AJALI: Meli ya mizigo iitwayo HAPPY yazama eneo la Chumbe, Unguja ikitoka Dar kuelekea Zanzibar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,696
2,000
Meli ya mizigo iitwayo Happy ikitokea Dar es salaam kwenda Zanzibar imezama eneo la Chumbe, Unguja.

Taarifa zimedai kwamba Meli hiyo ilianza kuzama saa 10 alfajiri baada ya kuingiza maji ndani na kukosekana kwa vifaa kama motor ya kutolea maji hayo kufikia saa 1 asubuhi hii Meli hiyo iliendelea ilizama kabisa ndani ya maji.

Meli hiyo ilikuwa imebeba Dengu gunia 450 pamoja na Mbao zaidi ya 1000 huku wafanyakazi sita waliokuwa ndani ya Meli hiyo wakiokolewa.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ni meli ya mizigo mitupu na mabaharia mpaka sasa imeripotiwa kwamba wote ni wazima.
13502130_1070396369720352_3702524120513408319_n.jpg
13495064_500820163444320_103952615715841024_n.jpg

13529254_500820133444323_9094812653178131848_n.jpg
 

KANYAMA

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
964
2,000
Uoko
Taarifa za sasa hivi zilizonifikia ni kwamba, Meli ya mizigo iitwayo Happy ikitokea Dar es salaam kwenda Zanzibar imezama eneo la Chumbe, Unguja.

Taarifa zimedai kwamba Meli hiyo ilianza kuzama saa 10 alfajiri baada ya kuingiza maji ndani na kukosekana kwa vifaa kama motor ya kutolea maji hayo kufikia saa 1 asubuhi hii Meli hiyo ilizama kabisa ndani ya maji.

Inahofiwa baadhi ya watu wakiwemo mabaharia wa Meli hiyo wameshindwa kujiokoa, wamezama.
View attachment 360339 View attachment 360341
View attachment 360340
Uokoaji ufanyike haraka. Watanzania tuko nyuma sana katika Uokoaji. meli imezama tangu saa kumi na ukute Hakuna timu ya Uokoaji iliyofika eneo la tukio sitashangaa sana. Tuwaombee kwa mungu wahanga wote awanusuru na kila baya wakiwa Wanasubiri kuokolewa. Amen
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
25,037
2,000
Chumbe Halafu Inashindikana Kutoa Msaada Kwa Wakati? Nchi Hii Inakwenda Wapi Jamani
Kwa Mtu Aliyefika Unguja Anapajua Vema Hapo Eneo La Ajali Kwa Maana Umbali Hadi Unguja
 

hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
1,444
2,000
Poleni wote mliofikwa na kuguswa na janga hili.

Mungu awape subra na uvumilivu ndani ya kipindi hiki kigumu.
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,405
2,000
Marehemu gani hao wakati "...mpaka sasa imeripotiwa kwamba wote ni wazima." Acha kukurupuka.
kiongozi huu mwezi kwa wengine ni swaumu kali mno lakini pia wengine jana ilikuwa wkenda kwa hiyo kuingia chaka ni kama given hivi
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,405
2,000
Marehemu gani hao wakati "...mpaka sasa imeripotiwa kwamba wote ni wazima." Acha kukurupuka.
kiongozi huu mwezi kwa wengine ni swaumu kali mno lakini pia wengine jana ilikuwa wkenda kwa hiyo kuingia chaka ni kama given hivi
 

Mussolin5

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,398
2,000
Kikosi chetu cha Navy kiko wapi? Matukio kama haya ndio ya kujichukulia point.

Utayari wa vikosi vyetu kwa matukio kama haya ni mdogo sana.
 

Odili

JF-Expert Member
Feb 8, 2015
1,757
2,000
Intelijensia ya kuzuia wawakilishi kuongea na wananchi ingetumika kuzuia ajali kama hizi taifa lingesonga mbele kwa haraka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom