Jamani kwa mwenye taarifa kamili,nimesikia kuna ajali ya basi la NBS lililokua linatoka Dar kwenda Tabora.
=======
Basi la NBS linalotoka DAR kwenda TABORA limepata ajali mbaya maeneo ya Gairo Morogoro. Watu 4 wafariki na 10 kujeruhiwa katika ajali ya basi la NBS.
Huku ajali nyingine ya basi la KISBO likijeruhi watu kadhaa Morogoro. Basi la Kisbo T895CYL Limepata ajali ya kuparuzana na trailer flatbed eneo la Magubike Kilosa.
========
Updates;
========
Watu 5 wamefariki dunia na 35 wamejeruhiwa katika ajali ya basi mkoani Morogoro
Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine 35 kujeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya NBS lenye namba za usajili T909BXK lililo kuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Tabora kuanguka katika eneo la Tabu Hotel kata ya Chigela wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Mganga wa hospitali ya wilaya ya Gairo Mushi Mabula amethibitisha kupokea maiti tano na majeruhi 26 ambapo amesema watu saba hali zao sinzuri na watahamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Kwa upande wao mashuhuda wakiwemo majeruhi wa ajali hiyo wameeleza jinsi ajali hiyo ilivyotokea huku mashuhuda wakiwataka madereva kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro huku majeruhi wakilazwa katika hospitali ya wilaya ya Gairo.
Chanzo: ITV