Bingwaman
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 548
- 288
Kwa mara kadhaa katika siku za karibuni nimejiunga na kifurushi cha dakika 20 cha Airtel kwenda mitandao yote lakini nimeongea si zaidi ya dakika tatu na simu kukatika kwa maelezo kuwa kifurushi kimekwisha. Kibaya zaidi hata unapoangalia salio unakuta hakuna kitu. Kwa mfano, leo nilibakiwa na salio la shilingi 2,000 baada ya kujiunga na kifurushi, lakini nimezungumza dakika tatu tu na simu kukatika, eti kifurushi na salio vimeisha. Huu ni wizi wa wazi kabisa unaofanywa na 'Baba Lao', lakini mamlaka zetu tukufu ziko kimya. Nimeamua kuiweka sandukuni laini yangu ya Airtel.