Ajali Mbezi Magari Saba

Ajali Mbezi Magari Saba

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Kuna magari matatu yamegongana muda huu eneo la Mbezi Magari Saba. Lori moja lilikuwa na shehena kubwa mno ya "mapipa" kana kwamba kuna lami ndani. Kumbe si lami, bali ni shaba ya magendo. Baada ya kupinduka, mapipa yameanguka na kupasuka, ndipo siri hii imebainika.

Jamani, magendo haya yatakoma lini?
 
siku za mwizi ....................................................
 
Mambo ya M23 haya..mimi naona kwa kiasi flani hata Tanzania wanahusika katika kupora rasilimali za Congo wala siyo Rwanda na Uganda peke yake..natamani Congo wajitambue na wasimamie rasilimali zao kama Zambia walivyoweza..
 
Vijana hawajachangamkia kupata mali hapo? Maana hailipuki kama petrol ati. Ukiiba nawe jiandae kuibiwa!! Kula nawe uliwe -alisema mkuu wangu wa nchi siku anatoa hotuba yake bungeni pale alipugusa masuala ya epa eti kuna mtu alichoma utambi!!!! Ha ha ha!!
 
Hahahahaaaaa kwahiyo tutegemee watu wa Mbezi muda si mrefu au wkend hii wanajaa kwenye Bar zao...

Natumaini hakuna aliyepoteza maisha ? au hakuna alijeuriwa?
 
dereva atakuwa amefanya makusudi kuwaumbua mafisadi akaligongesha hilo lori ili vilivyojificha sirini vionekane hadharani
 
Mungu amewarejeshea mikononi waja wake rehema na mali walizoibiwa. Itakuwa ni ujinga wakiziacha zirudi tena mikononi mwa manyang'au. Akili kichwani.
 
majeruhi wapo?

Sidhani kama Prince Riz, vidili vidogo vigogo kama hivyo eti vya shaba anajishughulisha navyo. Yeye ni dhahabu na ana ready market, Barrick, ukiachana na ile nyingine anayotumia makontena chapa watu pamoja na ile ya clearing ya"flat rate per container" ya 10m anayoshirikiana na home shopping, ukiachana na hizi za Wawekezaji fake.
 
Vipi wale vibaka wanaoshinda sana maeneo ya Kwa Yusuph hapo na kule Luguruni hawajashtukia dili hilo wajitwaalie mzigo huo.
Maana cha magendo halali kuibwa hakuna wa kukushitaki hapo!!

Kuna magari matatu yamegongana muda huu eneo la Mbezi Magari Saba. Lori moja lilikuwa na shehena kubwa mno ya "mapipa" kana kwamba kuna lami ndani. Kumbe si lami, bali ni shaba ya magendo. Baada ya kupinduka, mapipa yameanguka na kupasuka, ndipo siri hii imebainika.

Jamani, magendo haya yatakoma lini?
 
Mungu amewarejeshea mikononi waja wake rehema na mali walizoibiwa. Itakuwa ni ujinga wakiziacha zirudi tena mikononi mwa manyang'au. Akili kichwani.

mkuu kitu cha magendo maana yake kimekwepeshwa kulipiwa kodi au tozo stahiki...haimaanishi kuwa kimekwapuliwa mahali
 
mkuu kitu cha magendo maana yake kimekwepeshwa kulipiwa kodi au tozo stahiki...haimaanishi kuwa kimekwapuliwa mahali
Kwani mkuu kutolipa kodi siyo wizi? Halafu bado wanatumia barabara tunazojenga kwa kodi zetu walalahoi.
 
Manyerere Jackton, haijalishi ni kwa kiasi gani lakini unaonyesha siku za mbeleni waweza kuwa nguli wa habari, nakukubali maana habari kubwa kubwa daima zinaanzia kwenye 'petty reporting' kama hizi.
Huyo jamaa namkubali sana tokea siku nyingi, na kama sikosei ndiye yule yule mwandishi wa makala nzito nzito.
 
Kwani mkuu kutolipa kodi siyo wizi? Halafu bado wanatumia barabara tunazojenga kwa kodi zetu walalahoi.

Yasome vizuri tena haya maneno yako ya mwanzo na uyatafakari kaka...nadhani utapata picha kwa nini nilikujibu vile pale juu...
Hakuna shaka yoyote kuwa kuiibia serikali mapato ni uizi, au kwa lugha nzuri zaidi huwa inaitwa kuhujumu uchumi

Mungu amewarejeshea mikononi waja wake rehema na mali walizoibiwa. Itakuwa ni ujinga wakiziacha zirudi tena mikononi mwa manyang'au. Akili kichwani.

Maandishi mekundu yanabainisha kabisa uliowalenga ni watu na sio serikali....zaidi umetabanaisha kuwa hiyo mali imeibwa.
 
Back
Top Bottom