Habari wapendwa katika Bwana
Kuna ajali imetokea Tazara karibia na mataa ya Tazara Bakhresa kuna binti amegongwa na Lori la mizigo. Kichwa chote kimesagika kwakuwa tairi zimepita kichwani hivyo kichwa kimetoka kabisa hivyo hajulikani. Polisi wamezuia kuchukua picha lakini alikuwa amevaa simpo nyeusi. Nguo hazitambuliki. Anaonekana kwa kukisia ni kama binti wa miaka 12-17 hivi.
Chanzo cha ajali alikuwa anajaribu kupanda daladala iliojaa kupita kiasi konda akamshusha kwalengo lakunguza abiria bahati mbaya akadondoka ndipo Lori likamkanyaga.
Kondakta kafanya unyama sana. Ila sina uhakika kama kakamatwa. Nimeuliza washuhuda wamekosa majibu sahihi.
Huyu dereva wa Lori hakusimama kabisa na huyu wa daladala hakusimama pia kwakuwa magari yalikuwa yameruhusiwa kwenye taa. Ndg watakaopotelewa na binti waende buguruni polisi kwa taarifa zaidi labda atakuwa ndugu yao. Pia kitu pekee chakumtambua marehemu labda mavazi maana kichwa hakipo kabisa yaani kama kachinjwa vile.Pole kwa wafiwa,
inasikitisha sana
Kuna kosa kwa dereva wa daladala hasa katika kupark hiyo daladala, lakn pia kwa konda ambaye aliamua kumshusha abiria sehemu isiyo stahili.
Wananchi hususan mashuhuda wa ajali hiyo wanaweza wakawa na walau chanzo kizuri cha kuikamata hiyo daladala ingawa kwa kweli si kawaida ya watanzania kunakiri namba za magari.
Konda achukuliwe hatua kwanini amfanyie dogo unyama kama huo na kumsababishia kifo, pole sana waliopatwa na msiba. Mtoto amaeamka salama kwenda shuleni jioni wazazi wanaletewa taarifa binti yao amepoteza maisha inasikitisha kwa kweli
Mimi nazani kama kuna abiria alikuwepo kwwnye hiyo daladala na anasoma Uzi huu na aliona hilo tukio muwakamate haraka sana hao wahusika kondakta na dereva wapelekwe polisi. Pia hata hilo Lori naamini kwa foleni ya Mandela road hata Ubungo halijafika kama kuna washuhuda wanalikumbuka Lori walifukuzie na bodaboda watalikamata.
Hata wakinakiri bado huwa hawajitokezi kutoa ushahidi unless kama ushahidi ungekuwa unatolewa bila kuonekana, ndo zetu hizi watz huruma machoni lakini ikifika kwenye kukamilisha zoezi ili huruma yako imsaidie mhusika unaogopa kutoa ushahidi. RIP mdadaPole kwa wafiwa,
inasikitisha sana
Kuna kosa kwa dereva wa daladala hasa katika kupark hiyo daladala, lakn pia kwa konda ambaye aliamua kumshusha abiria sehemu isiyo stahili.
Wananchi hususan mashuhuda wa ajali hiyo wanaweza wakawa na walau chanzo kizuri cha kuikamata hiyo daladala ingawa kwa kweli si kawaida ya watanzania kunakiri namba za magari.