Ajali!! Ajali!! Ajali!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali!! Ajali!! Ajali!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mutakyamirwa, Aug 10, 2012.

 1. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,872
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Kwa ujumla ajali zimekuwa nyingi na watanzania wengi wanaendelea kupoteza maisha. Viongozi wetu nahisi wamechoka sasa kutoa rambi rambi zao kwa wakuu wamikoa na familia husika ktk ajali hizo. Inavyoonekana jambo hili linakaribia kuonekana la kawaida kwa watanzania na serikali yao. Hivi hatuwezi kuona 'mtanzania mmoja hakifa kwa ajali ni wengi mno'! Kama sheria zipo ni kwanini hazitekelezi hili kuzuai ajali hizi; ni kwanini wantanzania hawana elimu ya kutosha kujilinda na kulinda maisha ya wenzio kiasi hiki! Ni nani hatusaidie kuondoa tatizo hili kama sio sisi wenyewe.

  Natoa rai kwa viongozi wa nchi hii-hali hii haikubaliki, chukua hatua. Watangazieni/waelimisheni watanzania-kupitia redio, tv na simu na njia nyingine mjuazo (hata zile mnazotumia kulinda usalama wenu) kuwa ajali hizi sasa mwisho! Inawezekana (jifunzeni kwa wenzenu wanaoweza kusimamia sheria)-Rwanda is a good example.
   
 2. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nchi imeoza kwa RUSHWA, mfano hii ajali ya Tabora waliofariki 17, majeruhi 76, ukijumlisha 93 bado ambao hawakujeruhiwa utagundua basi lilikuwa na zaidi ya abilia 100, wakati mabasi mengi uwezo wake ni abilia 66. Rushwa itatumaliza, katiba mpya walarushwa wanyongwe hadi kufa na sheria hiyo itekerezwe mara moja mtu anapohukumiwa, nadhani hii itakuwa tiba kwa ajali.
   
 3. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,836
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Sasa wewe Hushangai kwa nini polisi wana Vitambi?
   
 4. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mambo mengine kweli ni kukosekana kwa maadili na imani kwa wenye vyombo vya usafiri na polisi. Kwel inaingia akilini kwel kuona basi la abiria 65 linabeba 100??? Sheria inasemaje kwa polisi anayeruhusu basi la namna hiyo kupita ktk check point yake?? Hata hili tulaumu ukoloni???
   
 5. AMEND

  AMEND Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mapungufu haya yote bado ni wazi kwamba Watanzania wengi hawana elimu ya kutosha kuweza kujikinga na ajali za kuepukika hasa vijana na watoto. Kwa kuanzia na hili vifo vingi ni vya kuepukika.
   
Loading...