Airlander 10: Ndege kubwa zaidi duniani tayari kwa kupaa angani

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Angani.jpg
Kampuni ya Kiingereza ya 'Hybrid Air Vehicles' imezindua ndege kubwa zaidi duniani ikiiacha ndege maarufu ya Airbus ambayo ndiyo ilikuwa ikishikilia rekodi kabla yake. Ndege hio ina uwezo wa kubeba tani nyingi za mizigo na imebuniwa kubaki angani bila crew tuliyoizoea ya kuendesha ndege kwa wiki tatu.

Kampuni hio imesema timu yake ya wahandisi inafanya matayarisho ya mwisho kuipeleka ndege hio angani na wanatarajia kuwa tayari kwa ajili ya kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu.

Wauzaji wanatarajia uimara na kujitegemea kwa ndege hio kutawavuta wanunuaji mapema. Kitabu cha rekodi cha dunia kinaenda kuweka nukuu nyingine kwenye uwanja wa teknolojia.

 
Dah safi sana aiseee.

Nafurahi sana kuona jinsi mataifa makubwa yanavyowekeza pesa nyingi katika project kubwa kubwa, sisi hapa kwetu hata ka-project ka kawaida tu hatuwezi.
 
Back
Top Bottom