AIRTEL wanatuibia bundle ghafla zinaisha.....ukipiga customer care inagoma

AIRTEL wanatuibia bundle ghafla zinaisha.....ukipiga customer care inagoma

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,739
Asubuhi leo mida ya saa mbile nimeweka bundle 400 lakini......muda huu hakuna kitu. Sijadownload vitu vingi wala nini zaidi ya kuperuz JF lakini nashangaa. Napiga huduma kwa wateja mtambo unapokea lakini hakuna kinachoongelewa ndo nini sasa. Yaani ukipiga 100 inalia shwaaaaaaaaaaaaaaa,

Meseji ya kwanza hii hapa

Name:
Number: 15444
Content:
Dear Customer. You have successfully received 400MB. To view your balance and expiry date, dial *154*44# and follow instructions. Thank you
Time: 25/04/2012 08:58:51

Baadae kidogo muda huo unajieleza

Name:
Number: 15444
Content:
Dear Customer .Your internet bundle has expired.To buy a new bundle,dial *154*44# and follow instructions.Thank you
Time: 25/04/2012 11:54:10

Wadau nisaidieni hapo.
 
Mkuu hiyo hata mimi ilishawahi kunitokea lakini wakaja kunirudishia kama siku 2 kupita.Lakini kipindi hicho sikuweka bundle tena nikitafakari siku naulizia balance mara nikaona zimerudi tena kwa hiyo wewe wakaushie uone.Sema kama kuna matatizo ya computer kujiupdate automatic baadhi ya program inaweza nayo ikawa tatizo.
 
Bundle ya 400MBs haipo tena ...vigezo na masharti kuzingatiwa!
Usipotoshe watu Mkuu, Bundle ya 400mb ndiyo ninayotumia mimi na ipo kama kawaida, ila nawashauri watu wawe wanatoa line wanaziweka kwenye simu na ndio unarecharge kwa njia ile ya zamani ya 15444, ukishapewa 400mb zako ndio unarudisha line kwenye modem.
 
Kaka bora umesema ukweli. mie nitawadai nielekezeni jinsi ya kuwadai
 
Mi nimeunga jana,natumia simu lakini hadi sasa natumia na nimeshatumia mb 2 tu! Kati ya mb400.
 
Delivery has failed to these recipients or distribution lists:
helpdesk@tz.airtel.com
The recipient's mailbox is full and can't accept messages now. Microsoft Exchange will not try to redeliver this message for you. Please try resending this message later, or contact the recipient directly.

nimewatumia mail haya ndo majibu
 
Kaka bora umesema ukweli. mie nitawadai nielekezeni jinsi ya kuwadai
Wapotezee tu utapoteza muda wako bure, mimi ni vocha ya voda ya shilling 50,000/= nilirechargre siku moja baada ya expire date ndio nikagunduwa nilichelewa nimekwenda ofisini kwao wakaniambia niingize baada ya siku 3 na msg ya namba ya ombi langu kushugulikiwa ninayo lakini huu ni zaidi ya mwezi hakuna, na nimeamuwa kusamehe.

Inshort makampuni ya simu Tanzania hayatoi huduma bali wapo kibiashara na isitoshe AIRTEL sasa hivi ni ya Wahindi hata Customer care namba ni ya kulipia na wamewapa kampuni nyingine kufanya hiyo kazi kwa niaba yao. kubali yaishe tu mkuu wajinga sisi Watanzania ndio waliwao.
 
Mkuu hio baada ya muda kidogo ulifanya nini.., isije ikawa ulikuwa unashusha mamovies ya kufa mtu..?

Anyway sio kwamba ninawatetea hawa jamaa ila siku hizi wapo slow sio kama zamani, alafu ile bundle ya DATAWIKI (3gb) kwa elfu 15 nadhani haipo tena :sad:
 
Ta muganyizi,walipokutumia hizo mb 400 na kukuelekeza jinsi ya kucheki salio ulicheki? Ulipaswa ucheki salio ije msg inayosema salio na muda wa kuexpire hizo MB.Pole rafiki
 
Ta muganyizi,walipokutumia hizo mb 400 na kukuelekeza jinsi ya kucheki salio ulicheki? Ulipaswa ucheki salio ije msg inayosema salio na muda wa kuexpire hizo MB.Pole rafiki

Dada nilicheki kila kiu na sio mara ya kwanza. Inabidi wajue kuwa hata kama wao ni wafadhili wa JF kuibiana sio dili na sio mara ya kwanza.
 
Dada nilicheki kila kiu na sio mara ya kwanza. Inabidi wajue kuwa hata kama wao ni wafadhili wa JF kuibiana sio dili na sio mara ya kwanza.

oops! Pole sana kweli inakera! Mimi niliweka before easter ika last week moja,juzi nimeweka nilipocheki salio ikaniambia muda wake utaexpire tar 23 may so hapa naskilizia! Wakiendelea hivyo watapoteza wateja maana haieleweki wala kuaminika tena!
 
Lakini dada hapo ukishusha episodes kama mbili za series au movie moja nadhani inaweza kuisha kwa usiku mmoja, cha maana ni kuangalia matumizi yako kama ni kweli yanamaliza 400mb, mimi sijawahi kukaa na 400mb mwezi mzima, ila mara nyingi ni matumizi yangu mwenyewe
 
Hawa jamaa ni wezi sana, halafu tena wanatangaza kuwa ukinunua nmodem mpya unatumia bure kwa miezi sita, siyo kweli ni wahongo na wezi watupu
 
bando ya 2500 yaani 400MB hapo awali ilikua inafika mwezi kabisa bila hata kuimaliza sasa hivi hata siku 10 haziishi kushney
 
tatizo la eatel ni kuwa bando zao ni limited so utumie kwa umakini. Voda ni unlimited. Mathalan ukinunua ya wk chezea unavyotaka
 
Back
Top Bottom