tungekuwa tunazungumza mengine sasa hivi. Hawa waendesha pikipiki hawajui sheria, na wengine hujifanya wanajua sana kukatiza mbele ya magari yaendayo kasi. Bila kuwapa elimu ya usalama barabarani tutaendelea kupoteza watu wengi bila sababu.
 
Kaka nami nilikuwa kwenye gari nimeshuhudia yule dada japo c mkubwa sana akipigwa na gari.CHA AJABU YAKE BAADA YA DADA KUGONGWA NA GARI, WAMETOKEA VIJANA WATATU WAKACHUKUA MKOBA WAKE NA KUCHUKUA POCHI NA SIMU, CHA AJABU WAKAANZA KUNG'ANG'ANIANA NA MMOJA WAO KUFANIKIWA KUCHUKUA SIMU NA POCHI.Mama mmoja alipojaribu kupiga kelele wakamtishia.
NINAPICHA ZA MKOBA NA HAO VIJANA WAKING'ANG'ANIANA MKOBA NASHINDWA KU-UPLOAD KWENYE SIMU.
 
Guys, tukubali kuwa sio kila ajali ni uzembe wa mvukaji, kuna baadhi ya barabara hapa Bongo kama sio kurekebishwa vizuri ili zivukike bora viwekwe vidaraja, e.g eneo la kijiji cha Makumbusho, yaani ile barabara ilivyo pana na hamna pakupumzikia katikati yake, jioni ukivuka, ukifika upande wa pili inabidi ufute jasho kabla ya kuendelea na safari yako, yaani pamekaa tafrani tupu!
 
kwani Mbunge wenu mliemchagua hayupo kila kitu Serikali hata kuvuka barabara? Mm nawapa Pole wafiwa na RIP aliyegongwa

Hii imekaa kishabiki.

Kwani huwa mnalipa kodi kwa Mbunge?

Kwani Job description ya mbunge ina kipengele hicho cha ujenzi wa Public goods

Nadhani mnapaswa kuacha ushabiki na kuona vitu kwa uhalisia. Yeye anawatetea mpaka anafukuzwa bungeni na bado hamuoni!!!!
 
watu wazembe sana eneo hilo wanatembea as if wako bed room kwao....mi napasua mtu tu kama anavuka bila utaratibu

Mkuu umekosea sana. Unapaswa kufanya jitihada zote kuokoa uhai wa binadamu yeyote yule!
 
ruttashobolwa du we jamaa inaonesha ni jeuri au unatoka ikunga mang'ali a.k.a kijijini ambapo magari yakipita watu hushangalia ! "swala kama hili ambalo linamgusa kila mtu lakin bado unaona kama ni upuuzi ajari yaweza kumpata yeyote ndugu jamaa au rafik yako kwa kupeana taarifa kupitia jamiiforum yetu, ona binafsi nimepata somo zuri sana na kiukweli nasema asante kwa wote waliotoa mawazo yao! Viva great thinkers! May God be with long live! With succes!
 
Last edited by a moderator:
Kwa ile ajali kiukweli barabara ya ubungo to buguruni, pale magari yanaporuhusiwa 2 huwa yanaenda kwa kasi sana na ndiyo maana ajali hizi hutokea maramara.
 
daraja la manzese tusisingizie vibaka, watu haswa watz ni wagumu kufuata sheria, daraja la manzese watu hawataki kuvuka mpaka waliweka zile fensi kuwazuia watu wasivuke ovyo ovyo.
mpwa Kigogo nakuunga mkono, mi mwenyewe napasua tu BICHWA la mtu anaevuka kizembe na sisimami nduki nene 180kmph
 

Watu kama nyinyi ccm haiwatakagi. Kina malima na kina josefati ndio wanapendwa ccm
 
too bad nimepita hapo mida ya saa moja. mwez uliopita nilishuhudia kilema mmoja akiwa amegongwa eneo la ubungo mataa na kufa hapo hapo it was a bad day for me
 

pikipiki ni janga
 
too bad nimepita hapo mida ya saa moja. mwez uliopita nilishuhudia kilema mmoja akiwa amegongwa eneo la ubungo mataa na kufa hapo hapo it was a bad day for me

inalillah wainaillah rajiuun
 
watu wazembe sana eneo hilo wanatembea as if wako bed room kwao....mi napasua mtu tu kama anavuka bila utaratibu

Siku watapasua mama yako au mwanao ndipo utajuta kwamba ajali haina ajizi wala kujitapa, jifunze uuungwana kwani ukisimama au kupunguza speed utapungukiwa nini?

Labda kama huna ndugu wala jamaa wakupasuliwa. take care.......
 
Hizi boda boda zitatumaliza

Hapana si boda boda ni pick up mkuu. Pole sana mfiwa. Ila kusema ukweli hili eneo la Riverside madereva ni baru sana halafu kuna vituo vya daladala pale sasa nayo ni hatari nyingine watu huwa wanavuka mbele ya magari bila kuona vizuri magari yanayokuja na kwa kasi kiasi gani. Elimu ya kuvuka barabara ni muhimu sana ila Tanzania mambo mengi ni bora liende.
 
Watu kama nyinyi ccm haiwatakagi. Kina malima na kina josefati ndio wanapendwa ccm

Hahaha ha umenichekesha sana mkuu, mimi mwenyewe kwa kweli CCM siitaki, Ila ninapenda sana kuitumikia nchi yangu kwa uaminifu mkubwa sana whether iwe chini ya CCM au chama chochote kile. Tatizo la CCM ni ubinafsi. Haikawii utakuta mtu anaomba tenda ya kusimamia sheria ili penalty zote ziwe zake na yeye kulipia leseni tu.

Chukulia mfano wa TPS (Tanzania Parking System) wameikabidhi familia ya kigogo wa CCM ndiyo inakusanya mapato, wakati ile ni kazi ya halmashauri. Tenda ya kuzoa taka nayo wakabidhiana wenyewe, hizi zote ni nafasi za mapato. Tatizo la CCM watu wanaogopana nani amfunge paka kengere?. Ukileta pendekezo la kumuondolea mtu ulaji akikujua anakutumia hata majambazi yakumalize. Tunahitaji kuwa nchi ya kufuata sheria siyo kubembelezana kufuata sheria na kuogopa kulaumiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…