Ajali Osaka

njokii

New Member
Nov 9, 2013
4
0
Habari wana Jf, mimi nipo njia moja kuelekea Ar, nimepata taarifa kuwa basi la Osaka Ar-DAR limepata ajali mbaya mbele kidogo ya same! Kama kuna mwenzetu amefika atujuze. Asante
 

mnhonya

Member
Mar 15, 2013
14
20
Jamani madereva wote naomba sana muwe makini wakati huu hasa wa sikukuu za mwisho na mwanzo wa mwaka, ndio maana ni vema kila bus kabla halijaondoka stendi pamoja na abiria wake kuchukua dakika angalau moja kumshukuru Mungu na kukabidhi safari mikono mwake. Tunawapa pole sana walioumia na ajali hiyo. Ikiwa kuna roho za kutoa watu kafara mwanzoni mwa na mwishoni mwa mwaka tunapiga kwa jina la YESU hakuna damu zaidi itakayomwagika kwa sababu ya kafara ama tambiko lolote, napiga kwa Jina la YESU WA NAZARETH zishindwe kabisa.
 

mnhonya

Member
Mar 15, 2013
14
20
Polisi wa usalama wa barabarani nisikilizeni! Huu sasa ndio wakati wa ninyi kufanya kazi kwa bidii na hasa hizo barabara za masafa marefu mikoani. Gari kama Hood ya Mbeya to Arusha, mabasi kama Ngorika ya Arusha Dar na hili la Mghamba la kwneda Mwanza Arusha, yaangalieni sana kwa umakini ninyi polisi wa Babati na Singida na Tabora, na hawa Polisi wa Pwani hapo Chalinze na Morogoro fanyeni kazi yenu kwa umakini sana ajali ni nyingi sana kagueni magari mpaka ndani, muwahoji abiaria kwenye vituo vya chakula wanaposhuka muwe mna mtu wenu pale ahoji abiria wanapoingia na kabla ya kutoka mwendo wa gari ukoje. watawaambia na toeni namba zenu za simu na wala sio ile namba ya mtu mmoja alieko ofisini Dar.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom