Ajali ya Toyo yaua Mwinjilisti Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mwinjilisti wa Kanisa wa Kanisa LA Kilokole la AGT,William Lemomo mwenye umri wa Miaka 54 Mkazi wa Mswakini Juu ,wilayani Monduli,Mkoani Arusha amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongana na pikipiki nyingine


Tukio.hilo limetokea Jana majira ya SAA 12.30 jioni katika eneo la Makuyuni ,wakati mwinjilisti huyo akitokea kituo cha Mafuta kilichopo eneo hilo la Makuyuni kuweka mafuta na kuingia ghafla barabarani.


Kwa Mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ,Peter Lesangai Mkazi wa Kijiji cha Makuyuni, marehemu baada ya kuweka mafuta aliendesha pikipiki yake kuingia barabara kuu akielekea Mnadani .


Shuhuda alieleza kuwa Marehemu alikutana na pikipiki nyingine ikitokea upande wa kushoto ikiwa kwenye Mwendo kasi na kumgonga ambapo marehemu alianguka chini nakupata majeraha makubwa kichwani yaliyopelekea kuvuja damu nyingi na baadae kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospital ya wilaya ya Monduli alikokuwa amepelekwa kunusuru maisha yake


Shududa ameeleza kuwa Mwinjilisti huyu alikuwa amempakia muumini wake aliyetambulika kwa jina la Raymond Tukuyani (30) Mkazi wa Kijiji cha Naiti Ambaye naye alijeruhiwa vibaya na amelazwa katika hospital ya wilaya ,Monduli.


Wengine waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni dereva wa pikipiki iliyomgonga Marehemu iliyokuwa ikiendeshwa nadereva bodboda aitwaye Christopher Edward (24)Mkazi wa kijiji cha Naitory ambaye alivunjika Mguu na anaendelea na matibabu katika hospital hiyo ya wilaya huku Mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika chumba cha maiti Mto wa Mbu ukisubiri uchunguzi na Maziko.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'anzi amesema bado hajapata taarufa hiyo kwa kuwa alikuwa safarini ila ameahidi kufuatilia nankutoa taarifa kwa vyombo vya habari.


Hata hivyo kamanda Ng"anzi ameonya watumiaji wa pikipiki lazima wachukue tahadhali has a pale wanapokuwa wakitoka barabara za mchepuo kuingia barabara kuu .


[https://lh3]
 
Back
Top Bottom