Ajali ya Bodaboda Ubungo Kibangu: Dereva na mama wafariki, mtoto apona

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,067
10,936
Wakuu, usiku wa kuamkia leo imetokea ajali mbaya sana eneo la Ubungo kuelekea Buguruni hapa njiapanda ya kuelekea Kibangu.

Bodaboda akiwa amebeba abiria mama na mwanae mwenye umri kama wa mwaka mmoja wamepata ajali, mama na bodaboda wamefariki ila mtoto amepona.
 
sio vizuri sana kutupia pic hapa ila kwa sababu umetupia ngoja tuziangalie tu
 
Hii si ni ile ya jana au? Khaa hizi boda zifutwe tu! Khaa! Muda wote ni viroba! Bora kupiga kwata ila si kuweka maisha rehani kwa hawa jamaa! Alaf utasema ajali haina kinga? ? Shame on them!!!
 
Hii si ni ile ya jana au? Khaa hizi boda zifutwe tu! Khaa! Muda wote ni viroba! Bora kupiga kwata ila si kuweka maisha rehani kwa hawa jamaa! Alaf utasema ajali haina kinga? ? Shame on them!!!
Hii ni nyingine, ile ya jana ilitokea pale shekilango. Naona bodaboda zinachinja kupita maelezo.
 
Kuna haja ya madereva wote wa Bodaboda kuchunguzwa akili zao kila baada ya miezi sita maana ni majanga jamani,ninachoshangaa mimi ni kuona watu wakizidi kuangamia kwa ajali za bodaboda na serikali ipo na hakuna jitihada za makusudi zikichukuliwa.
 
Nimefarijika sana kusikia ajali hii dereva wa bodaboda naye amepoteza maisha. Safi sana pole kwa wafiwa wa abiria, pole kwa mtoto mdogo anakatiziwa malezi ya mama na hawa wahuni wa bodaboda.

Ndugu zangu natowa wito najuwa changamoto za foleni na najuwa uwezo wetu kipesa ni mdogo, ila natowa ushauri ni vizuri tukawa na namba za simu za madereva wa bajaji angalau kidogo usafiri huu uko salama kiasi chake maana bajaj walau ina body na repoti za ajali za bajaji ni chache sana na hayajaripotiwa madhara makubwa yaliyotokana na bajaj, lakini bodaboda body ni mwili wako.

Tuanze sasa kuthimini uhai, bado Watanzania wengi hatujui thamani ya uhai mpaka tuone coffin.
 
Ushauri mzuri, bajaj ni salama mara mia zaidi ya hayo maboda. Kwanza wengi wamestaarabika, yani muendesha bajaj vs boda wanaonekana tofauti mara nyingi.
 
Hata dereva wa bodaboda akiwa ni mtu wa makamu wote wana tabia za kufanana tu...Kulazimisha kupita mahali ambapo hapafai kabisa, itokee dereva wa gari uwe makini tu utanue kidogo kusave life lake lakini wao hawajali kabisa....Abiria yabidi tuwe wakali usikubali kukimbizwa kimbizwa tu na hawa watu..
 
Ushauri mzuri, bajaj ni salama mara mia zaidi ya hayo maboda. Kwanza wengi wamestaarabika, yani muendesha bajaj vs boda wanaonekana tofauti mara nyingi.
Pamoja na kwamba kipato chetu ni kidogo lakini kukodi bajaj bado ni affordable, na kuna route nyingine bajaj wanalamba vichwa kwa jerojero na bukubuku.

Tukubali tu ukweli Watanzania wengi bado hawaijui thamani ya uhai, humo wapo madereva wa daradara, madereva wa bodaboda, madereva wa maroli na abiria wenyewe ambao hata umbali wa kilometer 1 tu siku hizi mtu hataki kutembea angalau hata mwili upate mazoezi, haya ni mazoea mabaya na ya kipuuzi mno.

Kwa mfano inashangaza mtu anakaa Ilala ati unamkuta kituo cha bus dakika 20 anasubiri usafiri wakati muda huohuo angeutumia kutembea na ile nauli angenunuwa karanga tu areflesh mdomo. Wabongo tuna tatizo kubwa la mindset.
 
Kuna ajali nyngne jana pia nimeisikia bodaboda na mwendo kas boda alitaka kuovatek akashidwa mtoto alifarik mama akapona kila mara wanaambiwa wasipite kwenye njia za mwendo kas jamaa hawaelew yaan bodaboda ni akil za viroba sana
 
Back
Top Bottom