Aiyenacho hata kidogo hunyang'anywa

musa yasini

Member
Dec 15, 2020
28
36
Inasikitisha sana kuona wanasiasa wetu wanaojiita wazalendo, kuwa na malimbikizo na misururu ya marupurupu na posho starehe, kusinzia, kupiga meza na kupongezana kuchaguliwa tena, tena wakiwa hawakatwi kodi na baada tu ya muhula wao kwisha ,bila kuchelewa, wameshachukua chao.

TENA WANACHOTEWA HASWAA, huku kundi lingine la watumishi wa umma ndio limebebeshwa mimba inayosumbua sana yenye mlundikano wa kero, kuonewa,unyanyasaji,kodi, mikopo kandamizi, mishahara duni, kuzuiliwa kuhama na kukosa matumaini juu ya mambo yajayo. Huku ndiko kuna ile sheria ya kwamba ukifa kabla hujatimiza miaka miaka mitano hupewi hata elfu moja japokuwa kiuhalisia unakuwa umefikisha si chini ya milioni 5! Je huu si wizi?

Bado ni katika kundi hilihili ambako wapiga meza wanatamani kuwapangia MAKOKOTOOO! ili kuleta shida zaidi juu yao kana kwamba wao ndio walikuwa wanawatunzia hizo pension zao. AIBUUU! Miaka 60 ndio upewe pension halafu uipeleke wapi au ugawie ndugu na wajukuu? NONSENSE! Je, haya mambo hawayaoniii au wamefumba macho wasisikie? Laiti ingetokea nikawa mfalme Naapa ningewanyoorosha! HUU SI USAWA WALA SI UZALENDO ,TUNADANGANYANA !!
 
Ndiyo hawa hawa wanao tuhamasisha kwa maneno matamu tulipe kodi bila shuruti! huku wenyewe wakiwa hawalipi!
 
Ndiyo hawa hawa wanao tuhamasisha kwa maneno matamu tulipe kodi bila shuruti! huku wenyewe wakiwa hawalipi!
Ndio haohao wanaosisitiza vijana wajiajiri ingali wao ndio wenye mitaji na hawataki kuwaachia vijana hizo nafasi wao wwkajiajiri Ila vijananao wakusanye mitaji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom