Nilidhani hili tatizo linanikumba mimi tu. Nimeamua kuwapa likizo maana wamevuna sana hela zangu. Bora kwenda ambako bundle lina bei kubwa lakini ukiweka linakaa nanmakato angalau yanaendana nanhali halisi kuliko kuibiwa mchana kweupe.Airtel ni wezi sana wa MB. mwenyewe ni muhanga wa hilo..sa zile GB 5 kwa wiki ndo kabisa fasta zmeisha.
Na wameshaona ni sawa kutuibia na hatuna la kufanya. Inasikitisha TCRA kutosimamia vitu kama hivi vya msingi kabisa.Hilo ni tatizo kubwa, juzi wamechukua GB 1 Kama masihara nimejiunga usiku, nikazima data asubuhi natumiwa msg nimetumia asilimia 100 ya bundle. Hawa ni wezi. Selikali yetu Ina kazi ya kushughulikia kina Gigi money, inaacha haya majizi.
Nilipolalamika kuhusu hili hili Wiki iliyopita tu na Uzi upo hapa hapa JF mliniona kama vile nawasingizia na naongopa. Sasa tutaelewana vyema tu.Sijui kama kuna tatizo kwenye simu yangu au kuna tatizo kwenye mtandao wa Airtel. Leo nimenunua vifurushi vya internet vya thamani 1GB lakini havikuchukua hata masaa matatu vikawa vimeisha.
Nikiangalia matumizi sioni kitu ambacho nimekifanya cha kuweza kumaliza GB moja nzima ndani ya masaa matatu zaidi ya kuingia Jf na kusoma meseji Whatsap. Ukiwapigia wadada wa huduma kwa wateja wala hawana majibu ya maana zaidi ya kukuambia umemaliza bundle lako.
Nikiangalia kwenye simu sioni kama kuna updates zimefanyika ambazo zinaweza kumaliza hicho kifurushi.
Airtel kama mnaanza wizi wa namna hii jiangalieni sana na tambueni hii ni January watu tuko sensitive sana na matumizi. Hapa imebidi niachane nao nihamie mtandao wa Vodacom naendelea kutiririka tu; ka bundle ka buku lakini kamekaa muda kuliko ilivyokuwa kwenye bundle ya 1GB.
Tutawakimbia tulio wengi. TCRA waangalieni sana Airtel nahisi kuna kitu hakiko sawa leo.
Hao jamaa kazi yao kudukua mazungumzo ya wakosoaji tu.Na wameshaona ni sawa kutuibia na hatuna la kufanya. Inasikitisha TCRA kutosimamia vitu kama hivi vya msingi kabisa.