Ajali yasababisha nirudi JF kuomba msaada wa kazi

PRINCEBOY

Member
Apr 23, 2014
73
52
Heshima kwenu wakuu,

Naomba msaada wenu niweze kupata kazi maana nilipata ajali ya bodaboda nikiwa narudi nyumbani.

Nilishindwa kuendelea na kazi, nilikaa nyumbani muda wa wiki mbili.

Baada ya kupata unafuu nilimtafuta boss wangu lakini nilijibiwa kuwa tayari kuna mtu mwingine hivyo naomba msaada wenu wa kazi yoyote ile iliyopo wakuu.

Kwa umri wangu mimi ni miaka 26, elimu yangu ni form four. Nilihitimu mwaka 2012, naishi mkoa wa Mbeya.

Nina uzoefu katika kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

1. Kazi ya jikoni

Nimefanya hii kazi kwa mda mrefu hvyo naweza kuimudu vizuri. Kwa upishi wa vyakula mbalimbali pamoja na kukaanga chips mayai,kuchoma nyama n.k.

2. Kazi ya sales

Nimefanya hii kazi kwa vitengo viwili,
A.sales man/freelancer.

Nilikuwa katika mtandao wa simu wa MICTLTD unajulikana kwa jina la Tigo, hapa nilikuwa nasambaza laini, vocha, simu na moderm za internet.

Pia nilifanya settings katika simu zote za smartphone kwa wenye matatizo ya internet kwa sim zao.

B. Team Leader

Hapa nilifanya kazi katika mtandao wa halotel nikiwa kiongozi wa timu ya mauzo. Pia hapa nilihusika kutoa mafunzo kwa timu yangu ya mauzo ili wajue hatua na kanuni za mauzo kuwafanya wasikate tamaa wanapokuwa hawajapata wateja na kuwakumbusha kuwa mauzo ni dakika zote 600 kama ilivyo mpira dakika 90. Pia kuwa na lugha nzuri kwa wateja.

3.Mahesabu
Hapa nilifanya kazi katika maduka ya jumla ya vinywaji pamoja na yale ya vitu vya nyumbani katika kazi ya kupanua wigo wa biashara idara ya usambazaji pamoja na kufunga hesabu ya bidhaa kila jioni baada ya mauzo ili kujua kiasi cha pesa kilichotumika na kiasi kinachotakiwa kubaki (Cash in hand).

4. Lodge
Hapa nilifanya kazi kama mtu wa mapokezi kwa muda wa miezi 6 ambapo baadaye boss wangu alinipandisha na kuwa msimamizi/Manager wa ofisi yake ambayo pia ilikuwa na Restaurant na baa.

Naomba msaada wenu wakubwa, mbali na hizo kazi nilizo zitaja hapo nnao uwezo wa kufanya kazi yoyote ile ambayo ntapewa maelekezo kidogo na kuweza kuendelea mwenyewe kulingana na maelezo niliyopewa.

Sehemu yoyote naweza fika pia kuhusu swala la nauli ntahangaikia mwenyewe.

Kwa mawasiliano yangu ni 0712312205.

Asanteni wakuu.
 
Kwa mfano ikitokea upatiwa kazi sehemu fulani kulingana sifa zako utaweza kumlipa huyo mtu aliyekutafutia kazi kwa mapatano ya bei gani kila mwezi.
 
Kulingana na mshahara mkuu,au tunaweza kufanya mshahara wa mwezi wa kwanza ukachukua wewe mkuu
 
Kwa mfano ikitokea upatiwa kazi sehemu fulani kulingana sifa zako utaweza kumlipa huyo mtu aliyekutafutia kazi kwa mapatano ya bei gani kila mwezi.
Mkuu kama kazi unazo wewe tuingie mkataba tu niunganishe kazi utachukua share yako unayoitaji kwa makubaliano malumu hamna tabu
 
umejielezea vizuri kijana,kila la kheri,kuna watu wana degree lakini kuandika CV zao au kuweka tangazo hivi hawawezi

Watu wenye maelezo meengi namna hii huwa ni wajanja wajanja tu na si wafanyaji kazi.. yaani kwenye chips yumo kwenye gesti yumo halotel yumo tigo yumo kupika ugali yumo maandazi yumo.. halafu eti hana kazi!!!
 
Hongera mkuu, unajua kujieleza vizuri. Yani mim na ka elimu kangu ka pale zoom polytechnic sikufikii aisee
 
Kwa mfano ikitokea upatiwa kazi sehemu fulani kulingana sifa zako utaweza kumlipa huyo mtu aliyekutafutia kazi kwa mapatano ya bei gani kila mwezi.

Hayo malipo utakayolipwa na huyo uliomuunganishia kazi yatakuwa ni malipo pamoja na LAANA YA MUNGU utapokea

Utajikuta unapata matatizo na itakutoka hela mara kumi ya hio hela uliopewa kwa kula jasho la mtu
Kama huna msaada acha kutoa msaada
Usichukulie kigezo cha shida ya mtu ndio iwe kipato chako wewe
 
Mshahara ni rushwa unayopewa ili kusahau ndoto za maisha yako.
 
Attachments

  • Screenshot_2018-05-01-03-13-59.jpg
    Screenshot_2018-05-01-03-13-59.jpg
    42 KB · Views: 37
Sawa mkuu nashukuru kwa hilo,ila kumbuka kuwa na ujuzi wa kitu sikuwa na kazi,ujuzi kwanza kazi zinatafutwa huwezi kukaa tu nakushindwa kuomba kazi kisa tu maneno ya watu kama yako hayo,ila si mbaya kama mtu unaweza kulala nakuota ndoto kwaninini usile ulicho kiota?
QUOTE="kalagabaho, post: 26914721, member: 30674"]Watu wenye maelezo meengi namna hii huwa ni wajanja wajanja tu na si wafanyaji kazi.. yaani kwenye chips yumo kwenye gesti yumo halotel yumo tigo yumo kupika NN yumo maandazi yumo.. halafu eti hana kazi!!![/QUOTE]
Watu wenye maelezo meengi namna hii huwa ni wajanja wajanja tu na si wafanyaji kazi.. yaani kwenye chips yumo kwenye gesti yumo halotel yumo tigo yumo kupika ugali yumo maandazi yumo.. halafu eti hana kazi!!!
Watu wenye maelezo meengi namna hii huwa ni wajanja wajanja tu na si wafanyaji kazi.. yaani kwenye chips yumo kwenye gesti yumo halotel yumo tigo yumo kupika ugali yumo maandazi yumo.. halafu eti hana kazi!!!
 
Watu wenye maelezo meengi namna hii huwa ni wajanja wajanja tu na si wafanyaji kazi.. yaani kwenye chips yumo kwenye gesti yumo halotel yumo tigo yumo kupika ugali yumo maandazi yumo.. halafu eti hana kazi!!!
Exactly, you are correct. Sidhani kama ana hizo 'talents' alizoorodhesha hapo. Ana malengo tofauti Kwa kuwa ziko taarifa kwamba alipata ajira kwenye duka la jumla somewhere kwa malipo ya Tshs.240,000/- kwa mwezi na baada ya miezi mitatu akaondoka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom