Ajali yauwa Arusha!!!

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,837
Watu wanne wamefariki dunia papo hapo na wengine 32 wamejeruhiwa ,baada ya basi la kampuni Polepole walilokuwa wakisafiria toka mkoani Arusha kuelekea mjini Babati mkoani Manyara kuligonga trekta, pikipiki ya magurudumu matatu na gari dogo aina ya Toyota katika eneo la Changarawe lililopo katika barabara kuu inayotoka mjini Babati kuelekea mkoani Arusha.
 
Loh! Hatari sana jamani. Na wale wote waliopatwa na mauti mwenyenzi Mungu awapumzishe kwa Aamani yake. Na hata majeruhi awape nguvu wapone mapema!
 
Habari mbaya sana hii!

Kibo10........ajali hii imetokea sehemu inayoitwa Changarawe.
Hebu niambie ni sehemu gani hii katika barabara ya Arusha Babati?

Copy kwa; PakaJimmy Mzee wa Rula Arushaone Preta marejesho Lily Flower Blaki Womani Mungi na Mtumishi Wetu ni eneo gani hili?

Watu wanne wamefariki dunia papo hapo na wengine 32 wamejeruhiwa ,baada ya basi la kampuni Polepole walilokuwa wakisafiria toka mkoani Arusha kuelekea mjini Babati mkoani Manyara kuligonga trekta, pikipiki ya magurudumu matatu na gari dogo aina ya Toyota katika eneo la Changarawe lililopo katika barabara kuu inayotoka mjini Babati kuelekea mkoani Arusha.
 
Last edited by a moderator:
Hii ajali imeniuma sana. Imemchukua kijana na rafiki yangu mmoja, niliyemfundisha kidato cha tano na sita mwaka 2008 na 2009 kule Babati.
Hapa ni kijana huyo, Daniel Chimbalambala (kulia) akiwa na rafiki yake aitwaye Charles ambaye pia amefariki katika ajali hiyo. Hivi hizi ajali zitaisha lini?

Dani.jpg
 
View attachment 125620

mwl Lubua jaribu tupe taarifa vizuri maana habari ijaonyesha mazingira vizuri, kuna treka, toyota ilikuaje?
 
Mungu awajalie afya njema majeruhi wapone haraka.

Pole kwa wafiwa
 
Back
Top Bottom