Airtel Mnatugombanisha!

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Kuna wakati unampigia ndugu,jamaa au mke unasikia simu inaita tu,ukienda kukutana naye anakwambia mbona simu ilikuwa imezima! Na mwingine hiyo line ya Airtel wakati huo haitumii na simu inaline nyingine lakini wewe mpigaji unasikia simu inaita hadi inakata yenyewe. Sasa kinachofuata ni ugomvi "kwanini napiga simu hupokei? Ulikuwa wapi?" Tatizo hili limenikumba mara kadhaa na kusababisha mitafaruku kabla ya kujua kuwa huwa Airtel wanatatizo hili.Nawaomba Airtel wajitazame marambili kwani malalamiko ni mengi ikiwa ni pamoja na kuibiwa muda wa hewani. Kwa mtu asiyemwelewa ndoa inaweza kuwa matatani baada ya simu kupigwa bila kupokelewa kumbe simu ilikuwa imezima kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom