Kuna kitu kinatendeka kuhusu hii airtel internet.
Wao wamekuja na offer wanakupa 200mb free ukiongeza credit kabla ya saa 6 usiku, sasa cha kushangaza nimekuja kugundua kwamba ukiweka credit na ikifika saa 6 usiku na ukaanza kusurf basi kama ulikuwa na mb zako zilizokuwa kwenye (malipo ya bundles hasa ya 400mb) zinakatwa na badala yake wana weka hii offer ya 200mb ambayo pia ikifika saa 12 asubuhi balance ya mb inakatwa.
Hii mimi imenitokea mara mbili baada ya kutumia aidha kwa modem yao au hata kwa kutumia mobile phone kama modem, sijui kama kuna mwenzangu yeyote aliepata tatizo hili.
Labda cha kufanya hakikisha una balance ya mb zako za bundle kiasi gani kabla hujaanza kusurf kuanzia 6 usiku na ukimaliza pia ucheki kama zimebaki vilevile?[/QUOTE
Ndg yangu hilo limenitokea mimi pia zaidi ya mara tatu na hii yangu ni kali zaidi kwa kuwa ukiachilia mbali hiyo ya bonus ya mb 400 hela yangu iliyokuwamo kwe simu ikaliwa, huwa najiunga na bundle ya wiki ya shs 15000 na hela ya ziada inayokuwemo huw inaliwa pia, wizi ulioje airtel? nimejaribu kuongea na customer care kuhusu hili naishia kupewa namba ya kumbukumbu ya tatizo langu na kuambiwa tatizo linatafutiwa ufumbuzi nitapigiwa simu ("mpendwa mteja, tunashughulikia ombi lako, kumbukumbu no. yako ni 516477 tutawasiliana nawe hivi punde") haya ndo majibu yao hii ilikuwa ni tar 20/04/2011 nyingine ni kumb na 530247 ya tar 25/04/2011, hizi ni baadhi tu ninazo ahadi nyingi nilizoahidiwa kutatuliwa tatizo langu lakini bado nikijiunga na bundle hela yangu ya ziada iliyokuwamo inaliwa. Watanzania wenzetu mlioko kwenye airtel mtusaidie ndg zenu tunadhulumiwa, eneo nililopo napata airtel pekee unless ningekwisha hama zamani. Wewe unayejiita CCRAIRTEL humu JF una msaada gani ktk hili au ni kuweka matangazo tu humu jf ya ku-support dhulumati kwa watanzania wenzio? naomba unisaidie niweze kurudishiwa hela zangu zilizokatwa ilihali zimeshakatwa elfu 15 za bundle ya wiki.