Kumetokea ajali ya basi la majinja lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Dar. Sababu ya ajali ni mwendo kasi wa basi la majinja ambalo lilitaka kulipita gari lingine ambapo walikutana na lori upande wa pili na kumlazimisha dereva kulipeleka gari porini kuepusha kugongana uso kwa uso na hivyo, basi kupinduka vibaya sana. Hakuna vifo mpaka sasa ila majeruhi zaidi ya 28 wamepelekwa hospitali ya Morogoro. Majeruhi zaid wanaendelea kupokelewa. Dereva wa basi amekimbia. Ajali imetokea morogoro mjini eneo la nane nane.
Chanzo. Radio one stereo breaking news.