Natamani Mungu angekuwa anashuka at the moment pindi mtu hasa kiongozi mkubwa wa cnhi au idara unaudanganya umma,hivi ni kweli waliokolewa hai wanafika idadi hiyo,na je waliokufa ni idadi hiyo tu?kama ni hivyo manifesto iwekwe wazi mbona kama imepotea?na je meli ilikuwa imebeba tani ngapi za mzigo na je capacity ya meli ni kubeba tani ngapi?je Nani alisaini Meli kuondoka bandarini,nani aliifanyia ukaguzi kabla ya kuondoka?Je report za kitaaluma zinasema meli ilikuwa na tatizo gani kwa kipindi japo cha miezi mitatu ya nyuma na je ilipatiwa matengenezo?Je ilituwaamini hawa kwa siku zijazo wananchi na waathirika wote wa majanga makubwa haya tufanyaje?maana ya MV Bukoba,ya Treni pale Nsagali-karibia Dodoma na la MV Spice kutokea inamaana hakukuwa na fundisho lolote kwa matukio ya nyuma na mambo yaliendelea kufanyika kwa mazoea.Tuambie ukweli tujue watanzania wenzetu wangapi wamepoteza maisha,jamani wenzetu mlioko Zanzibar shirikianeni na walioko Pemba mjue ukweli wa ndugu waliofariki,wala msitumie JF kutoa habari zisizo rasimi semeni ukweli tutawaamini kuliko wenzetu wa Chama chetu na mwenzao B.