Ajali ya Noah iliyoua yazua kasheshe

Ajali ya Noah iliyoua yazua kasheshe

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191

Watu wawili wamekufa na wanane kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Mwada na kuhusisha gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Magara kuelekea Magugu na Babati.

Aidha, ajali hiyo ilizua mvutano mkubwa baada ya wahudumu na maofisa wa kituo cha afya kugoma kupokea majeruhi wakidai wapewe fedha kwanza.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Deus Nsimeki, alitaja gari hilo kuwa ni T .728 CLV na kuwa dereva wake, Kazumba Musa aliyekimbia baada ya ajali hiyo, anatafutwa.

Alisema gari hilo lililokuwa na abiria kumi lilipinduka kisha kugonga mti baada na kuvutwa na mchanga.

Waliokufa ni Godlack Loshiye (25) na mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Angela.

Waliojeruhiwa ni Niko Demu, Maganga Sele, Rasuli Abdallah, Abdallah Mohamed, Edward Machel, Yuda Sanga, Lucia Francis, Paskalina Jovita, Saumu Hamisi, Anna Bernard na Tekla Leonard.

Katika tukio lingine, wauguzi na madaktari katika Kituo cha Afya Magugu walikataa kupokea miili ya marehemu na majeruhi wakidai kupatiwa Sh. 50,000 kwanza.

Hali hiyo ilizuwa tafrani kubwa kati yao na ndugu na jamaa wa marehemu pamoja na majeruhi, hali iliyoulazimisha uongozi wa Wilaya ya Babati Vijijini akiwamo Mkurugenzi Mtendaji kufika katika kituo cha afya.

Viongozi hao walikwenda kituoni baada ya kupigiwa simu na wananchi waliofika kutambua miili ya marehemu.

Mmoja wa wahudumu wa kituo hicho alidai mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Babati, Dominick Kweka, kuwa hawezi kushika damu ya mtu hadi apatiwe kitita walichokitaka Hali hiyo ilimkasirisha Kweka aliyefuatana na madaktari wa wilaya na kuamuru polisi kuwakamata wote waliyokataa kuwapokea majeruhi na kudai rushwa.

Pia aliamuru kukamatwa kwa nesi aliyekuwa amefuatana na wagonjwa wengine kwenda hosptali ya Dareda akamatwe baada ya kubainka kuwa aliwatelekeza wagonjwa baada ya kufika Babati mjini.

Chanzo: Nipashe
 
Hatari sana nchi hii kwani hawajapata mshahara hadi wadai pesa kwanza ndiyowahudumie wagonjwa?
 
Kuna baadhi ya wauguzi na madaktari walistahili kuwa katika kikosi cha mgambo wa jiji badala ya kazi wanazofanya hivi sasa
 
ukidharau la Escrow, hutolishangaa la hawa manesi wetu. Anajitolea kwa moyo wote halafu anasikia mafisadi wanapeta uraiani pamoja na ushahidi wote, kwa nini asijiulize mara mbilimbili uadilifu wake una maana gani? POLENI WAHANGA

Watu wawili wamekufa na wanane kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Mwada na kuhusisha gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Magara kuelekea Magugu na Babati.

Aidha, ajali hiyo ilizua mvutano mkubwa baada ya wahudumu na maofisa wa kituo cha afya kugoma kupokea majeruhi wakidai wapewe fedha kwanza.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Deus Nsimeki, alitaja gari hilo kuwa ni T .728 CLV na kuwa dereva wake, Kazumba Musa aliyekimbia baada ya ajali hiyo, anatafutwa.

Alisema gari hilo lililokuwa na abiria kumi lilipinduka kisha kugonga mti baada na kuvutwa na mchanga.

Waliokufa ni Godlack Loshiye (25) na mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Angela.

Waliojeruhiwa ni Niko Demu, Maganga Sele, Rasuli Abdallah, Abdallah Mohamed, Edward Machel, Yuda Sanga, Lucia Francis, Paskalina Jovita, Saumu Hamisi, Anna Bernard na Tekla Leonard.

Katika tukio lingine, wauguzi na madaktari katika Kituo cha Afya Magugu walikataa kupokea miili ya marehemu na majeruhi wakidai kupatiwa Sh. 50,000 kwanza.

Hali hiyo ilizuwa tafrani kubwa kati yao na ndugu na jamaa wa marehemu pamoja na majeruhi, hali iliyoulazimisha uongozi wa Wilaya ya Babati Vijijini akiwamo Mkurugenzi Mtendaji kufika katika kituo cha afya.

Viongozi hao walikwenda kituoni baada ya kupigiwa simu na wananchi waliofika kutambua miili ya marehemu.

Mmoja wa wahudumu wa kituo hicho alidai mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Babati, Dominick Kweka, kuwa hawezi kushika damu ya mtu hadi apatiwe kitita walichokitaka Hali hiyo ilimkasirisha Kweka aliyefuatana na madaktari wa wilaya na kuamuru polisi kuwakamata wote waliyokataa kuwapokea majeruhi na kudai rushwa.

Pia aliamuru kukamatwa kwa nesi aliyekuwa amefuatana na wagonjwa wengine kwenda hosptali ya Dareda akamatwe baada ya kubainka kuwa aliwatelekeza wagonjwa baada ya kufika Babati mjini.

Chanzo: Nipashe
 
Kuna baadhi ya wauguzi na madaktari walistahili kuwa katika kikosi cha mgambo wa jiji badala ya kazi wanazofanya hivi sasa

Hii ni matunda ya kupeleka watu kusomea hizi kazi kama kimbilio....Utasikia mzazi anasema-Mtoto tumehangaika kumpatia kozi aiyotaka imeshindikana...Tumefanikiwa kumpatia nursing.....
 
Mkuu SURUMA,

Nafikiri tatizo ni zaidi ya hilo, Nini maono yetu kama taifa, mfumo wa kuendesha nchi uko vipi?. Maana alisema marehemu Kabuye kuwa awali kuku walikuwa hawajisaidii wanapolala, lakini baada ya Jogoo kuanza kujisaidia wanapolala, vifaranga navyo vikaanza.
 
Hii ni matunda ya kupeleka watu kusomea hizi kazi kama kimbilio....Utasikia mzazi anasema-Mtoto tumehangaika kumpatia kozi aiyotaka imeshindikana...Tumefanikiwa kumpatia nursing.....

Kweli kabisa watu wanafanya kazi kwa ajili ya kupata mishahara wasijue kazi zingine ni wito kama unesi na ualimu
 
Tumefika huko kwa ajili ya utawala wa CCM. Kama DED anapuuzwa hivyo, je, mgonjwa wa kawaida mambo yangekuwaje?

Na hao wananchi nao sijui kwa nini wanakuwa wapole kiasi hicho? Walistahili kuwatia mkong'oto ili DED awakute wao ndo wanastahili kulazwa! Ushen.zy mtupu!!
 
Tumefika huko kwa ajili ya utawala wa CCM. Kama DED anapuuzwa hivyo, je, mgonjwa wa kawaida mambo yangekuwaje?

Wenye nchi wanapuuza wananchi. Sasa ni upanga kwa upanga. Za escrow wamechukua kila mtu anaina ni halali kudai rushwa. C C M majanga.
 
Back
Top Bottom