Ajali mbili Mandela Road...

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Kuna ajali mbili zimetokea barabara ya Mandela majira ya saa 5 usiku huu, moja maeneo ya Tabata Matumbi, ikijumuisha Semi-Trailer ya DAF na Starlet ndogo ambayo ni taxi, lori limehama njia na Starlet imekuwa nyakanyaka. Nilikuwa mu-daladala hivyo sikujua habari ya majeruhi wala maiti.
Nyengine imetokea maeneo ya Ubungo Gereji, lori moja limegonga jingine kwa nyuma!
Mwenye updates si mbaya akatuwekea!
 
Hakuna kitu kina nikosesha usingizi kama kuona scenes za road accident... I hope hakuna casualties...
 
Aisee. . .
Hopefully hamna waliopoteza maisha.

sidhani dada, labda kwenye ajali ya pili ya lori kwa lori. Ile ya lori na Starlet sidhani kama in'toka kapa, maana ki-Starlet kilikuwa nyakanyaka!
 
Hakuna kitu kina nikosesha usingizi kama kuona scenes za road accident... I hope hakuna casualties...

pole na hiyo accso-phobia! As I said earlier, sikuwa katika nafasi nzuri ya kujua kila kitu. Nadhani wenye updates watakuja...
 
tunaandaa matamasha tonatoa elimu lakini idadi ya ajali inaongezeka je raia hawaelewi somo je waelimishaji hawaeleweki? au barabara ni mbovu sana au magari tunayotumia ni vimeo..
pole wote mliopata ajili :A S embarassed:
 
Ajali haziwezi isha mpaka leseni sianze kutolewa kwa kuzingatia uelewa badala ya kuwa chanzo cha mapato kwa serikali na polisi. Kwa mfano mimi sijui hata kupiga start lakini nimetoa 150000 nikaletewa leseni ofisini. Ajali zitaishaje.
 
Back
Top Bottom