Ajali mbaya sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali mbaya sana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 27, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Msiba wa mwaka watokea Dar, Lori lalalia daladala [​IMG] Lori la mafuta likiwa limelalia daladala aina ya Hiace katika ajali iliyotokea katika eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam jana kwenye barabara ya Morogoro na kusababisha vifo vya watu kumi papohapo. Hidaya Kivatwa na Julieth Ngarabali, Kibamba
  VILIO, simanzi na majonzi vilitawala jana eneo la Kibamba darajani, jijini Dar es Salaam ambako watu kumi akiwamo mama mjamzito walifariki dunia papo hapo baada ya lori la mafuta kuliangukia daladala.

  Watu watano waliokufa wametambuliwa na ndugu zao ambao waliwahi kufika eneo la tukio baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo.

  Waliotambuliwa ni Ester Paulo ambaye alikuwa mjamzito, Zainabu Alli, Abdultwalibu Twaibu, kondakta wa daladala hiyo ambaye amekatika kiuno Faraja Ngarambe na Shukuru Hussein, wote wakazi wa Kibamba, Dar es Salaam.

  Ni ajali ya kutisha ambayo kila mtu aliyefika katika katika eneo hilo alotokwa na machozi ama kupigwa bumbuazi kwani basi hilo la daladala aina Toyata Hiace maarufu kama kipanya, lilikuwa limefinyangwa na kuwa kama chapati, kiasi cha kutoamini kama kulikuwa na watu ndani yake.

  Mwandishi wa gazeti hili alipofika katika eneo la tukio kwenye saa mbili kasorobo asubuhi, alishuhudia umati wa watu waliofurika katika eneo hilo wakishangaa, huku wengine wakijaribu kutoa msaada.

  Asubuhi hiyo maiti wawili walitolewa katika gari hilo na kupakiwa kwenye gari la polisi na kupelekwa hospitali ya Tumbi Kibaha kuhifadhiwa.

  Mashuhuda wa ajali hiyo wali mweleza mwandishi huyo kwamba, ilitokea kwenye saa 10:30 alfajiri wakati lori hilo lililokuwa linasafirisha mafuta ya taa kutoka Dar es Saalam kwenda Lusaka Zambia kuacha njia na kuligonga daladala hilo uso kwa uso.

  Lori hilo lililigonga daladala hilo uso kwa uso na kulitumbukiza kwenye mtaro kisha kuliangukia kwa juu," alisema mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.

  Shuhuda mwingine Rashid Mfaume alisema: "Nilifika eneo la tukio majira ya saa 11 kasoro hivi na kukuta lori hili likiwa limelala juu ya daladala huku dereva wake akiwa ameshakimbia".

  Dereva mmoja wa gari la wanafunzi, Frank Msemwa alisema gari lake lilikuwa karibu na daladala hilo kabla ya kugongwa na kueleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya lori kuacha njia na kuligonga daladala hilo kwa mbele na kuliburuza hadi mtaroni.

  “Lori liliondoka kwenye njia yake kwenda upande lilikokuwa daladala. Likaligonga uso kwa uso na kulisukuma kurudi nyuma kama linaliburuza hadi kufikia kwenye mtaro huu ," alisema Msemwa.

  Mashuhuda wengine walidai kuwa ajali hiyo ilitokea wakati lori la mchanga aina ya Fusso lililotaka kulipita gari lililokuwa mbele na ghafla dereva alipoona kuna daladala mbele yake alirudi katika sehemu yake, ndipo dereva wa lori la mafuta lilokuwa nyuma, ili kukwepa kuligonga(fuso) akaenda upande wa pili na kukutana uso kwa uso na daladala hilo.

  Akizungumzia ajali hiyo jana, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga ambaye alifika eneo la tukio, alisema ajali hiyo ni mbaya kuliko zote zilizotokea jijini mwaka huu.

  Alidai uchunguzi umebainisha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa dereva wa lori la mafuta lililoacha njia na kwenda upande lilipokuwa daladala.

  “Ajali hii ni mbaya kuliko zote zilizotokea Dar es Salaam mwaka huu na kwa mtazamo imesababishwa na uzembe wa dereva wa lori hili kutokana na kuhama njia yake na kulifuata daladala," alidai Kamanda Mpinga.

  Kwa mujibu wa Mpinga, lori hilo lililokuwa limebeba mafuta ya taa kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka Zambia, linamilikiwa na Mahamud Mohamed na daladala hilo lilikuwa likifanya safari zake kati ya Mlandizi, Kibaha na Dar es Salaam.

  Alibainisha dereva wa lori hilo alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo na jeshi la polisi linamtafuta kwa kosa la kusababisha ajali hiyo.

  Mwandishi wa habari hii alishuhudia kazi ya kuondoa maiti waliyokuwamo kwenye daladala hilo ilivyokuwa ngumu kutokana na kupondeka na kufinyangwa kama chapati. Hadi saa 2:00 asubuhi maiti mbili tu ndizo zilizokuwa zimetolewa.

  Ugumu wa kazi hiyo pia ulichangiwa na uzito wa lori hilo lenye futi 40 lililokuwa limebeba tani 30 za mafuta ya taa kulilalia daladala hilo.

  Ugumu huo wa uokoaji ulililazimu jeshi la polisi kuomba gari nyingine ya mmiliki wa lori hilo kwa ajili ya kunyonya mafuta. Gari hilo lilifika eneo la tukio majira ya saa 2:30 asubuhi.

  Gari hilo pia lilishindwa kuliondoa lori hilo hadi polisi ilipoamua kukodi gari lingine la kuvutia lori kutoka kampuni ya BMK.

  Baada ya lori hilo kuinuliwa na kuanza kutoa miili katika daladala hilo, baadhi ya watu ambao ndugu zao walitambuliwa kuwemo walianza kulia akiwamo kijana ambaye mama yake alifariki.

  Wakati huo huo, jana jioni Kamanda Mpiga alilitaarifu gazeti hili kwamba, muda mfupi baada ya kushughulika kuondoa maiti na magari yaliyohusika ilitokea jali nyingine iliyohusisha magari mawili makubwa na ndogo aina ya Saloon kugongana, lakini hakuna mtu aliyekufa wala kujeruhiwa.

  Wakati huohuo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Kinondoni kimetuma rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa katika ajali hiyo.

  Aidha Chadema imetoa wito kwa serikali na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vyanzo vya ajali za mara kwa mara katika eneo la Kibamba ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

  Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kinondoni John Mnyika alitaja baadhi ya matukio ya ajali katika eneo hilo kuwa ni ajali iliyotokea Desemba mwaka 2007 maeneo ya Kibamba Hospitali na kusababisha vifo vya watu saba akiwemo mjamzito na wengine 11 kujeruhiwa.

  "Aidha mwezi Aprili 2008 Bunge lilielezwa kuwa jumla ya watu 181 wamepoteza maisha kwa kugongwa na magari kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2007 katika eneo la kuanzia Kibamba mpaka Ubungo kwenye mataa," alisema Mnyika na kuongeza:

  "Ikumbukwe pia Mei 2009 madereva wawili walikufa baada ya magari yao kugongana uso kwa uso maeneo hayo hayo ya Kibamba na Januari 2010 watu 18 walijeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Morogoro eneo la Kibamba Darajani,"


  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18764
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuweni tayari, kila dakika saa na sekunde!
  Poleni sana enyi muliokuwa nadani ya hiyo panya!
  Mlipata maumivu makali
  Lakini Mungu ndiye tumaini kuu!
  Amen.
   
Loading...